Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

Sometimes this guy anakuwa anasema ukweli lakini watu wake ndio wanakuwa wagumu sana katika kutekeleza mambo yao
 
watz wakienda ng'ambo wanaiga mavazi na sio mbinu za kuendeleza nchi yao.jamani utawsikia wanalonga kuhusu maduka ya mavazi ma restaurant sijui ma KFC na MENGINEYO.
 
Mhhh! Kichekesho! Mhe Pinda mara ya mwisho aliwaasa watendaji wakuu serikalini kuacha kuagiza magari ya kifahari, hajui kwamba watanzania tumechoka kusikia porojo kila kukicha. If you want to take action you dont have to go to the media and say, chukua hatua tuone mashangingi serikalini yameisha barabarani, hapo hatahitaji hata kusema sie watanzania tutaona tu. Yaani huyo ni Waziri Mkuu eti anahasa, badala ya kuamuru. hivi kweli hapa tuna viongozi kweli, Inasikitisha.

Hebu wakati mwingine tujaribu kuwa realistic. Sidhani kwamba Pinda alitoka ofisini kwake kuwafuata media kuanza kuelezea habari za kuvaa suti! Pinda alitoa comment hiyo wakati akifunga mkutano. Nina uhakika waliokuwa wamehudhuria mkutano huo walikuwa wamevaa suti zao na kujiniga makoo kwa tai. Kwa maana hiyo audiance aliyokuwanayo ilikuwa ndiyo hasa walengwa waliostahili kupewa somo hilo!

Kuendesha Serikali kuna utaratibu wake - eti achukue hatua tuone mashangingi yameisha barabarani. Bila shaka unataka atume traffic police wakae barabarani na kila shangingi linalopita liambiwe likae pembeni au labda yapelekwe kwenye uwanja wa jangwani until further instructions! Kama tunataka utawala bora nchini mwetu basi hautakuja kwa kumtaka Waziri Mkuu afanye au aendeshe nchi kwa amri za kidikteta ama kijeshi.

Mpeni nafasi Pinda muone atakaloweza kufanya na kwa hili la kuvaa suti tumtendee haki kwa kuelewa na kukubali kwamba tumekuwa tegemezi mno na mafundi wa kuiga mambo kiasi kwamba itafika mahali tutaanza (kama hatujafika huko tayari) kutaka Wazungu watuelekeze namna ya kuishi na wake zetu majumbani! Shame on us copy cats!
 
Hebu wakati mwingine tujaribu kuwa realistic. Sidhani kwamba Pinda alitoka ofisini kwake kuwafuata media kuanza kuelezea habari za kuvaa suti! Pinda alitoa comment hiyo wakati akifunga mkutano. Nina uhakika waliokuwa wamehudhuria mkutano huo walikuwa wamevaa suti zao na kujiniga makoo kwa tai. Kwa maana hiyo audiance aliyokuwanayo ilikuwa ndiyo hasa walengwa waliostahili kupewa somo hilo!

Kuendesha Serikali kuna utaratibu wake - eti achukue hatua tuone mashangingi yameisha barabarani. Bila shaka unataka atume traffic police wakae barabarani na kila shangingi linalopita liambiwe likae pembeni au labda yapelekwe kwenye uwanja wa jangwani until further instructions! Kama tunataka utawala bora nchini mwetu basi hautakuja kwa kumtaka Waziri Mkuu afanye au aendeshe nchi kwa amri za kidikteta ama kijeshi.

Mpeni nafasi Pinda muone atakaloweza kufanya na kwa hili la kuvaa suti tumtendee haki kwa kuelewa na kukubali kwamba tumekuwa tegemezi mno na mafundi wa kuiga mambo kiasi kwamba itafika mahali tutaanza (kama hatujafika huko tayari) kutaka Wazungu watuelekeze namna ya kuishi na wake zetu majumbani! Shame on us copy cats!

