Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Ngekewa unafanya kosa kumuona Pinda peke yake ndiye mkosaji. Lugha za kibabe hazikuanza kwake. Maneno kama 'kutingisha kiberiti n.k' yote yalitokea visiwani. Hivi karibuni pamekuwa na ushindani wa kuweka visheria kandamizi za kuwabana wanaotoka bara huko visiwani. Sheria zinazohusu ajira, haki ya kumiliki ardhi n.k. zimewekwa katika hali ya kumfanya mtu wa bara aonekane sawa na mKenya na wengine. Mfano mwingine ni lugha ya kibabe inayotumika katika suala la mafuta. Mnachosema wenzetu ni kuwa, mmeishaamua basi. Hamna mjadala! Hii kweli ni haki katika nchi inayodai kuwa ni ya Muungano?

Mimi natofautiana na Pinda katika imani yake ya kuwa serikali moja ni suluhisho. Mimi nitawashangaa sana wazanzibari kama watakubali kugeuzwa kuwa mkoa katika nchi ya Tanzania. Tukilazimisha hilo ndio tutawakimbiza hata wale ambao wangependa Muungano. Nchi zote zilizolazimisha kufanya hivyo zimeishia pabaya ( Ethiopia, Yugoslavia, USSR n.k.).

Vile vile sidhani kuwa serikali tatu ni suluhisho. Kutokana na tofauti ya uchumi, ukubwa wa nchi, idadi ya watu, maendeleo kati ya Zanzibar na Bara, watu wa bara watashawishika kutochangia katika hiyo Federal government na hivyo kuipeleka kaburini. Mfano ni kifo cha Jumuia ya Afrika Mashariki.

Kwa mawazo yangu, mfumo uliopo sasa wa serikali mbili ndio pekee ambao unaweza kuwa sustainable. Lakini ili iwe hivyo, itabidi kuwa masuala yanayohesabika kama ya muungano yapunguzwe hadi yabakie yale ambayo ni basic ( k.m. Mambo ya nje, Ulinzi na Hazina). Hatuwezi kujiita nchii moja tukiwa na balozi tofauti, majeshi tofauti na sarafu tofauti. Hayo mengine ( madini, elimu, bandari, uvuvi, kilimo, afya n.k.) kila nchi ijisimamie. Kwa hali hii, nchi ya Zanzibar iwe na uwakilishi mdogo katika Bunge la Muungano maana masuala mengi yatahusu bara na si visiwani. Ila katika hayo masuala machache ya Muungano yaliyobaki, nchi zote mbili ziwe na uwakilishi kwenye hizo wizara. Uwakilishi huu si lazima uwe based kwenye idadi ya watu bali uipe kila nchi uwezo wa kukataa jambo ambalo halikubaliani nalo. Lakini ukweli kuwa Bara ndiyo mhimili mkuu wa masuala yote ya Muungano ni lazima utambulike. Bara ni lazima ikubali kubeba mzigo mkubwa wa kuendesha shughuli za serikali ya Muungano na Zanzibar lazima ikubali kuwa kwa kufanya hivi inastahili haki zaidi. Mfano ni nchi ya Greenland na Denmark. Sasa, kama hapo baadae nchi ya Zanzibar itaamua kujitoa pasiwe na pingamizi. Na hivyo hivyo kwa nchi ya Tanzania ikiamua kuwa haihitaji zanzibar. Muungano ni lazima ukubali uwezekano wa kutengana. Kwa kufanya hivyo kutaupa legitimacy maana utakuwa wa hiari na si wa kulazimishana.

Amandla........

AMANDLA...!
Nafurahi sana kupata mtu anaejali mawazo ya nduguye.

