Pinda Jiuzulu kazi imekushinda!

Pinda Jiuzulu kazi imekushinda!

Huyu mzee siyo fisadi isipokuwa anafikiria watu wote wako innocent kama yeye, hawezi ku-grasp kwamba sasa anatumika...yaani akili yake ni nzito kama kondoo inachukua muda mrefu sana kuelewa kinachoendelea...

Pinda dunia uwanja wa fujo bado uko usingizini unasafisha wasiosafishika

Fisadi ni fisadi tu ndugu yangu Tumain ila anajificha kwenye ngozi ya kondoo huwezi kusema wewe si jambazi kwa vile huwa huendi frontier wakati huo huo unakodisha bunduki yako ikatumike
 
Mh Pinda ametufanya sisi watanzania hatujuwi kusoma, pia amelifanya bunge kuwa kama ni mahali pakupiga porojo na sio mhimili ktk serikali.

Pinda anapaswa kuwajibishwa kwanza na vyombo vya usalama, either kwa maandish au kumfuata ofisini kwake na kumwambia ukweli.

Pia Bunge lenyewe via spika kwa kuzingatia maslahi ya Taifa kumuwajibisha.

Kitendo cha Mh Pinda kujikomba kwa Rostam Azizi ni sawa na mbwa kula matapishi yake. Pinda ameiaibisha serikali, bunge na hata cheo chake.

Rostam ni mtu anayepaswa kushtakiwa anytime from now na kutueleza ushiriki wake ktk kampuni Tata ya Richmond. Nahisi Pinda kaonyesha nidhamu ya woga na sasa analiaibisha taifa.

Nchi hii hatuogopi mtu mweupe wala mweusi, hatumuogopi mwenye fedha au asie kuwa nazo wote tupo sawa ktk sheria.

Tuache kuvaa miwani kwa wahujumu uchumi. Wafilisini na Mungu atalibariki hili Taifa.

Nimesikitika sana ukizingatia Pinda ni mwana usalama yani hata yeye anajikomba kwa Rostam?

Shame 4 real.
 
Bwana Tumaini! Kuhusu Rostam usiseme kabisa, acha kama hivyo hivyo ilivyo, I guess he is above the law. Yule ndio CCM kama ulikuwa hujui, yaani inatapisha, sometimes I ask myself what is wrong with these Government leaders; yaani ni kama wanaongea vitu bila kufikiria the consequences baadaye!

Mie Waziri Mkuu ndo kanichosha kabisa. Ee Mungu sikiliza kilio chetu na utupe busara za kufanya maamuzi yenye manufaa October 2010.
 
sisi wenyewe ndo tunajiharibia kwa nini tunawapigia kura hawa mabaradhuli CCM?
 
Inawezekana sisi kama nchi wa kulikomboa taifa hili kutoka kwenye haya makucha ya CCM hajazaliwa bado. Jinsi nilivyokuwa na imani na huyu bwana na mambo anayoyafanya binafsi amenifedhehesha sana, najuta hata kumfahamu.
 
Pinda Jiuzulu kazi imekushinda.


Alipoapishwa hapo juu aliapa kuilinda katiba na sio marafiki na Mafisadi papa.
Hii serikali kwa ujumla imekosa mwelekeo, huyu kafanya hivi inamaana asomi magezeti? hawasikilizi wananchi? hajui RA na ufisadi wake? Nina wasiwasi anajua kuwa huyu RA ni best wake JK, na labda anataka kufurahisha bosi wake! Jamani hapa tulipofika ni hatari!! HE HAS TO GO!!
 
“Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu aliendelea kusema .......nafahamu mambo ya pale bungeni ni ya UZUSHI na UMBEA wala msiwe mnayasikiliza sana......kaazi kweli kweli

Naomba kupata uhakika kama maandishi meusi paragraph ya mwisho yalitamkwa kweli na Mheshimiwa Waziri Mkuu au yameongezwa chumvi ili tutakapomsulubisha tumtendee haki.

Kama kweli ameyatamka hayo maneno hastahili kurudi tena bungeni lakini kama hakutamka hayo maneno lakini yamebandikwa hapo hatumtendei haki kwa kumlisha maneno.
 
Umaskini taaaaaaaabu tupu kweli jamani.
Nahisi ameahidiwa mifuko ya Mbolea ya Minjingu jimboni kwake Mpanda.
Ndo hapo mtakapo jua pesa ina nguvu kuliko utu.
 
