Tanzania sio masikini Mheshimiwa Pinda wacha kutubeza,umasikini wa waTanzania unatokana na ulaghai na udanganyifu wa kuiongoza nchi hii katika utawala bora na wenye kufuata sheria.
Leo hii Mtanzania alitakiwa awe anaishi katika nyuimba bora na ya kisasa iliyojengwa au aliyojengewa na serikali ,hebu angalieni vile vijiji vyote vinavyozunguuka machimbo ,Mheshimiwa Pinda muulize Kikwete akuelezee nyumba walizojengewa wananchi na serikali za Falme za Kiarabu ,nchi hizo zina mafuta tu na si kingine ,inakuwaje sisi wenye madini na hazina ya kila aina tunashindwa au serikali yetu inashindwa hata kutuwekea madawa ya uhakika pale kiliniki ?
Tumezunguukwa na mito na maziwa yanayofurika maji ,vipi mmeshindwa kuwapatia wananchi maji swafi ? bahari inaanzia kaskazini mpaka kusini bado bei ya samaki ni juu ,hii ikimaanisha mbinu zenu za kuwaendeleza wananchi na kuwawezesha ni duni na dhaifu na zimejaa ubabaishaji na urasimu kiasi cha kukatisha tamaa ,kutwambia tuvae batiki ni kutudhalilisha na kuona hatufai hatustahili kuvaa vile tupendavyo ,ni aibu kuilinganisha Tanzania na Indonesia maana kama ni kulinganisha basi tafuta cha kulinganisha na sio mavazi ,hebu tueleze ulifika kwenye vyuo vyao ,ulifika kwenye mahospitali yao ,ulifika kwenye viwanda vyao au walikuona unatoka Afrika wakakupeleka kwenye mabonde ya mpunga na wewe ukaona umeona jogoo.
Mheshimiwa Pinda ni aibu ilioje ,watu wanenda mbele hawarudi nyuma ,nilitumai utaona kuwa sisi tumeendelea kiasi cha kufikia kuvaa suti.
Ndio maana WaZanzibar wakaona wanacheleweshwa na fikra mgando zisizoona mbali,mimi naona fahari nikiona Mtz anaendesha gari la kifahari ,naona fahari nikiona Mtz ana nyumba nzuri inayopendeza ,naona fahari Mtz akitokeza mbele kwenye wasomi ,kumbe bado kuna wenzetu wanaona fahari eti kuiga vazi la kimaskini na kujifanya bado hatujafikia ,na kwa inavyoonyesha chini ya utawala wa CCM ni choyo tu na Mtz asiweke matumaini ya kusonga mbele kutoka na kuongeza daraja la kimaisha.