Huyu mzee siyo fisadi isipokuwa anafikiria watu wote wako innocent kama yeye, hawezi ku-grasp kwamba sasa anatumika...yaani akili yake ni nzito kama kondoo inachukua muda mrefu sana kuelewa kinachoendelea...
Pinda dunia uwanja wa fujo bado uko usingizini unasafisha wasiosafishika
Hii serikali kwa ujumla imekosa mwelekeo, huyu kafanya hivi inamaana asomi magezeti? hawasikilizi wananchi? hajui RA na ufisadi wake? Nina wasiwasi anajua kuwa huyu RA ni best wake JK, na labda anataka kufurahisha bosi wake! Jamani hapa tulipofika ni hatari!! HE HAS TO GO!!Pinda Jiuzulu kazi imekushinda.
Alipoapishwa hapo juu aliapa kuilinda katiba na sio marafiki na Mafisadi papa.
Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni, alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu aliendelea kusema .......nafahamu mambo ya pale bungeni ni ya UZUSHI na UMBEA wala msiwe mnayasikiliza sana......kaazi kweli kweli
Watajiuzulu wangapi jamani?
Naomba kupata uhakika kama maandishi meusi paragraph ya mwisho yalitamkwa kweli na Mheshimiwa Waziri Mkuu au yameongezwa chumvi ili tutakapomsulubisha tumtendee haki.
Kama kweli ameyatamka hayo maneno hastahili kurudi tena bungeni lakini kama hakutamka hayo maneno lakini yamebandikwa hapo hatumtendei haki kwa kumlisha maneno.
Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni, alisema Waziri Mkuu.
Kwa hiyo haya ndiyo maneno mazuri kwako kutamkwa na waziri mkuu