Pindi Chana hafai kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

Pindi Chana hafai kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

Mwl Nyerere aliwahi kuwaambia Wanaccm wenzake kwamba, Nanukuu , "KAMA UNAMPENDA MTU KWA SABABU YA SURA YAKE BASI NENDA KANYWE NAYE CHAI” Mwisho wa kunukuu.

View attachment 2518743

Ni lazima Mamlaka ya Uteuzi ijifunze kutafuta watu wengine nje ya hawa watu wa TISS au watoto wa viongozi. Watanzania ni zaidi ya 60 milioni, haiwezekani wote hawa wasiwe na akili ila akili iwe kwa watoto wa viongozi, au hawa TISS wa kupachikwa ama na wale mamluki wenye Koneksheni tu , Hii si sawa hata kidogo.

Pindi Chana hana uwezo wa kuwa Waziri popote pale , kumpachika Wizarani kwa kulazimisha ni kudumaza maendeleo , kuna ulazima gani wa yeye kuwa Waziri wakati hana Uwezo , mbona Makada wa ccm huko Tiss na Kwingineko wako wengi tu , si wapachikeni wenye uwezo basi?

View attachment 2518739
mpendwa hata mimi nikihojiwa namna wanavyopeana vyeo nitasema kwa jazba kwanini wawe wao tu miaka yote wakati kuna watu wengi wasomi nchi hii?Mnakomaa ma walewale kwanini?Toka tunasoma shule ya msingi tunasikia familia ya kikwete,kinana,makamba,pindi chana,umi mwalimu,ndalichako,membe why?Mnatuletea chukibhana watalam na wasomi wa kila fani wapo wapeni fursa.Kupeana kindg kunadumaza ufanisi ndiyo mana wizi,ufisadi na kutowajibishana kumekitiri.Mi ctaki mavyeo yenu wapeni hawa wengine nitafurahi.
 
Hajawahi kuwa na uwezo wowote kiuongozi huyu mama, ishu ni moja tu ni mpiga kelele mithiri ya akina Sophia Simba ...kiufupi hana tofauti na akina Sophia Simba ama Zakia Meghji
 
Hajawahi kuwa na uwezo wowote kiuongozi huyu mama, ishu ni moja tu ni mpiga kelele mithiri ya akina Sophia Simba ...kiufupi hana tofauti na akina Sophia Simba ama Zakia Meghji
Ndio wanafiti kwenye nafasi hiyo kwa serikali hii ya ccm. Kelele zao zinasaidia kuonyesha kazi inaendelea. Wizara inashikiriwa na katibu mkuu, waziri yeye kazi yake ni kuchukua madesa na kuyapigia kelele bungeni, baada ya hapo ni kutembelea utekelezaji kunyoshea kidole utekelezaji uendelee huko field. Mimi ugonjwa wangu katiba nzuri ya kuseti watu gani wakamate nafasi hizi. Ili kupunguza matumiz ya kodi zetu.
Katibu mkuu anaweza kufanya kazi ya waziri vizuri zaidi na kusiwepo kitu kinachoitea waziri, kwani kitu hiki kinatulia kodi zetu bure.
Kwa sasa hata Msukuma anaweza kuwa waziri mzuri tu.
 
Hii picha inahusiana vipi na habari, nyie wapinzani subirini mchaguliwe mjenge serikali yenu hii ya sasa haiwahusu msitupangie
USSR
USSR katka ubora wake, ametoa maoni kwa mujibu wa katiba sio kumzodoa ok. Sote ni wananchi wa Tanzania, sote tunajenga Tanzania lakini pia sote tunauchungu na Tanzania yetu ok.

USSR ilisha sambaratishwa na kamwe haiwezi rudi, kuendelea kujiita USSR inamanisha hata historia yenyewe uelewi, na ndo maana unatumia ubabe usio wa lazima kwa Mtanzania mwenzako.

Jifunze kuelemisha wenzako, kuliko kutumia ubabe nashindwa kuelewa ulisoma wapi au ndo vijana wasomi wenye PhD uchwara?
 
Hili jambo huwa linashangaza sana.

Wenye mamlaka kila wakitaka mtu ni kama kuna ka data base kao huwa wanachomoa jina moja maisha yanaendelea.

