Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Shalom wapendwa katika Bwana.
Mapishi ya keki ya chocolate yapo mengi leo nawawekea pishi hili.
Mahitaji
- Unga wa ngao 250g
- Kokoa vijiko vya mezani(tbsp) 3
- Baking powder vijiko vya chai(tsp) 2
- Siagi 250g
- Sukari 250g
- Mayai 4
- Maziwa 10tbsp
- Pasua mayai na uyapige pige kwenye bakuli
- Weka unga, kokoa, sukari na baking powder kwenye bakuli la kuchanganyia (mixing bowl) na changanya pamoja.
- Ongeza sukari, siagi, mayai na maziwa na changanya hadi viwe vimechanganyika kabisa.(viwe kama uji mzito). Ni rahisi zaidi ukitumia mixing bowl ya umeme.
- Miminia mchanganyiko kwenye tray la kuokea la ukubwa wa kati.
- Washa oven joto la 160 degree za centigrade na oka kwa dakika 50.
- Chomeka kijiti chembamba kwenye keki na kama kikitoka kikavu basi keki imeiva
- Epua na weka icing kadiri unavyopendelea.
- Inaweza kuliwa na chai, kahawa, juice, soda au hata maji.
Kwa watakaofanikiwa kuipika tafadhali naomba feedback.
Mungu akubariki sana.