Mara nyingi mwanamapinduzi wa kweli huwa ni ngumu sana watu kumuelewa.PM ana nia nzuri lakini kama ilivyo ada kidole kimoja hakivunji chawa ,ndivyo ilivyo kwake.Hana support ya watendaji kufanyia kazi anayopanga. Na ndio maana Edward Moringe Sokoine alikufa mapema kwa sababu ya uchungu wa nchi yake na kukosa ushirikiano.
Nani asiyejua kuwa kuvaa suti ya milioni wakati jirani yako anakufa kwa kukosa hela ya hospitali au kulala na njaa ni dhambi na ufisadi vilevile?
jamani mambo mengine tujichunguze wenyewe.Upendo kwa jirani yako sio lazima ushauriwe na PM au serikali.
Na inawazekana kabisa suti za PM ni za bei rahisi,au na yeye anataka kuacha kuvaa.
Tuwe makini jamani,
 
Mimi nafikiri PM kakosa dira kwenye hili. kuwakataza watu wake kuvaa suti kwa sababu eti ya kuiga ni kuishiwa kifikra. Mbona kuvaa nguo in the first place tumeiga? Zamani hakuna mtanzania aliyekuwa anavaa nguo. Tulijisetiri kwa majani na ngozi. Teknolojia zikaingia watu wakendelea wakagundua nguo za aina mbalmbali. Ugunduzi huo nina uhakika haukufanywa na watanzania. Kwahiyo nguo tunazovaa tumeiga kutoka nje!

Nguo ziko za aina mbalimbali. Sina hakika kama Tanzania ina vazi la kitaifa. Kama lipo basi wizara ya utamaduni imezembea kazi yake. Kama halipo, yeyote atakayekurupuka na kudai kuwa kuvaa nguo ya aina fulani ni kuiga na aina nyingine sio kuiga atakuwa amekosea stepu.

Ninachokiona kinachoweza kuwa kweli ni kwamba kama unaweza kupata vazi fulani kwa bei nafuu na kama unalipenda, nunua hilo. Lakini ngoja kwanza; utampangiaje mtu nini cha kununua iwapo humgharamikii? Mimi nafikiri labda huyu mheshimiwa alikuwa anazungumzia watu fulani ambao wananunuliwa nguo na fedha za umma? Sijui kama wapo?

Kama wapo, je ni nani mwenye mamlaka na hizo bajeti zao? Hao ndio wa kuongea nao. Nahisi anataka hiyo allowance itolewe kwa watu wake lakini anaogopa kwenda straight kwa walengwa. Anatangazia umma ili iweje na huku umma wote haununuliwi nguo? Mimi nivae shati au fulana hakuna wa kunipangia maana nanunua mwenyewe jinsi bajeti yangu inavyoniruhusu. Hata nikivaa suti au shati tu, nikkingia kwenye daladala au corola yangu isiyokuwa na A/C ni uamuzi wangu. PM anahitaji kunipangia hilo kweli?

Kama mimi ni mfanyakazi wa serikali na niko entitled to lishangingi, mafuta yasiyo kipimo; as long as nimeruhusiwa kisheria, kuna ubaya gani niki enjoy benefit yangu? Again, ukitaka kubadilisha hiyo huna haja ya kupigia kelele umma mzima maana nina contract na serikali. Issue ni kuiagiza wizara husika (I guess utumishi?) ku revise hizo benefits na ku-define upya ni nani yuko entitled to gari gani na mafuta kiasi gani etc. Hakuna swala la demokrasia hapo, ni issue ya mwongozo wa utendaji tu.

Hayo magari, suti na tai kama kuna wenye hizo benefits ni kwamba ziko kwenye utaratibu unaokubalika na serikali. Na hakuna gari inayoagizwa bila kuwekwa kwenye bajeti. Ni utoto au kuwafanya watu wajinga kutangaza eti unawataka viongozi waache kuagiza magari na kununua suti wakati umeshiriki kwenye kupitisha bajeti ya hivyo vitu.

Tumechoka kudanganywa. Kama PM alifikiri anaongoza mazezeta, ajue muda wake umepita na sasa hatudanganyiki tena!
 
“Tazameni hata nchi ya Indonesia, juzi juzi nilikuwa huko ilinibidi hata mimi na msafara wangu tuache suti zetu na tuvae mashati ya batiki ya yaliyoshonwa kwa kutumia kitambaa cha nchi hiyo, ili tuweze kuonana na rais wao ambaye pia tulimkuta akiwa katika vazi la shati la kawaida kabisa hivi sisi Watanzania kwa nini tunapenda vitu vya kuiga?" aliuliza Pinda.

