Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Hakuna hata takwimu, maana tunaenda kama nyumbani tu, ndio maana mie naona faida mojawapo ya muungano.
Muungano ukivunjwa itabidi tuwe na passport, ila sasa ni raha tu muda wowote unaamua tu kupanda boti na kwenda zako zenji.

I don't think many Wabara even care to go there in the first place
 
una maana WATANGANYIKA?

well, nadhani its about time wakaget a grip kuwa huu muungano hautodumu zaidi ya miaka 20 ijayo au less than that
 
Hakuna hata takwimu, maana tunaenda kama nyumbani tu, ndio maana mie naona faida mojawapo ya muungano.
Muungano ukivunjwa itabidi tuwe na passport, ila sasa ni raha tu muda wowote unaamua tu kupanda boti na kwenda zako zenji.

Muungano ni mzuri tu pale serikali zinapowajibika vizuri kwa Wananchi wake. Tatizo kubwa lililopo TZ, ni Umaskini unaosababishwa na viongozi wetu. Kwa mfano, angalia muungano wa USA unamanufaa kwa sababu serikali inawajibika vizuri kwa Wananchi wake; lakini muungano wa nchi za Soviet umevunjika kwa sababu ya serikali ilikuwa haiwajibiki ipasavyo. Kazi kwetu sasa WTZ.
 
If it were up to me this muungano would have been cut long ago..
 
So what's new over here? Z'bar can keep the oil if it wants wala sioni kwa nini iwe ishu, Baada ya mafuta wata tafuta kingine cha kulalamika.

To be sincere, Zanzibarians if want lets them keep their own Pemba and Unguja, and let Tanganyika keeps their Tanganyika. If it were Rukwa, Mbeya, Kigoma etc debating to depart I would react differently! There are so many things in this, which unless constitution is changed where position of Zanzibar and Tanganyika is looked again, and see the way we can enjoy equally the benefits of our mother counties, being socially economically to politically, the protest will always be there.
 
Kuyachukua mafuta ya Zanzibar ni ufisadi ,sasa jamaa wameshageuza adhabu baada ya kuona mnapiga makelele sana na hamuelewi,ndio wamepasua jipu kabisa ,kuwa waheshimiwa Muungano sasa Zanzibar hawauvinji tena ila mafuta ndio hayakabidhiwi ndani ya Muungano.

Kikwete kasema hayapo ,haina haja ya kugombana ,Pinda kasema watu wagawane mbao tuone ?

Ila jawabu kutoka Ikulu Zanzibar ndio hio Muungano hauvunjwi uwepo kama ulivyo lakini hili kopo la girisi msahau kama limo ndani ya Muungano.Kama ilivyokuwa dhahabu na Almasi hazimo hivyo na haya nayo hayamo ,sasa makelele ya nini na kutishana ?

So let me get this straight. Umesema Z'bar inaibeba Tanganyika. Pia ukasema Muungano unarudisha nyuma maendeleo ya Z'bar na pia kwamba Z'bar would be better off alone. Lakini bado kuvunja Muungano hamtaki? Kama nilivyo sema mwanzo Z'bar can keep it's oil. No point fighting over a venture which has not even made a single penny yet.
 
Wanzibar, wananichekesha kweli, kuamua hawako tayari. Hebu basi japo mwaka huu mjaribu kuamua. Kwakuwa nyie mna serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambayo haiitendi lolote lililo la muungano. Na kwa kuwa hata pale ambapo hata rais wa Zanzibar anahudhuria baraza la mawazi la muungano, kwenye masuala yanayohusu Tanganyika yeye huweka pamba masikioni, basi mwaka ujao na uwe wa kwanza kuteua wagombea wote wa nafasi za urais wa Zanzibar huko huko Zanzibar na sio kusikilizia chimwaga kama tulivyowazoea, msipoweza hilo, haya mengine mtayaweza je, wakati hamna rais wenu?
 
angalia matumizi ya maneno; niliisoma hiyo zamani sana na hakuna chembe ya objectivity zaidi ya hisia ya kuonewa na kuvunjwwa kwa ufalme mtukufu wa Sultani. Yaani, ni sumu kali ya machungu na kimsingi anawabebesha lawama kina Nyerere na Kanisa na kwa mbali kujaribu kutetea utawala wa Kisultani.