Naomba kupata uhakika kama maandishi meusi paragraph ya mwisho yalitamkwa kweli na Mheshimiwa Waziri Mkuu au yameongezwa chumvi ili tutakapomsulubisha tumtendee haki.

Kama kweli ameyatamka hayo maneno hastahili kurudi tena bungeni lakini kama hakutamka hayo maneno lakini yamebandikwa hapo hatumtendei haki kwa kumlisha maneno.

“Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa hiyo haya ndiyo maneno mazuri kwako kutamkwa na waziri mkuu
 
pinda kapinda,
hana jipya kwa nchi,
na mimi nilishasema hii awam ikimaliza mda wake hata kama ni 2015
watalumiwa kuliko mkapa.na hawa ndo wanapaswa kupelekwa mahakamani, maana ushahidi upo wakati wakiwa madarakani
 
Huyu PM hamna kitu!
Hebu fikiria yeye kama mkuu wa mawaziri anashindwa kuwaamuru mawaziri wasinunue mashamgingi na kusema atamwambia rais awaagize mawaziri wasinunue mashangingi!
Magufuli akiwa waziri wa Miundombinu aliweza kuwafurumusha mawaziri na vigogo mpaka mashangingi yaliyokuwa ya mewekwa TZ na TX yakarudishwa lakini mtoto wa mkulima na uPM wake hawezzi!
 
“Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.

Kwa hiyo haya ndiyo maneno mazuri kwako kutamkwa na waziri mkuu

Ni bora kumuadhibu mtu kwa kile alichokisema kuliko kumuadhibu mtu kwa kosa asilolitenda.Maneno aliyoyaongea Pinda hayakubaliki kwa kuwa anajaribu kumsafisha fisadi aliyechafuka kwa maji taka.

Hakika fisadi hafai na huyo anayemsafisha pia hafai.
 
Amesema ukweli anaoujua. Bungeni kumejaa porojo nyingi. Wapiga kura wanaangalia mbunge wao kawafanyia nini sio kapiga kelele kiasi gani bungeni. Cha muhimu hapa "performance" tatizo la watu wetu ni kwamba wanapenda sana kusikia porojo na ubishani ambao hata tija kwa mpiga kura haina.
 
Bwana mkubwa Uhuru wa Inchi hii uko mikononi mwa Watu wachache, hao ndo wanaofaidi matunda ya Uhuru.Ndo hao wasio Guswa wala kutikiswa.Elewa tu, kwamba bado tuko Utumwani mpaka sasa.
 
Pinda ni UWT wasiwasi wenu nini kenda kukusanya maushaidi ye mwenyewe. Hapo anajua ni ngoma nzito mtoto hatumwi tungoje matokeo na ikawa kinyume na matumaini yangu 66 kushangaa maana hata RICHMOND kazimwa eti posho mbili zinachunguzwa.

Sijui nani anadanganywa na nani.

AKILI YA KAWAIDA TU yanambia posho mbili limezushwa ili kumzika RICHMOND. Mwakyembe alitangulia b4 upuuzi wao na laiti SIRI KALI ingeakuwa makini Hosea angekuwa pande yake inayomstahili then mrithi wake angeleta hiyo hoja mlazo.

Nchi imekumbatia MAFISI ADI tusikonde tushakuwa na PM mshiriki UFISI so natuwe wavumilivu tu.

Pinda anatafuta ufadhili ili apate UBUNGE nini tena
 
Michanga ya macho tu,lets wait and see...

Huku kuna habari kwamba kulikuwa na plot ya kum assasinate speaker wa bunge,wakati huo huo waziri mkuu anakuja na kusema mambo ya bungeni ni porojo,sasa lipi ni lipi?

Certainly maisha ya mtu kuwa hatarini kamwe si porojo....Haya mambo yote yawekwe wazi ili tujue nani tumwulize swali lipi nk.....Other than that ni kutuchanganya tu,nadhani ccm imegawanyika,kuna wenye kutaka mafisadi wasafishwe na wasiotaka.....

Eventually wananchi waende kuwachagua wenye kuonyesha kwa vitendo kuwa hawataki mambo ya kipuuzi ya kusafishana.Bali wanata haki itendeke....

Pinda keshaingia kwenye kundi la wapinda haki.
 
Back
Top Bottom