Suala la kauli zisizofaa kwa Muungano zimeanzishwa na upande wa Bara. Kauli ya kutingisha kibiriti ilikuja kipindi kirefu cha kauli ya kusema "moja na moja tatu". Hiyo ni kauli mashuhuri iliyotolewa na kiongozi mashuhuri kutoka Bara. Na ukiangalia kauli za Pinda kwa kweli hazikuhitajika kutamkwa na Kiongozi mkubwa kama yeye kwa kujibu suwala la kutaka kujulikana hadhi na haki ya upande mmoja wa muungano. Bila shaka hilo la harakati za kuwazuia Wabara zanzibar linaweza likajibiwa kwa sababu mbili
1. Pengine sasa Wazanzibari wameshagunduwa kuwa kuna lemgo baya kwa harakati zilizoppamba moto za kununua makazi zanzibarambako tunaambiwa hakuna maana yoyote. Wazanzibari wameshitushwa na vitendo na kauli ya mihimili mikubwa kutoka Bara. Kwanza Bunge likiongozwa na mkuu wa Pinda na pili kauli za Wabunge wa dini nyengine wakiongozwa na juhudi za Kanisa. Kwa hiki wasilaumiwe Wazanzibari kwani wanaishi kwa imani nyengine isiyo ya Kikiristo na si Mkiristo au mwengine alie tayari kuona imani yake inaingiliwa.
2. Wazanzibari wanaogopa ule msemo wa bahari inapoamuwa kujaza mto bari ni gharika. Ivo kila mkowa wa Bara itowe watulaki moja na kuwapeleka Zanzibar nini kitatokea?
Ama kuhusu serikali tatu kuwa sio suluhisho naomba nipingane hapo kwani Zanzibar siku zote ilikuwa ikisisitiza mfumo wa serikali mbili lakini Wasomi na Wabunge wa Bara walisema kuwa tatu ndio suluhisho. Uzoefu ni kujifunza na Wazanzibari wameshakubali sasa kuwa wasomi walikuwa sahihi.
Ama la kuchangia kwenye serikali ya tatu hilo lisiwe issue kwani asiechangia matumizi hapati ile huduma inayolipiwa na kwanini Bara wakatae kulipia wakati kwa lolote wao ndio wanaofaidika zaidi kwani wao si ndio nchi kubwa yenye kuhitaji kuduma zaidi kuliko kijinchi kidogo cha Zanzibar.
Nionavyo mimi; Bara hawana will ya Muungano bali kutawala na wakiondowa fikira hiyoMUUNGANO UTADUMU!
 
how did it the writer come to such a conclusion that Nyerere's statement above "proved" that he was the ONLY Tanzanian who knows?



Unquestionably true.



Where did they get this insight about how Nyerere "saw" that the Islamic Zanzibar a threat to Christianity?



Wrong history! Yaani Nyerere ndiye aliyeyabuni mapinduzi ya Zanzibar?



Ridiculous assertion void of evidence to support it.


Mzee since when evidence has been that important when it comes to posting here?
 
Mwiba una matatizo makubwa sana kaka .Yaani wewe Udini na Uzanzibari unakuumiza sana mkubwa .Yaani mimi Lunyungu niogope kuachana na Jangwa ? Kuna nini hapo kisiwani ? Beach ama nini? Beach zaweza kuwafanya muishi na uvivu wenu huo .Niko nyuma ya Pinda namuunga , jaribuni muone .

Huyu nano sijui mwenyeji sijui mwenyehija mwenyewe anajua moto wake anaongelea mafuta na hana nia ya kuuvunja muungano lakini ngoja kuna siku tuaamka na kumtangaza Mkuu wa Mkoa wa huko tuna maliza kazi .

Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya Mzanzibari na Mbara. Wakati wewe hufahamu thamani ya Utaifa na imani Mwiba hathamini Ufisadi na uporaji wa sehemu ya mwengine.
Nanakupenda Lunyungu kuwa huimind Zanzibar kama wanavyimind wale wengine wakiongozwa na Kanisa na kuwafanya wavamie kila pahala na kutaka kuweka makanisa ya vibanda vya makuti. Au labda hujafika huko Zanzibar ndio maana hujaamuwa kuacha nci ya rutuba na kwenda jangwani Zeni/ Au sio?
 
Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya Mzanzibari na Mbara. Wakati wewe hufahamu thamani ya Utaifa na imani Mwiba hathamini Ufisadi na uporaji wa sehemu ya mwengine.
Nanakupenda Lunyungu kuwa huimind Zanzibar kama wanavyimind wale wengine wakiongozwa na Kanisa na kuwafanya wavamie kila pahala na kutaka kuweka makanisa ya vibanda vya makuti. Au labda hujafika huko Zanzibar ndio maana hujaamuwa kuacha nci ya rutuba na kwenda jangwani Zeni/ Au sio?
haya wengine wasiokuwa na mitafiti mizuri, kuropoka tuuuu na kubwata
 
Hiyo ndio tofauti kubwa kati ya Mzanzibari na Mbara. Wakati wewe hufahamu thamani ya Utaifa na imani Mwiba hathamini Ufisadi na uporaji wa sehemu ya mwengine.
Nanakupenda Lunyungu kuwa huimind Zanzibar kama wanavyimind wale wengine wakiongozwa na Kanisa na kuwafanya wavamie kila pahala na kutaka kuweka makanisa ya vibanda vya makuti. Au labda hujafika huko Zanzibar ndio maana hujaamuwa kuacha nci ya rutuba na kwenda jangwani Zeni/ Au sio?


,,,Kila PAHALA wapi Mkuu MWIBA????,,,hii society inakua,na inapokua ndipo na mambo mengine huongezeka pia,Zanzibar ya enzi zile ilikua na walevi wachache sana,leo hii mijitu kibao,tena wanakamua hadharani kabisa,achana na wale wanaojificha kwenye vikuta na chochoro za pale michenzani makonteina,tusisingizie kila jambo ati linatokea upande wa pili,hilo ni kosaa!!!!!.
 
hana mabawa!!!!

na aanaonekana bado kinda
 
Du hii kali kweli kweli!

Iceland walijifanya wanaweza kuruka wenyewe- leo wanawapigia magoti EU kuomba kujiunga na jumuia kubwa!
 
Utashangaa wengi Visiwani tena wanaolalamika wapo ughaibuni..hawapo Zenj..wengine wanadhani Muungano ulivunjika basi Usultani utarudi!

Hakuna sumu mbaya kama malalamiko yasiyokwisha kwa mtu mzima!
 
Asante Fundi Mchundo kwa kujaribu kuweka historia sawa - tatizo la wengi ni kuwa wamezaliwa miaka mingi baada ya mapinduzi ya Zanzibar. Hata hiyo historia ya Okello, alivyoweza kuwashawishi na kuwapa hamasa vijana wanamapinduzi kumuunga mkono, hawaijui. Nikiwa Dar es Salaam nilishuhudia, siyo kusimuliwa, Okello alivyohadaiwa kuja Dar es Salaam na kutiwa nguvuni uwanja wa ndege kwa amri ya Mwalimu. Huko visiwani hakuwepo hata mtu mmoja aliyeweza kutamba mbele ya Field Marshall John Okello. Kama kuna historia iliyopindishwa ni kuhusu ushiriki wa Okello katika kufanikisha mapinduzi ya mwaka 1964. Kujaribu kuingiza Udini katika swala hilo ni uzushi unaotawaliwa zaidi na chuki na ujinga wa hawa watu waliochoka kiakili.

Kuna watu wanajaribu ama kujipa au kupewa credit at the expence ya huyu Mganda, Field Marshall John Okello, lakini kamwe hawatafanikiwa kufuta historia yake. Wengine tunakumbuka siku aliyotangaza kwenye radio kuwa mapinduzi yamefanikiwa na yeye amekamata dola kama mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi, Zanzibar - huo ndio ukweli, mengine ni spin tu. Akina Karume walikuja kupewa tu ulaji baada ya ngoma kutulia - walijificha wakiogopa mapambano dhidi ya Usultani. Vugu vugu alioanzisha Okello visiwani vilifanya aogopwe kama ukoma na tawala zote Afrika Mashariki - hakuna aliyetaka kujihusisha naye. Bila Okello mapinduzi hayangewezekana kwa wakati ule na historia ya Zanzibar haingekuwa kama ilivyo hii leo - ndio ukweli !!
 