Hayo ni maoni yako kwani nawe si umo katika wale wenye kutekeleza ''Agenda za Siri''. Si, wewe ndio kuna siku ulijifanya hujui kwa nini Nyerere anataka kupewa ''utakatifu''? Jee, bado hujui kwa nini?
 
Last edited by a moderator:
Wale wakina nani? Ukweli uniume nini mimi? If Nyerere kweli alifanya mimi ina niponza vipi?

Ulitaka evidence japo ''circumstantial'' sasa unaanza ligi, utaiweza?
 
Last edited by a moderator:
not even close. Unless una mfano wa kuonesha nimemquote nikionesha bias.

Karibu 90% ya uliyoandika kumtaja JMK unaonyesha ulivyo biased nikianza ku -quote utaanza kurusha hapa, nakuahidi nta ku-quote.
 
Kama huu muungano utaendelea, inabidi aungaliwe upya kabisa, serikali 1, ili zanzibar iwe kama mkoa, au serikali 3 kama wengine wanavyopendekeza kila sehemu ichangie ipasavyo, na hapo muungano mnaoimba nao unavunjikia mbali mara moja. Vinginevyo, kwa sasa haya wanayosema mkataba wa muungano una mambo 12, inabidi kuanisha kuwa mambo hayo 12 yanaangukia katika waizara zipi, ili hata katika vikao vya bunge la muungano, wabunge wanaotoka upande wa Zanzibar wahudhurie vikao vya wizara husika tu.
 
not even close. Unless una mfano wa kuonesha nimemquote nikionesha bias.

Moja hii, unataka zingine?

Kikwete siyo safi! - yes I said it! Mzee Mwanakijiji
user_offline.gif
22nd October 2007, 07:07 PM
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/6534-kikwete-siyo-safi-yes-i-said-it-31.html#post539103
 
Tatizo WaTanganyika tumewabeba lakini vichwa na miguu inaning'inia.

Ndugu zangu, ninaushauri wa dhati kwa wabara na wavisiwani. Tusianze kutukanana, haitatusaidia. Tujadiliane na kama kweli hatuhitaji muungano basi tuuvunje, tuachane kwa amani. Baada ya muda tukiona umuhimu, najua tutauona kwa kuwa mke au mme anajulika uzuri wakati wawili wanopopeana taraka rejea, basi iwezekane kurudiana. Mimi niko pamoja na Pinda katika kumuomba Mungu siku moja nchi yetu iwe moja na yenye serikali moja. Na ninaomba hili litokee si kwa kulazimishana bali kwa kuelewana. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Ndugu yangu Dar-Es-Salaam,
Kushindana na wengine ni kama kumpigia guiter (gita) mbuzi. Wengine walishapigwa muhuri kwenye miyoyo yao na Menyezi Mungu, na wengine wamepigwa muhuri na Nyerere, huna vya kuwambia au kumkosoa Nyerere wakakubali. Na if you quote mwandishi yoyote yule (wa ki-islam) alioandika habari za ukweli madam kamkosoa Nyerere wao hawatamkubali. Hivi huyu Nyerere amewalisha nini hawa wa-jamaa ? Nani mwenye akili zake tamamu asiejua kua huyo Nyerere ndie mastermind wa 1964 mapinduzi ya serikali HALALI ya znz ? Namna Nyerere alivyokua hana raha na znz kwa uislam ulivyo nawiri alifika kusema kama ana uwezo angalivitia kamba visiwa hivi (unguja na pemba) akaviburuta mpaka katikati ya Indian ocean. Halafu huyo ndio mtakatifu. Si wakati huo alimpata Karume akamtisha kua usipoungana warabu watakupindua. Na mpaka hii leo kuna wapumbavu wanaosubutu kusema "vunja muungano uone vipi warabu watakavyowateka" Hebu neendeni huko Dubai na Omani baadae mpime maneno yenu kabla ya kusema. Kwa kina sisi tusio na uwezo wa kwenda tuwaulize wendao.
 
