Pishi la boga, nakosea wapi?

Pishi la boga, nakosea wapi?

Hapo juu nimeona Evelyn Salt anasifia na magimbi πŸ™†β€β™€οΈπŸ™†β€β™€οΈπŸ™†β€β™€οΈπŸ™†β€β™€οΈ

Magimbi ni mabaya jamani loh!ama mi ndo nina taste mbaya ya chakula
Haujapata vike vigimbi vidogo nje kama vyeusi halafu ndani vina rangi flani ya purple....weee navipika kama viazi, au navikaanga kwa mafuta.

Au navichemsha kidogoo kisha nachovya Kwenye ngano yenye yai nakaanga vitamu πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹
 
Haujapata vike vigimbi vidogo nje kama vyeusi halafu ndani vina rangi flani ya purple....weee navipika kama viazi, au navikaanga kwa mafuta.

Au navichemsha kidogoo kisha nachovya Kwenye ngano yenye yai nakaa vitamu πŸ˜‹πŸ˜‹πŸ˜‹


Vigimbi hivyo hivyo vidogo ndio navijua ila navyo siviwezi,tena yanakaangwa kumbe!!πŸ™†β€β™€οΈ

Vyakula jamii ya mizizi napenda mihogo tu
 
Boga nlikua nakula kipindi mdogo kwa kulazimishwa na mama, tangu nimekua sijala tena sikumbuki hata ladha yake. Hata kuchagua sokoni zuri lipi sijui.
 
Wapishi wa humu nawasalimu.

Napenda sana kula boga, ila upishi wangu unanikatisha tamaa, nikinunua boga kwenye migahawa huwa nakula linakua zuri linakua na unga unga kama kiazi kitamu.

Ishu sasa nije nilipike mimi, linakua lina maji maji, yani linanyonya maji sijui likiiva nikiliweka kwenye sahani linavuja maji tu (mchuzi maji)... hata halivutii tena kula linakata stimu. Nakosea wapi?

Huwa naandaa hivi: nalikata vipande namenya maganda, naweka kwa sufuria, chumvi kidogo na maji kidogo nachemsha.

Ila matokeo ndio hayo mimaji, kuna upishi mwingine? Au nakosea kuchagua boga? ( Siku zote sijui tu kuchagua mmh).
Niliwahi kusikia linatakiwa kuanikwa kabla ya kupika, ni kweli?
Naombeni ujuzi.
Kama una kitu kinaitwa Air Fryer tumia hicho kulifanya liwe gumu, baada ya kuchemsha boga likaiva chukua vipande vyako weka huko kwa muda mfupi litakuwa unavyotaka.
 
Mchawi chumvi . Boga haliwekewi chumvi,pika hivyo hivyo bila kuweka chumvi
 
Back
Top Bottom