Mbona hapo mwenyewe ameshaiga tayari? Kwani Tanzania hatuna mashati ya batiki? Kwa nini avae mashati ya batiki ya Inddonesia?

Kwa maneno yake Mheshimiwa nimepata picha kuwa ni mtu asiyejiamini na asiyejua anataka nini hasa kwenye uongozi wake.
 
Nguo za bei mbaya zipo za aina nyingi kuliko hata hizo suti. Kuna watu hawavaagi suti lakini pamba zao hiyo bei utachemsha. Hizo nazo je? Nikijishughulisha nikapata fedha yangu kwa jasho langu kihalali, bila kudhulumu, je, kwa sababu kuna watanzania hawana chakula basi nisinunue vitu vya bei mbaya nilazimike kwenda kuwagawia?

Naweza ku-guess atakachokuja nacho next;
Atasema watanzania wanaishi kwenye majumba ya kifahari mno. Wanajenga maghorofa ya gharama sana, yenye kila kitu ndani yake hadi viyoyozi wakati kuna watanzania wengi wanaishi vijijini kwenye vibanda vya nyasi.

Atatolea mifano India na Indonesia ambako watu wamebana anasa hizo, wanaweka tu vibanda kandokando ya barabara na kuishi na familia zao!

Kudos PM, only in Tanzania.
 
Nadhani ni hoja za msingi kwa wale wanaosema kuwa Mh. Pinda hahitaji kupiga kelele kama vile akihitaji support ya wananchi. Yeye ni PM, na kama nafasi yake haimpi nafasi ya kufanya mageuzi basi akaongee na mkubwa wake waanagalie namna ya kumpa madaraka ya kiofisi. Vinginevyo aachie madaraka kama bosi wake hamuungi mkono.

Haina maana kabisa kila siku asikike akilalama, mara semina, washa marufuku, mambo ya kununua magari ya kifahari amenaza tangu mwaka juzi, na badp anaendeleza ngonjera hizohizo. Tunaamini wanaotakiwa kupiga makelele ni wapinzani, wananchi, NGO na wengine wasio nafasi ya kufanya maamuzi na madiliko ya jinsi serikali ifanye mambo yake. lakini yeye anaonekana kuwa ni mtu wa kulalamika zaidi wakati sisi wananchi tunatarajia yeye atutangazie maamuzi ya serikali juu ya mambo mbali mbali ya nchi. Atoe maelekezo yenye nguvu ya sheria, kanuni lakini siyo kubwabwaja tu.

Nakumbuka fisadi Lowasa alikuwa ni mtekelezaji na muagizaji zaidi kuliko kuwa mlalamishi kama huyu Pinda. Sikumbuka mahala Lowasa alibebeleza viongozi/wananchi wa serikali yake. Vingivyo, basi Pinda amepewa ofisi bila kufafanuliwa mipaka ya madaraka yake. Kama sivyo, basi ofisi ya Waziri Mkuu ni ubabaishaji tu na inaelekea inategemea zaidi uhusiano (ukaribu, urafiki, kuaminiana) wao Rais na PM au na personality ya PM mwenyewe. Kama ndiyo basi haja ya kubadiri katiba na kuweka wazi madaraka ya ofisi ya PM ni muhimu kuangaliwa kwa mapana zaidi.

Kwa mfano, sifahamu kama kweli PM ana madaraka yoyote yenye nguvu ya kikatiba (nje ya Bunge) juu ya Waziri/katibu na maafisa wengine wa wizara husika, kwani wengi ni wateule wa Rais. Sidhani kama PM ana kikao chochote chenye nguvu za kikatiba cha kukaa na mawaziri wa serikali nzima zaidi ya yeye kuwa mjumbe kama mawaziri wengine kwenye kikao cha cabinet. Nadhani ndioyo maana hata J. Ulimwengu kuna kipindi aliongelea katika Rai ya Ulimwengu kwenye gazeti la Raia Mwema juu ya nafasi ya ofisi PM kikatiba. La sivyo, kwa wale wanao jua basi watujuze, vinginevyo tusimlaumi Pinda bali tumhurumie kupewa ofisi isiyo na meno.
 