Z'bar wavunje muungano tu. Muungano wa Soviet umevunjika kwa sababu hakuna maendeleo yoyote yaliyotokea wakati wa Muungano. Z'bar wakivunja muungano wataendelea zaidi kuliko sasa hivi. Kazi kwao Wanazanzibar kudai independence yao.
natamani siku moja niamke asubuhi nikikute kisiwa hiki korofi kimejitenga.....na baada ya miezi mitatu watapiga kura ya kutaka kutawaliwa na UAE au Iran, huku wakiwatayari wamejiunga na OIC , baada vya miaka kumi Mungu akinijalia uhai nione hatua ya maendeleo watayokua wamepiga, maana kinachokera ni wao kudhani Tanganyika Tukufu inawanyonya,
Ni ndoto za umasikini zilizojaa ubinafsi kua wakipata mafuta wabara watafaidi,
TUWAACHE WAENDE ZAO , wadosi wanakisubiri kijikisiwa hicho ili wakinyonye na kukifyonza.
NENDA ZNZ USIGEUKE NYUMA, NENDA KAWASALIMIE KINA USSR, YUGOSLAVIA, NENDA UNGUJA NA PEMBA.
 
Naona viongozi wa Z'bar kuvunja Muungano au kuinitiate hiyo process wenyewe hawataki. Wana taka Serikali ya Muungano ndiyo ifanye hivyo ili wao wasionekane kufanya kosa. They are playing it safe. Ndiyo maana maneno kama ya Pinda yana waweka sehemu mbaya because it forces them to find a response. Na response zao kwa kawaida wata ponda ila mwishoni watasema lakini bado tuna utaka Muungano.

Rejea. Hata "Mapinduzi ya Zanzibar" ambamo SMZ inatokana, hawakuyafanya. Walisepa. Wakamwachia Tito Okello (Mganda) aliyejiita baadaye "field marshall" na genge lake, wakachapa kazi, wakamchimba mkwara Sultani mpaka akatema nchi. Jamaa hao wakakwea viboti, wakapiga makasia kurejea kisiwani, wakachukua "credit".

Talking, talking, talking cheap. Walete mswada kurekebisha vifungu vya katiba. Yaani wanapiga kelele ili Bara wawabadilishie vifungu.

Nimeshasema huko nyuma, kelele hizi ni gia za uchaguzi 2010. Ngoja upite. Kimyaa.
 
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi juzi wakati akifunga kikao cha Baraza la wawakilishi..
“Hatuna lengo la kuvunja Muungano Mheshimiwa Pinda ,isipokuwa afahamu pale watu wanapogombana ndipo wanapojua tatizo la kuimarisha maelewano,” alisema Dk. Mwinyihaji.


Hata hivyo, alisema kuhusu suala la mafuta na gesi asilia serikali ya Zanzibar imeshaweka msimamo kuwa suala hilo liondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano.
“Suala hili tumeshaliwekea msimamo wake na hatutarudi nyuma,hivyo kama akina Pinda na wenzake wanalirandia na kulinyemelea wasahau” alisema Waziri.
Ndio maana yake, mpo ?
Aradhi ya bara ni suala la Mungano wa si la Muungano?
 
Kama huu muungano utaendelea, inabidi aungaliwe upya kabisa, serikali 1, ili zanzibar iwe kama mkoa, au serikali 3 kama wengine wanavyopendekeza kila sehemu ichangie ipasavyo, na hapo muungano mnaoimba nao unavunjikia mbali mara moja. Vinginevyo, kwa sasa haya wanayosema mkataba wa muungano una mambo 12, inabidi kuanisha kuwa mambo hayo 12 yanaangukia katika waizara zipi, ili hata katika vikao vya bunge la muungano, wabunge wanaotoka upande wa Zanzibar wahudhurie vikao vya wizara husika tu.
 
