Babylon
JF-Expert Member
- Feb 5, 2009
- 1,332
- 83
- Thread starter
- #321
Kwa wale ambao wanajua undani wa Muungano, uliosukwa na kusukika, hatimaye nchi mbili tofauti, Zanzibar na Tanganyika, zikaungana na kuwa nchi moja, Tanzania, mnamo mwaka 1964, mtajua wazi kwamba Muungano huu ulikuwa na lengo moja tu: KUILINDA ZANZIBAR dhidi ya hatari za mashambulizi ya kuvamiwa tena, na kuwa chini ya Falme za Kisultani.
Muungano huu haukuwa na faida kwa Tanganyika, kwani, hata tukiangalia Uchumi wa Zanzibar, pamoja na rasilmali zake zote, hakukuwa na (zaidi ya karafuu) zao hata moja ambalo lingeweza kusaidia kipato cha Serikali ya Muungano. Na kweli, Zanzibar, toka "iungane" na Tanganyika, imekuwa ikifaidi ruzuku kutoka Serikali ya Muungano.
Mengi (yaliyofichwa) yaliandikwa kwenye Mkataba wa Muungano, ambao mpaka leo unafanywa kuwa SIRI. Watanzania tujiulize. Hivi, kwenye "maslahi ya taifa", sisi wote tukiwa ndio wenye TAIFA, kuna SIRI ambayo hatupaswi kuijua? Hiyo SIRI imewekwa kwa manufaa ya NANI haswa?
Nawakumbuka wale WAJINGA waliotaka tuwe na Serikali tatu; Serikali ya Muungano, Serikali ya Tanganyika, na Serikali ya Zanzibar. Watu wa ajabu sana wale! Wa ajabu kweli kweli! Hivi, ka-nchi kadogo kama haka, kawe na Serikali tatu, itawezekana kweli? Yaani, tuwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Tanganyika, na Rais wa Zanzibar? Halafu tuwe na Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika na Bunge la Zanzibar? Halafu tuwe na Baraza la Mawaziri la Muungano, la Tanganyika, na la Zanzibar? Halafu tuwe na Wabunge, wa Muungano, wa Tanganyika, na wa Zanzibar? Itawezekana kweli, kama si ujuha, upumbavu na UHUNI?
UHUNI? Ndio! Ni UHUNI kudai Serikali tatu! Uhuni mkubwa uliokithiri na kuvuka mipaka yote ya ustaarabu.
Nchi ya watu, takriban milioni 40, ambao asilimia 70 ya watu wake ni maskini, wanaoishi vijijini. Watu hao hao, uwalipishe ushuru na kodi lukuki, kukidhi haja za Serikali tatu? Kama si uhuni, sijui ni nini?
Tuzungumzie hali halisi iliyopo kwa sasa.
Serikali mbili... nchi moja! Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nnini maana ya Muungano? Kwa nini kuwe na Serikali mbili, ndani ya NCHI MOJA? Ndani ya Muungano kuna Watanzania, hakuna Watanganyika wala Wazanzibar. Nje ya Muungano kuna Watanganyika na Wazanzibari. Ndani ya Zanzibar, nje ya Muungano, kuna Wazazibara na Wazanzibari. Ndani ya Zanzibar, nje ya Muungano, kuna Waunguja na Wapemba! Mnayaona haya?
Serikali mbili... nchi moja! Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Haiitwi Jamhuri ile. Inaitwa Zanzibar, basi! Si Jamhuri! Anayesema inaitwa Jamhuri ya Zanzibar aje na waraka huo uliopitishwa kisheria. Kimsingi, ZANZIBAR SIO NCHI! Zanzibar ni MKOA, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ndio maana tunasema Tanzania ina MIKOA ishirini na sita, mkoa wa mwisho ukiwa Zanzibar, ambao, ndani ya Jamhuri una Wilaya zake zinazotambulika!
