Pishi la Keki ya Chocolate

Pishi la Keki ya Chocolate

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
chocolate_cake.jpg


Shalom wapendwa katika Bwana.
Mapishi ya keki ya chocolate yapo mengi leo nawawekea pishi hili.

Mahitaji

  1. Unga wa ngao 250g
  2. Kokoa vijiko vya mezani(tbsp) 3
  3. Baking powder vijiko vya chai(tsp) 2
  4. Siagi 250g
  5. Sukari 250g
  6. Mayai 4
  7. Maziwa 10tbsp
Mapishi au Hatua za uandaaji
  • Pasua mayai na uyapige pige kwenye bakuli
  • Weka unga, kokoa, sukari na baking powder kwenye bakuli la kuchanganyia (mixing bowl) na changanya pamoja.
  • Ongeza sukari, siagi, mayai na maziwa na changanya hadi viwe vimechanganyika kabisa.(viwe kama uji mzito). Ni rahisi zaidi ukitumia mixing bowl ya umeme.
  • Miminia mchanganyiko kwenye tray la kuokea la ukubwa wa kati.
  • Washa oven joto la 160 degree za centigrade na oka kwa dakika 50.
  • Chomeka kijiti chembamba kwenye keki na kama kikitoka kikavu basi keki imeiva
  • Epua na weka icing kadiri unavyopendelea.
  • Inaweza kuliwa na chai, kahawa, juice, soda au hata maji.
Enjoy!

Kwa watakaofanikiwa kuipika tafadhali naomba feedback.
Mungu akubariki sana.
 
Asante mkuu. Wacha nifanye maandalizi ya pishi
 
Et nawezaje kupika cake kwa rice cooker? Napenda sana hii kitu basi tu nafail kuipika
 
Back
Top Bottom