Kwa mfano, sifahamu kama kweli PM ana madaraka yoyote yenye nguvu ya kikatiba (nje ya Bunge) juu ya Waziri/katibu na maafisa wengine wa wizara husika, kwani wengi ni wateule wa Rais. Sidhani kama PM ana kikao chochote chenye nguvu za kikatiba cha kukaa na mawaziri wa serikali nzima zaidi ya yeye kuwa mjumbe kama mawaziri wengine kwenye kikao cha cabinet. Nadhani ndioyo maana hata J. Ulimwengu kuna kipindi aliongelea katika Rai ya Ulimwengu kwenye gazeti la Raia Mwema juu ya nafasi ya ofisi PM kikatiba. La sivyo, kwa wale wanao jua basi watujuze, vinginevyo tusimlaumi Pinda bali tumhurumie kupewa ofisi isiyo na meno.

Sawa unavyosema, ila kama ofisi ina meno au haina ni jambo la kwanza analotakiwa kujua. Akishajua hilo, ndipo atumie busara kufanya kazi accordingly. Kwa jinsi amekuwa anabwabwaja siamini kama anajua mamlaka aliyo/siyo nayo.
 
Huyu ndiye pm wa bongo' hivi tutafika kwa mwendo huu.mwisho atasema tusile nyama ni expensive.
Akitoka kwenye nyama atahamia kwenye simu, atamalizia na basic needs za enzi ya mwalimu zibaki zile zile.
 
Huyu Pinda ni hovyo kabisa, mradi aropoke tu kila siku hata kama anayoropoka hayaingii akilini. Hawa ndiyo viongozi wetu wanaiopelena nchi pabaya. Sasa Watanzania kuvaa suti kuna kosa gani!? Anataka kurudisha mambo ya kaunda suti!? au hata Kaunda suit nayo ataipiga marufuku!? Ukistaajabu ya Mussa....
 
I had high regard for you Bluray but I never thought you would stoop so low and be so insulting.

High or low regard afforded me has never been able to sway me. I strive towards religious equanimity in praise or criticism.

If there is anybody who is so low and insulting, it is the PM. I am only pointing out how he is insulting that high office, the intelligence of Tanzanians and indeed his very own person by this substance lacking laughably insincere charade.

He is playing to the worst stereotypes of the bureaucratic ombudsman who want to lay down the rules for everyone else but operate by a different set of rules. What double standards!

Mr. PM, word to the wise, action speaks louder than words.What have you done to demonstrate your commitment to this end? Don't you think if you are going to speak about thse things you will sound credible if you will speak after demonstranstrating by actions and not before?

Do not get me started nitpicking on this nagging neanderthal nincompoop.
 
For a man of you intellectual capacity this one is too low!! Leave it to the uninitiated.

What intellectual capacity?

Are you denying that this is not buldgeoning buffoonery? Can you go toe to toe trying to dispute that? I would rather you do that than come here with some lopsided ad hominem enabling and morbidly unhealthy ancestor worship.
 
Last edited:
Tanzania sio masikini Mheshimiwa Pinda wacha kutubeza,umasikini wa waTanzania unatokana na ulaghai na udanganyifu wa kuiongoza nchi hii katika utawala bora na wenye kufuata sheria.

Leo hii Mtanzania alitakiwa awe anaishi katika nyuimba bora na ya kisasa iliyojengwa au aliyojengewa na serikali ,hebu angalieni vile vijiji vyote vinavyozunguuka machimbo ,Mheshimiwa Pinda muulize Kikwete akuelezee nyumba walizojengewa wananchi na serikali za Falme za Kiarabu ,nchi hizo zina mafuta tu na si kingine ,inakuwaje sisi wenye madini na hazina ya kila aina tunashindwa au serikali yetu inashindwa hata kutuwekea madawa ya uhakika pale kiliniki ?