Serikali mbili... nchi moja! Bunge la Muungano wa Jamhuri ya Tanzania. Baraza la Wawakilishi (na Wabunge?) la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
KICHEKESHO (au KILIO? Chagua moja!): Ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania, kuna Wabunge wa Jamhuri na Wabunge wa Zanzibar. Wote wanapigiwa kura.... kwa hiyo, Majimbo ya Ubunge ya Zanzibar yanatambuliwa rasmi kwenye Bunge, ndio maana yanasimimamiwa (wakati wa Uchaguzi) na (hiki ni KICHEKESHO zaidi) Tume ya Uchaguzi Zanzibar. Yaani, Zanzibar ina Tume ya Uchaguzi, ambayo baadhi ya watendaji wake wako kwenye Tume ya Taifa (Jamhuri) ya Uchaguzi. Mpo hapo? Tume mbili, nchi moja. Majimbo yanatambulika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Jamhuri), na pia yanatambulika huko Zanzibar. Lakini (KICHEKESHO ZAIDI) sijaona, sijasikia, Mbunge wa Jamhuri akaingia kwenye Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kuiwakilisha Jamhuri! Hilo HALIPO! Ila, wao wanaingia kwenye Bunge la Jamhuri! Nadhani mmenielewa!
Haya. Turudie.
Rais wa Jamhuri. Rais wa Zanzibar.
Bunge la Jamhuri. Bunge la Zanzibar.
Baraza la Mawaziri la Jamhuri. Baraza la Zanzibar.
Wabunge wa Jamhuri. Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar.
Serikali ya Jamhuri. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Jeshi la Polisi la Tanzania. Oh, hakuna Jeshi la Polisi la Zanzibar.
Jeshi la Wananchi la Tanzania. Oh, HAKUNA Jeshi la Wananchi la Zanzibar.
Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri. Oh, LIPO Jeshi la Kujenga Uchumi la Zanzibar (JKU).
Oh, HAKUNA Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo cha Jamhuri. Oh, lakini KIPO Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) cha Zanzibar.
Tathimini yangu?
Muungano huu haufai. Ni bora tuwe na Serikali Moja! Yeyote yule aliyeko Zanzibar aweze kugombea nafasi yoyote ile kwenye Uongozi, ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sitaki, sioni haja ya kuwa na Serikali Mbili ndani ya Muungano. Hakuna faida wala haja. Serikali moja. Hakuna haja ya kuwa na Bunge la Jamhuri na Baraza la Wawakilishi. Ina maana kwamba kuna Sheria za Muungano na Sheria za Zanzibar? Sasa nini haswa faida na haja ya kuwa na Muungano?
Tuache unafiki, tuanze kuambizana ukweli.
Kama Zanzibar haitaki Muungano, basi, wapige kura ya maoni kujitoa. Wakijitoa, vikosi vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi viondolewe mara moja huko Zanzibar. Vijana wetu warudi nyumbani! Kama hawataki Muungano, tunafuta mara moja ruzuku wanayoipata kwenye Bajeti yao. Mamlaka ya Mapato ya Tanzania ifunge virago vyake huko Zanzibar. Ukitaka kwenda Zanzibar, unagonga passport yako, unalipia VISA kama vile unakwenda nchi nyingine. Na wao pia, wakija Tanzania, walipie VISA. Wazanzibari wote waliopo Tanzania bara waombe na kulipia vibali vya makazi. Ndicho wanachokitaka?
Tuache unafiki, tuambizane ukweli.
Serikali Moja! Nchi Moja! Bendera Moja! Wimbo MMOJA wa Taifa.
Hakuna Bendera ya Jamhuri kisha kuna Bendera ya Zanzibar. Hakuna Wimbo wa Taifa kisha kuna Wimbo wa Taifa wa Zanzibar! ZANZIBAR SIO NCHI!
Namuunga mkono kwa dhati kabisa, Waziri Mkuu, Mhe. Pinda Peter Mizengo Kayanda, kwamba, SERIKALI IWE MOJA, kwani hii ni NCHI MOJA, inayojulikana kwa jina la, JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!
IDUMU JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
MUNGU WABARIKI WATANZANIA NA VIONGOZI WAKE!
MUNGU TULINDE WATANZANIA!
MUNGU TUEPUSHE NA UFISADI!
./Mwana wa Haki
P.S. Bado nitaendelea kusema. Mwenye kukerwa, aende kujirusha FERI! Au Bahari ya Hindi kama Magogoni hapatoshi!
Huna jipya au mapepe ya Gin&tonic bado yamo kichwani ?