PISHI: Dagaa Nyasa na mnafu unaweza kula na ugali

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
Hellow

Leo nikapata dagaa nyasa wangoni nipo tayari kunikosoa kama nimepika sivyo

Kwanza mimi nikawatoa vichwa dagaa

Kisha nika waweka jikoni kuwachemsha kwanza lazima uwachemshe vinginevyo huwezi kula

Baada ya kuchemsha kwa mda nikawaipua na kuwa weka kwenye chombo

Baada ya hapo nikaweka sufuria jikon nikaweka mafuta baada ya kupata moto nika weka dagaa kuwakaanga
Baada ya kuona wapo vizuri nikaweka kitunguu sasa
Baada ya hapo nikaweka karoti na hoho
Nika mix bay yas πŸ˜‚ ili viende sambamba nikaweka nyanya nilio isaga

Nika mix tena ika iva uzuri nikaongeza maji kidogo ili nipate mchuzi

Vikatokota nikaweka nazi sasa baada ya kuona mchuzi umekuwa vizuri

Baada ya kutia nazi ikachemka vizuri nikaipua




Tuje kwenye mnafu uku
Kwanza niliuchambua vizuri tu na nikaukatakata vizuri

Baada ya hapo nikauosha nikaweka maji kwaajili ya kuuchemsha kwanza nika weka jikoni

Baada ya kuchemka nikachuja maji kisha nikauweka tena jikoni ni kwasababu mchungu usipo fanya hivi hii mboga ukuli πŸ˜‚

Baada ya hapo nikaweka sufuri jikoni na mafuta kisha nikaweka karoti na kitunguu maji

Nika mix by yas kisha nikaweka nyanya

Baada ya nyanya kuiva nikaweka mnafu

Nika mix vizuri kisha nikaweka nazi si lazima

Nikaichanganya nazi vizuri nikahakikisha imekolea haswaa πŸ˜‚

Baada ya hapo nikawa nimemaliza. Imebaki kazi moja tu kusonga ugali na nitasonga saa moja na nusu njaa ikikolea

Song la wangoni
🎢 eti nyumba ya baba usilete hawala nyumba ya baba usilete hawala kujibanabana aheeeee ……………..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…