Tumezunguukwa na mito na maziwa yanayofurika maji ,vipi mmeshindwa kuwapatia wananchi maji swafi ? bahari inaanzia kaskazini mpaka kusini bado bei ya samaki ni juu ,hii ikimaanisha mbinu zenu za kuwaendeleza wananchi na kuwawezesha ni duni na dhaifu na zimejaa ubabaishaji na urasimu kiasi cha kukatisha tamaa ,kutwambia tuvae batiki ni kutudhalilisha na kuona hatufai hatustahili kuvaa vile tupendavyo ,ni aibu kuilinganisha Tanzania na Indonesia maana kama ni kulinganisha basi tafuta cha kulinganisha na sio mavazi ,hebu tueleze ulifika kwenye vyuo vyao ,ulifika kwenye mahospitali yao ,ulifika kwenye viwanda vyao au walikuona unatoka Afrika wakakupeleka kwenye mabonde ya mpunga na wewe ukaona umeona jogoo.

Mheshimiwa Pinda ni aibu ilioje ,watu wanenda mbele hawarudi nyuma ,nilitumai utaona kuwa sisi tumeendelea kiasi cha kufikia kuvaa suti.

Ndio maana WaZanzibar wakaona wanacheleweshwa na fikra mgando zisizoona mbali,mimi naona fahari nikiona Mtz anaendesha gari la kifahari ,naona fahari nikiona Mtz ana nyumba nzuri inayopendeza ,naona fahari Mtz akitokeza mbele kwenye wasomi ,kumbe bado kuna wenzetu wanaona fahari eti kuiga vazi la kimaskini na kujifanya bado hatujafikia ,na kwa inavyoonyesha chini ya utawala wa CCM ni choyo tu na Mtz asiweke matumaini ya kusonga mbele kutoka na kuongeza daraja la kimaisha.
 
Not even bread and circuses, just circuses, bad circuses at that!

Mwaka 1987 wakati Premier Ziyang wa China alivyokuwa ana spearhead mabadiliko ya kiuchumi, na kwa mara ya kwanza politburo ya China ilipoacha suti zao za Mao na kuvaa western suits, mwandishi wa habari mmoja ali remark kuhusu suti nzuri ya pinstripe aliyovaa Premier Ziyang. Premier Ziyang kwa kumjibu aliifungua ile suit na kuonyesha label iliyosema "Made in China"

Katika ulimwengu huu ambao unaendeshwa na uchumi wa dunia, kitu muhimu zaidi ya kuvaa au kutovaa suti ni suala zima la je, tuna produce?

Nimekuwa dissapointed kwamba Waziri Mkuu hajaweza kuliaddress hili in context.Tunaweza kuvaa traditional all we want, lakini kama hatuna viwanda vya kutengeneza hizi nguo bado tutakuwa tuna import tu -siku hizi hata nguo traditional za Afrika zinatengenezwa China!-

Kwa hiyo inabidi tuweze kuona the big picture hapa.

Halafu the irony ya hii story ni kwamba PM anaiga kutoiga, ina maana PM alikuwa hajajua hili kabla ya kwenda Indonesia? Au ndiyo ana confirm kwamba yeye ni reactionary na si critical thinker?
 
Last edited:
Wana Jamvi

Naona PM hapa ameweka fumbo, pengine mavazi anayozungumzia "suti za bei mbaya" ni zile zinanunuliwa kwa fedha za walipa kodi. Kama nakumbuka vizuri wakati wa Budget ya 2009, State house wamepewa fungu la mavazi & viburudisho, mapesa mengi tuu.

Hizi suit za JK anazobadilisha kila siku kweli hazitoki kwenye hili fungu la mavazi la State house? Natumaini hata ofisi ya VP na PM wanafungu kama hilo. Nimeona hata kwenye ofisi za jiji, madiwani wanavaa majoho kama ma-judge na nina hakika hizo sare zinanunuliwa kwa fedha za halmashauri husika. Kwa hivyo basi wito wa PM ukitekelezwa basi serikali kuu na hata hamshauri zetu zitapunguza matumizi, na fedha hizo kutengewa mswala ya maendeleo.

Kwa mtazamo wangu PM anamshitaki bosi wake, na anakemea hata halmshauri zinazotumia fedha za kodi kununua mavazi. Jamani kwani ni lazima kwa DIWANI kuvaa majoho ili wafanye kazi zao?

Kama PM yupo serious na hili la mavazi, basi aanze na budget iliyotengewa ofisi yake kwa ajili ya "mavazi na viburidisho" zipelekwe kwenye maswala ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom