Ngekewa unafanya kosa kumuona Pinda peke yake ndiye mkosaji. Lugha za kibabe hazikuanza kwake. Maneno kama 'kutingisha kiberiti n.k' yote yalitokea visiwani. Hivi karibuni pamekuwa na ushindani wa kuweka visheria kandamizi za kuwabana wanaotoka bara huko visiwani. Sheria zinazohusu ajira, haki ya kumiliki ardhi n.k. zimewekwa katika hali ya kumfanya mtu wa bara aonekane sawa na mKenya na wengine. Mfano mwingine ni lugha ya kibabe inayotumika katika suala la mafuta. Mnachosema wenzetu ni kuwa, mmeishaamua basi. Hamna mjadala! Hii kweli ni haki katika nchi inayodai kuwa ni ya Muungano?
Mimi natofautiana na Pinda katika imani yake ya kuwa serikali moja ni suluhisho. Mimi nitawashangaa sana wazanzibari kama watakubali kugeuzwa kuwa mkoa katika nchi ya Tanzania. Tukilazimisha hilo ndio tutawakimbiza hata wale ambao wangependa Muungano. Nchi zote zilizolazimisha kufanya hivyo zimeishia pabaya ( Ethiopia, Yugoslavia, USSR n.k.).
Vile vile sidhani kuwa serikali tatu ni suluhisho. Kutokana na tofauti ya uchumi, ukubwa wa nchi, idadi ya watu, maendeleo kati ya Zanzibar na Bara, watu wa bara watashawishika kutochangia katika hiyo Federal government na hivyo kuipeleka kaburini. Mfano ni kifo cha Jumuia ya Afrika Mashariki.
Kwa mawazo yangu, mfumo uliopo sasa wa serikali mbili ndio pekee ambao unaweza kuwa sustainable. Lakini ili iwe hivyo, itabidi kuwa masuala yanayohesabika kama ya muungano yapunguzwe hadi yabakie yale ambayo ni basic ( k.m. Mambo ya nje, Ulinzi na Hazina). Hatuwezi kujiita nchii moja tukiwa na balozi tofauti, majeshi tofauti na sarafu tofauti. Hayo mengine ( madini, elimu, bandari, uvuvi, kilimo, afya n.k.) kila nchi ijisimamie. Kwa hali hii, nchi ya Zanzibar iwe na uwakilishi mdogo katika Bunge la Muungano maana masuala mengi yatahusu bara na si visiwani. Ila katika hayo masuala machache ya Muungano yaliyobaki, nchi zote mbili ziwe na uwakilishi kwenye hizo wizara. Uwakilishi huu si lazima uwe based kwenye idadi ya watu bali uipe kila nchi uwezo wa kukataa jambo ambalo halikubaliani nalo. Lakini ukweli kuwa Bara ndiyo mhimili mkuu wa masuala yote ya Muungano ni lazima utambulike. Bara ni lazima ikubali kubeba mzigo mkubwa wa kuendesha shughuli za serikali ya Muungano na Zanzibar lazima ikubali kuwa kwa kufanya hivi inastahili haki zaidi. Mfano ni nchi ya Greenland na Denmark. Sasa, kama hapo baadae nchi ya Zanzibar itaamua kujitoa pasiwe na pingamizi. Na hivyo hivyo kwa nchi ya Tanzania ikiamua kuwa haihitaji zanzibar. Muungano ni lazima ukubali uwezekano wa kutengana. Kwa kufanya hivyo kutaupa legitimacy maana utakuwa wa hiari na si wa kulazimishana.
Amandla........
AMANDLA...!
Nafurahi sana kupata mtu anaejali mawazo ya nduguye.
Suala la kauli zisizofaa kwa Muungano zimeanzishwa na upande wa Bara. Kauli ya kutingisha kibiriti ilikuja kipindi kirefu cha kauli ya kusema "moja na moja tatu". Hiyo ni kauli mashuhuri iliyotolewa na kiongozi mashuhuri kutoka Bara. Na ukiangalia kauli za Pinda kwa kweli hazikuhitajika kutamkwa na Kiongozi mkubwa kama yeye kwa kujibu suwala la kutaka kujulikana hadhi na haki ya upande mmoja wa muungano. Bila shaka hilo la harakati za kuwazuia Wabara zanzibar linaweza likajibiwa kwa sababu mbili
1. Pengine sasa Wazanzibari wameshagunduwa kuwa kuna lemgo baya kwa harakati zilizoppamba moto za kununua makazi zanzibarambako tunaambiwa hakuna maana yoyote. Wazanzibari wameshitushwa na vitendo na kauli ya mihimili mikubwa kutoka Bara. Kwanza Bunge likiongozwa na mkuu wa Pinda na pili kauli za Wabunge wa dini nyengine wakiongozwa na juhudi za Kanisa. Kwa hiki wasilaumiwe Wazanzibari kwani wanaishi kwa imani nyengine isiyo ya Kikiristo na si Mkiristo au mwengine alie tayari kuona imani yake inaingiliwa.
2. Wazanzibari wanaogopa ule msemo wa bahari inapoamuwa kujaza mto bari ni gharika. Ivo kila mkowa wa Bara itowe watulaki moja na kuwapeleka Zanzibar nini kitatokea?
Ama kuhusu serikali tatu kuwa sio suluhisho naomba nipingane hapo kwani Zanzibar siku zote ilikuwa ikisisitiza mfumo wa serikali mbili lakini Wasomi na Wabunge wa Bara walisema kuwa tatu ndio suluhisho. Uzoefu ni kujifunza na Wazanzibari wameshakubali sasa kuwa wasomi walikuwa sahihi.
Ama la kuchangia kwenye serikali ya tatu hilo lisiwe issue kwani asiechangia matumizi hapati ile huduma inayolipiwa na kwanini Bara wakatae kulipia wakati kwa lolote wao ndio wanaofaidika zaidi kwani wao si ndio nchi kubwa yenye kuhitaji kuduma zaidi kuliko kijinchi kidogo cha Zanzibar.
Nionavyo mimi; Bara hawana will ya Muungano bali kutawala na wakiondowa fikira hiyoMUUNGANO UTADUMU!