Asante Fundi Mchundo kwa kujaribu kuweka historia sawa - tatizo la wengi ni kuwa wamezaliwa miaka mingi baada ya mapinduzi ya Zanzibar. Hata hiyo historia ya Okello, alivyoweza kuwashawishi na kuwapa hamasa vijana wanamapinduzi kumuunga mkono, hawaijui. Nikiwa Dar es Salaam nilishuhudia, siyo kusimuliwa, Okello alivyohadaiwa kuja Dar es Salaam na kutiwa nguvuni uwanja wa ndege kwa amri ya Mwalimu. Huko visiwani hakuwepo hata mtu mmoja aliyeweza kutamba mbele ya Field Marshall John Okello. Kama kuna historia iliyopindishwa ni kuhusu ushiriki wa Okello katika kufanikisha mapinduzi ya mwaka 1964. Kujaribu kuingiza Udini katika swala hilo ni uzushi unaotawaliwa zaidi na chuki na ujinga wa hawa watu waliochoka kiakili.

Kuna watu wanajaribu ama kujipa au kupewa credit at the expence ya huyu Mganda, Field Marshall John Okello, lakini kamwe hawatafanikiwa kufuta historia yake. Wengine tunakumbuka siku aliyotangaza kwenye radio kuwa mapinduzi yamefanikiwa na yeye amekamata dola kama mwenyekiti wa kwanza wa baraza la mapinduzi, Zanzibar - huo ndio ukweli, mengine ni spin tu. Akina Karume walikuja kupewa tu ulaji baada ya ngoma kutulia - walijificha wakiogopa mapambano dhidi ya Usultani. Vugu vugu alioanzisha Okello visiwani vilifanya aogopwe kama ukoma na tawala zote Afrika Mashariki - hakuna aliyetaka kujihusisha naye. Bila Okello mapinduzi hayangewezekana kwa wakati ule na historia ya Zanzibar haingekuwa kama ilivyo hii leo - ndio ukweli !!

Unfortunately kuna watu ambao wanataka kuhamishia mitazamo yao ya wakati huu iliyojaa udini kwenye wakati ambapo uzalendo (in the best sense of the word) uliwekwa mbele kuliko dini! Wanajaribu kuvisha koti la udini kila kilichotokea kwa vile tu wahusika fulani walitoka dini fulani! Wanachosahau ni kuwa hii mitazamo ni ya hivi karibuni. Hapo awali dini haikuwa na nafasi kubwa katika kumkubali mtu. Vya muhimu zaidi vilikuwa ni kabila, rangi na nafasi ya mtu katika jamii. Na hata haya hayakuwazuia vijana wa Umma kusimama kidete na ASP kupinga dhulma za wale waliofanana nao rangi! Kilichowaunganisha wakina Okello, Babu, Karume si dini bali uzalendo. Kama ilivyokuwa kwa wakina Julius, Dossa, Abdulwahid, John, Oscar, Hamza, Ally, Dunstan, Titi n.k. Hawa wote walijiona kwanza ni watanganyika kabla ya umisheni au uislamu wao.

Sumu ya udini imeletwa hivi karibuni na tusipo angalia itatufikisha pabaya.

Amandla.....
 
mimi binafsi nimefurahi sana kutufananisha kama ndege asiyekuwa na mbawa. Hii ni dhahiri kuwa namna munatudharau wazaznzibari. Hebu rudi kwenye historia yetu kabla muungano uone kama tulikuwa tukitegemea mtu au watu. Sisi, ni watu wenye historia yetu na hatushindwi kujiendeleza. Nyinyi mumetuua baada ya muungano. Mumeua elimu znz, tiba imezorota, makazi hamna na ubaguzi wa kijinsia umeletwa na nyinyi serikali ya CCM. Nyinyi ma CCM ni wakorofi sana na ni wezi wakubwa wa mali ya nchi. Hamuna historia safi kabisa. Iko haja vyama vya upinzani kushirikiana kwa dhati kabisa ili kuondosha uoza uliopo.
 
Katika kuonyesha kuwa anajipendekeza upande wa pili wa Muungano(ambao sasa wazanzibari wote wanauwona kama adui wa maendeleo yao) Waziri Kingozi anaemaliza muda wake,Bw. Shamsi Nahodha(kama Karume Mdogo alivyomwita "Mzigo") ameanza kampeni za kutafuta kuungwa mkono azma yake ya kugombea urais wa zanzibar katika uchaguzi Mkuu ujao 2010,kwa staili ya aina yake.
Habari kutoka Zanzibar zinasema kuwa makundi mengi ya wananchi yameonekana mitaani yakizungumza na kujadiliana kauli ya Mh. Nahodha kupuuza msimamo wa SMZ na Baraza la Mapinduzi wa kuliondoa suala la mafuta na gesi kutoka katka orodha ya mambo ya Muungano na kutaka badala yake kuwepo mijadala, Da 'Salma anasimulia kama alivyoshuhudia.........


WAZIRI Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha amesema kwamba mjadala wa mafuta na gesi asilia hakuhitajiki jazba katika kufikia ufumbuzi wa suala hilo iwapo lipakie aktika orodha ya mambo ya muungano au liondolewe na kusimamiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Nahodha aliyasema hayo wakati akiakhirisha kikao cha Baraza la Wawakilishi jana, ambapo alisema jambo hilo linahitaji busara zaidi kuliko jabza.

Msimamo huo wa Waziri Kiongozi unaonekana kwenda kinyume na hoja nyingi za wajumbe wa baraza la wawakilishi ambao mara kwa mara wamekuwa wakisisitiza kwamba uamuzi wa kuliondoka suala hilo katika orodha ya mambo ya muungano halihitaji mjadala zaidi ya utekelezaji.

Tayari baraza la wawakilishi pamoja na baraza la mapinduzi limeamua kuliondoa suala hilo katika muungano, lakini maamuzi hayo yanaonekana kupingana na hutuba ya waziri kiongozi.

Nahodha alisema kamwe suala hilo halitaachwa kuweza kusababisha kuvuruga amani na utulivu uliopo ambao kwa muda mrefu serikali ya Tanzania iansifikana kwa kuwa na hali ya mani ya utulivu katika bara la afrika.

Waziri Kiongozi alisema suala hilo halitaweza kusababisha mgogoro kiasi ya kuigawa nchi na kwamba Serikali ipo makini kuona ufumbuzi wake unapatikana kwa njia za amani.

“Waheshimiwa Wajumbe, napenda kuwajulisheni kuwa katika kulipatia ufumbuzi suala la mafuta na gesi asilia tutatumia busara katika kufikia ufumbuzi…Serikali italisimamia hilo” Alisisitiza Nahodha.

Katika uamuzi wake baraza la wawakilishi lilisisitiza ni lazima serikali ya mapinduzi Zanzibar iwasilishe sera katika baraza hilo ya nishati na gesi asilia ikiwa ni mchakato wa kuunda shirika la maendeleo ya petroli Zanzibar.

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Baraza la Mapinduzi wameamua kuwa suala la mafuta na gesi asilia liondolewe kwenye orodha ya mambo ya Muungano.

Wawakilishi hao walisema kwamba uamuzi huo ni wa wananchi wote wa Zanzibar na kamwe si utashi wa mtu mmoja ambapo walisema ni busara kuyaondoa kwa maslahi ya kulinda na kudumisha Muungano.

Tangu kuanza kupatikana kwa gesi asilia Zanzibar imekuwa hainufaiki na mapato ya nishati hiyo licha ya suala hilo kuwa ni la Muungano na badala yake upande mmoja wa Tanzania Bara ndio umekuwa ukinufaika.

Katika uamuzi wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM) limetoa maamuzi matano juu ya suala la mafuta na gesi asilia sasa liondolewe katika orodha ya masuala yanayojadiliwa na Kamati ya kujadili kero za Muungano iliyo chini ya Makamu wa Rais.

Maamuzi hayo ambayo ni pamoja na masuala yote yanayohusiana na mafuta na gesi asilia yatolewe kwenye orodha ya Muungano, usimamizi na udhibiti wa rasilimali hiyo katika maeneo yote ya ardhi na baharini pamoja na eneo la ukanda maalum wa kiuchumi ubaki kuwa chini ya SMZ peke yake.

Uamuzi wa tatu wa BLM ni Wizara husika imeagizwa kuanisha katika sera ya udhibiti wa rasilimali ya mafuta na gesi asilia kwa maeneo ya Zanzibar kama ilivyoelezwa katika mapendekezo ya Baraza la Wawakilishi.

Uamuzi mwengine wa BLM ni kuwa Wizara husika iandae mikakati ya kutayarisha sheria ya mafuta na gesi asilia Zanzibar ambayo inafuatiwa na kuanzishwa kwa Taasisi zitakazosimamia sekta hiyo Visiwani hapa.

Uamuzi wa mwisho wa SMZ kuwa ni taarifa ya maamuzi ya SMZ yawasilishwe katika kikao kinachofuata cha kujadili kero za Muungano ambapo kwa sasa kazi inayofuata ni utekelezaji wa maelekezo ya Baraza la Mapinduzi ili kuhakikisha kuwa SMZ inasimamia na kudhibiti sekta ya mafuta na gesi asilia kwa maslahi ya Wazanzibari.


SOURCE:
ZANZIBAR YETU BLOG.
 
Huenda anatafuta kuungwa mkono na wazanzibara, kwa kuwa wao ndiyo wanaoamua nani awe raisi wa wazanzibari.
Na hao wazanzibari wanapenda sana ubinafsi ndio maana waliposikia tu Nahodha anasema suala la mafuta kuwa au kutokuwa la muungano linazungumzika basi wao mara moja wanakimbilia kumtuhumu kwamba amenunuliwa na wabara.
Mambo kama hayo ndiyo yanayomkuta Mohamed Seif Khatib kila siku hawaishi kumnyooshea kidole, eti hawasaidii wala kutetea maslahi ya zanzibari.
 
Inaitajika busara zaidi kuliko jazba ndiyo kauli nzuri zaidi. Mbona hwa wa ndani ya bunge kuu hawasemi? Kwani wao wanawakilisha watu gani? Watoe msimamo wao ili tujue kuwa wazanzibar wote wana msimamo sawa.

Lakini mambo ya kuchanganya vitu hatuwaelewi. Wao wanajua kuwa serikali yao iko chini ya ile ya muungano na wanajua pia kuwa katiba ya muungano ndiyo mama sasa wanataka nchi ya tz iwe na katiba mbili?

Wale wawakilishi wao kwenye bunge kuu walete hoja binafsi za kurekebisha hizo kasoro zao siyo kupiga kelele kama hawakwenda shule.

Ubongo mtu hukupewa bure ulipewa ili uutumie tena wisely.
 
Mimi namuunga mkono Waziri Kiongozi kwa tamshi alilolitoa kwamba suala la Mafuta na gesi asilia linazungumzika.Kwa mtazamo wangu ametumia busara pengine ni kwa sababu huwa anashirikimkwenye vikao vinavyojadili kero za Muungano.Kwa ushiriki huo ndio umempa mwangaza wa namna kero mbali mbali za Muungano zinavyoweza kutatuliwa.

Hili ni la muhimu sana na kumpata kiongozi kama huyu Zanzibar anayetumia busara na hekima badala ya jazba kutatua matatizo ya wananchi ndiye afaaye kukiongoza kisiwa hicho.

Hajanunuliwa na Bara kama wanavyotafsiri isipokuwa ameamua kuwa objective kwenye suala hili na kuweka jazba pembeni.Bravo Waziri Kiongozi,viongozi kama hawa ndio wanatakiwa kuwaongoza watu.
 
Ataweza kuruka pale atakapoachwa huru . naamini wazi wapo wawezeshaji watakaojitolea kumuwezesha kuruka akiwa huru.
 