Kwa wale ambao wanajua undani wa Muungano, uliosukwa na kusukika, hatimaye nchi mbili tofauti, Zanzibar na Tanganyika, zikaungana na kuwa nchi moja, Tanzania, mnamo mwaka 1964, mtajua wazi kwamba Muungano huu ulikuwa na lengo moja tu: KUILINDA ZANZIBAR dhidi ya hatari za mashambulizi ya kuvamiwa tena, na kuwa chini ya Falme za Kisultani.

Muungano huu haukuwa na faida kwa Tanganyika, kwani, hata tukiangalia Uchumi wa Zanzibar, pamoja na rasilmali zake zote, hakukuwa na (zaidi ya karafuu) zao hata moja ambalo lingeweza kusaidia kipato cha Serikali ya Muungano. Na kweli, Zanzibar, toka "iungane" na Tanganyika, imekuwa ikifaidi ruzuku kutoka Serikali ya Muungano.

Mengi (yaliyofichwa) yaliandikwa kwenye Mkataba wa Muungano, ambao mpaka leo unafanywa kuwa SIRI. Watanzania tujiulize. Hivi, kwenye "maslahi ya taifa", sisi wote tukiwa ndio wenye TAIFA, kuna SIRI ambayo hatupaswi kuijua? Hiyo SIRI imewekwa kwa manufaa ya NANI haswa?

Nawakumbuka wale WAJINGA waliotaka tuwe na Serikali tatu; Serikali ya Muungano, Serikali ya Tanganyika, na Serikali ya Zanzibar. Watu wa ajabu sana wale! Wa ajabu kweli kweli! Hivi, ka-nchi kadogo kama haka, kawe na Serikali tatu, itawezekana kweli? Yaani, tuwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Tanganyika, na Rais wa Zanzibar? Halafu tuwe na Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika na Bunge la Zanzibar? Halafu tuwe na Baraza la Mawaziri la Muungano, la Tanganyika, na la Zanzibar? Halafu tuwe na Wabunge, wa Muungano, wa Tanganyika, na wa Zanzibar? Itawezekana kweli, kama si ujuha, upumbavu na UHUNI?

UHUNI? Ndio! Ni UHUNI kudai Serikali tatu! Uhuni mkubwa uliokithiri na kuvuka mipaka yote ya ustaarabu.

Nchi ya watu, takriban milioni 40, ambao asilimia 70 ya watu wake ni maskini, wanaoishi vijijini. Watu hao hao, uwalipishe ushuru na kodi lukuki, kukidhi haja za Serikali tatu? Kama si uhuni, sijui ni nini?

Tuzungumzie hali halisi iliyopo kwa sasa.

Serikali mbili... nchi moja! Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nnini maana ya Muungano? Kwa nini kuwe na Serikali mbili, ndani ya NCHI MOJA? Ndani ya Muungano kuna Watanzania, hakuna Watanganyika wala Wazanzibar. Nje ya Muungano kuna Watanganyika na Wazanzibari. Ndani ya Zanzibar, nje ya Muungano, kuna Wazazibara na Wazanzibari. Ndani ya Zanzibar, nje ya Muungano, kuna Waunguja na Wapemba! Mnayaona haya?

Serikali mbili... nchi moja! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Haiitwi Jamhuri ile. Inaitwa Zanzibar, basi! Si Jamhuri! Anayesema inaitwa Jamhuri ya Zanzibar aje na waraka huo uliopitishwa kisheria. Kimsingi, ZANZIBAR SIO NCHI! Zanzibar ni MKOA, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndio maana tunasema Tanzania ina MIKOA ishirini na sita, mkoa wa mwisho ukiwa Zanzibar, ambao, ndani ya Jamhuri una Wilaya zake zinazotambulika!