Sasa kama hoja hapa ni kulimit idadi ya watu wenye ufahamu na namna serikali inavyofanya sioni kama ni sawa maana hii nchi ni ya watanzania na mtanzania kushika nafasi flani pia ni haki yake ya kuzaliwa.

Kwakweli napinga kwa nguvu zote tabia hii mbaya ya kufanya recycling.
 
mpendwa hata mimi nikihojiwa namna wanavyopeana vyeo nitasema kwa jazba kwanini wawe wao tu miaka yote wakati kuna watu wengi wasomi nchi hii?Mnakomaa ma walewale kwanini?Toka tunasoma shule ya msingi tunasikia familia ya kikwete,kinana,makamba,pindi chana,umi mwalimu,ndalichako,membe why?Mnatuletea chukibhana watalam na wasomi wa kila fani wapo wapeni fursa.Kupeana kindg kunadumaza ufanisi ndiyo mana wizi,ufisadi na kutowajibishana kumekitiri.Mi ctaki mavyeo yenu wapeni hawa wengine nitafurahi.
Jamani, umi si wajuzi tu, kaibuka wakati wa bunge la katiba?.
Pindi chan hana hata miaka 30 serikalini, labda ndalichako kidogo,,, lakini katika uongozi wa nchi huwa hatufanti majaribio,, eti tuweke fresh from school awe waziri,,
Duniani kote, nafasi za uongozi wanapewa watu exprienced,,
Hata hapa US,, mfano mike pimpeo alikua shushushu,, akawa CIA director,,, akaja akawa waziri wa mambo ya nje,, na huenda akaja kuwa Rais wa marekani,,
Huwezi kumaliza UDOM,, halafu ukae miaka 5 una bet,, halafu direct uende kuwa RC, DC, mkuu wa ATCL au hata waziri,,
Lazima upande taratibu ngazi kwa ngazi, upate exprience na uwe na connection pia,,
Sasa uko huko uswekeni,, mlele, songwe,, unataka uwaziri😁,
Nani anakujua?, Huna exprience wala connection,,, hujawahi kuwa hata Afisa tarafa,, 🙆‍♀️, impossible
 
Hii picha inahusiana vipi na habari, nyie wapinzani subirini mchaguliwe mjenge serikali yenu hii ya sasa haiwahusu msitupangie
USSR
Halafu baada ya muda na wewe umemuanzishia Uzi Pindi Chana kwamba hafai. Kumbe mmejimilikisha Upambe na Ukosoaji mnataka kila kitu mfanye nyie?
 
Siku hz ccm na serikali yake wameona TISS ndo roho yao, ukienda kwa watendaji kata 70% ni hao hao... Makatibu tarafa ni hao hao, wakuu wa wilaya ni hao hao, makatibu tawala wa wilaya, ni hao hao.. wakuu wa mikoa nao pia...hii yote ni uoga wa kimadaraka tu, inapelekea hata sehemu inayohitaji mtaalamu wa hiyo fani basi anaachwa analetwa kada wa ccm na ambaye ni TISS... Kwahiyo nchi nzima wamejazwa jazwa wao tu hata kama uwezo huo hawana .. na wengi wao kwenye hiyo idara kichwani ni weupe sana, na ndo maana nchi haisogei kimaendeleo.. ni wapigaji na wakifanya ufisadi wanahamishwa hamishwa tu...
Bila kuliondoa hili kokolo la kijani, tutaendelea kurudi nyuma kimaendeleo.Wenzetu Kenya walishaachana na habari ya KANU siku nyingi na wanasonga mbele vibaya sana!
 
Hili jambo huwa linashangaza sana.

Wenye mamlaka kila wakitaka mtu ni kama kuna ka data base kao huwa wanachomoa jina moja maisha yanaendelea.

Sasa kama hoja hapa ni kulimit idadi ya watu wenye ufahamu na namna serikali inavyofanya sioni kama ni sawa maana hii nchi ni ya watanzania na mtanzania kushika nafasi flani pia ni haki yake ya kuzaliwa.

Kwakweli napinga kwa nguvu zote tabia hii mbaya ya kufanya recycling.
Antony Diallo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mbolea.
Mtu kampuni yake ya Sahara anayoiendesha inashindwa ata kulipa Wafanyakazi mishahara!
Hii nchi viongozi wamelaaniwa!!
 
Back
Top Bottom