Waziri wa Nchi katika Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma amesema kuwa matamshi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa suluhu ya matatizo ya Muungano wa Tanzania itapatikana kwa kuondoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni ya kihaini.
Hayo ameyaeleza mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi wakatin akizungumza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi siku ya kufunga kikao cha Bajeti, Waziri Juma alisema matamshi ya Pinda yanafaa kuchukuliwa hatua na vyombo vya kisheria.
Juma alisema “ Unaposema utaifutilia mbali Serikali ya Zanzibar ni uhaini. Sisi tunasema kuwa vyombo vya ulinzi vipo na kwa hivyo vitafanya kazi zao..na mwenye kusema maneno hayo ni shauri yake.”
Pinda alitoa matamshi hayo wakati alipokuwa akijibu suala katika Bunge la Jamhuri ya Muungano jambo ambalo limewakasirisha sana wajumbe wa Baraza hilo ambao walitaka kujua ni kwa nini Serikali ya Zanzibar haijatoa tamko lolote lile.
Juma alisema, “ Kwa hakika si yeye tu Pinda lakini watu wengi sana wana hamu kutaka Zanzibar isiwepo katika ramani ya dunia. Na kusemwa yeshasemwa mengi na yatasemwa mengi, lakini kutekelezwa ni vigumu.”
Akishangiriwa na Wajumbe wa Baraza hilo Juma alisema haitawezekana kabisa kuiondosha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar labda iwe kwa kile alichokiita “ mtutu wa bunduki.”
Wakitoa michango yao wajumbe wengi wa Baraza hilo walieleza masikitiko yao kwa kauli ya Waziri Mkuu Pinda na kusema hii ni kuonyesha kuwa dhamira iliyokuwa imejificha sasa inaaanza kuonekana.
Mjumbe wa Jimbo la Tumbatu Haji Omar Kheir amemtaka Pinda aanze kujizuia kutoa matamshi yake yanayoiweka Zanzibar katika wakati mgumu na wasiwasi wa utatanishi.
Alisema tatizo la Muungano linalalia kwenye uchumi na kubanwa na Serikali ya Muungano ndiko kunakowafanya Wazanzibari watoe hoja kadhaa juu ya muundo na utendaji wake.
“Uchumi wa Zanzibar haulingani na Tanzania Bara,bajeti ya Zanzibar ni 400 bilioni wakati wenzetu wanagota katika Trilioni 35,mafuta ni kichocheo cha SMZ kujinasua kiuchumi na kukuza maendeleo ya jamii lakini naona hivi sasa kila siku kunazuka jambo jengine”
Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake (CUF), Omar Ali Shehe amewataka wawakilishi na wananchi wote wa Zanzibar kulaani vikali matamshi hayo ambayo yenye kutishia kuifuta Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Alisema lengo la Tanganyika hivi sasa ni kuifanya zanzibar ni mkoa mmoja wapo wa Tanzania jambo ambalo kabisa halitawezekana kwa kwa kuwa Zanzibar ina mamlaka yake kamili kama ilivyo Tanzania.
Mwakilishi huyo wa Chake Chake alisema kufa kwa SMZ hakutakubaliwa kabisa kwani wazee waliotangulia walipindua kwa kutumia mawe, mashoka na mapanga ambapo wengi wao walipoteza maisha yao hivyo sio rahisi leo hii ielezwe kuwa hakuna serikali ya Zanzibar.
Mvutano baina ya Zanzibar na Tanzania Bara umekuwa mkubwa tokea Zanzibar kutangaza kuwa itasimamia rasilmali yake ya mafuta yenyewe kinyume na ambavyo Serikali ya Muungano inataka.
Pamoja na kuteuliwa Mshauri Mwelekezi juu ya nishati hiyo ya mafuta na kutoa mapendekezo ya mgawano, lakini Serikali ya Zanzibar imekataa ushauri huo kwa sababu ya kukosa imani na Serikali ya Muungano kutokana na mahusiano ya songosongo ya muda mrefu.
Hii ni mara nyengine tena kwa Waziri Mkuu Pinda kuingia matatani kutokana na kauli zake kuhusiana na mambo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mapema kabla ya tukio hili Pinda karibuni alisema kuwa ukivunjika Muungano ni Zanzibar ndio ikayosaga meno na kabla ya hapo mwaka jana alisema kuwa Zanzibar si nchi matamshi ambayo yaliutia Muungano katika mtihani mkubwa.

SOURCE:ZANZIBAR YETU BLOG.
 
Angalia nchi ndogo to kama Comoro au Brunei zina uhuru wake, sasa SMZ mnaogopa nini? Endeleeni kudai Independence yenu, ipo siku mtaipata tu.
 
Back
Top Bottom