Serikali mbili... nchi moja! Bunge la Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Baraza la Wawakilishi (na Wabunge?) la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

KICHEKESHO (au KILIO? Chagua moja!): Ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania, kuna Wabunge wa Jamhuri na Wabunge wa Zanzibar. Wote wanapigiwa kura.... kwa hiyo, Majimbo ya Ubunge ya Zanzibar yanatambuliwa rasmi kwenye Bunge, ndio maana yanasimimamiwa (wakati wa Uchaguzi) na (hiki ni KICHEKESHO zaidi) Tume ya Uchaguzi Zanzibar. Yaani, Zanzibar ina Tume ya Uchaguzi, ambayo baadhi ya watendaji wake wako kwenye Tume ya Taifa (Jamhuri) ya Uchaguzi. Mpo hapo? Tume mbili, nchi moja. Majimbo yanatambulika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Jamhuri), na pia yanatambulika huko Zanzibar. Lakini (KICHEKESHO ZAIDI) sijaona, sijasikia, Mbunge wa Jamhuri akaingia kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kuiwakilisha Jamhuri! Hilo HALIPO! Ila, wao wanaingia kwenye Bunge la Jamhuri! Nadhani mmenielewa!

Haya. Turudie.

Rais wa Jamhuri. Rais wa Zanzibar.
Bunge la Jamhuri. Bunge la Zanzibar.
Baraza la Mawaziri la Jamhuri. Baraza la Zanzibar.
Wabunge wa Jamhuri. Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar.
Serikali ya Jamhuri. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Jeshi la Polisi la Tanzania. Oh, hakuna Jeshi la Polisi la Zanzibar.
Jeshi la Wananchi la Tanzania. Oh, HAKUNA Jeshi la Wananchi la Zanzibar.
Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri. Oh, LIPO Jeshi la Kujenga Uchumi la Zanzibar (JKU).
Oh, HAKUNA Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo cha Jamhuri. Oh, lakini KIPO Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) cha Zanzibar.

Tathimini yangu?

Muungano huu haufai. Ni bora tuwe na Serikali Moja! Yeyote yule aliyeko Zanzibar aweze kugombea nafasi yoyote ile kwenye Uongozi, ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sitaki, sioni haja ya kuwa na Serikali Mbili ndani ya Muungano. Hakuna faida wala haja. Serikali moja. Hakuna haja ya kuwa na Bunge la Jamhuri na Baraza la Wawakilishi. Ina maana kwamba kuna Sheria za Muungano na Sheria za Zanzibar? Sasa nini haswa faida na haja ya kuwa na Muungano?

Tuache unafiki, tuanze kuambizana ukweli.

Kama Zanzibar haitaki Muungano, basi, wapige kura ya maoni kujitoa. Wakijitoa, vikosi vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi viondolewe mara moja huko Zanzibar. Vijana wetu warudi nyumbani! Kama hawataki Muungano, tunafuta mara moja ruzuku wanayoipata kwenye Bajeti yao. Mamlaka ya Mapato ya Tanzania ifunge virago vyake huko Zanzibar. Ukitaka kwenda Zanzibar, unagonga passport yako, unalipia VISA kama vile unakwenda nchi nyingine. Na wao pia, wakija Tanzania, walipie VISA. Wazanzibari wote waliopo Tanzania bara waombe na kulipia vibali vya makazi. Ndicho wanachokitaka?

Tuache unafiki, tuambizane ukweli.

Serikali Moja! Nchi Moja! Bendera Moja! Wimbo MMOJA wa Taifa.

Hakuna Bendera ya Jamhuri kisha kuna Bendera ya Zanzibar. Hakuna Wimbo wa Taifa kisha kuna Wimbo wa Taifa wa Zanzibar! ZANZIBAR SIO NCHI!

Namuunga mkono kwa dhati kabisa, Waziri Mkuu, Mhe. Pinda Peter Mizengo Kayanda, kwamba, SERIKALI IWE MOJA, kwani hii ni NCHI MOJA, inayojulikana kwa jina la, JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

IDUMU JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
MUNGU WABARIKI WATANZANIA NA VIONGOZI WAKE!
MUNGU TULINDE WATANZANIA!
MUNGU TUEPUSHE NA UFISADI!

./Mwana wa Haki

P.S. Bado nitaendelea kusema. Mwenye kukerwa, aende kujirusha FERI! Au Bahari ya Hindi kama Magogoni hapatoshi!
 
Back
Top Bottom