Pishi la mboga ya majani ya maboga

Pishi la mboga ya majani ya maboga

Ms Euna

Member
Joined
Oct 17, 2020
Posts
54
Reaction score
45
Salaam JF,

Leo napenda kushea nanyie jikoni kwangu,jinsi ya kupka majani ya maboga yakawa matam bila kutumia gharama kubwa.

@Mahitaji
  • majani ya maboga fungu1(kulingana na mahitaji ya familia yako)
  • Nyanya kubwa 2,zlzoiva vzur
  • kitunguu maji kikubwa kimoja
  • unga wa Katanga
  • mafuta ya kupkia kiasi
  • chumvi.

b)jinsi ya kuandaa(kupka)
  • osha vzur mbog,kisha zichambue na kuzikatakata.
  • katakata nyanya na vitunguu.
  • bandika sufuria jikon,weka mafuta na yakipata moto anza kukanga vitunguu,hakikisha haviwi brown ili viweze kuonekana kwenye mboga.
  • weka nyanya na kukoroka,
  • nyanya zkishaiva,chukua unga wakaranga vijiko4-5,koroga katika chombo ukiwaumeweka maji,kisha utaeka mchanganyo huu kwenye viungo vngne,koroga na funika kwa dakika 5,
Kisha weka mboga yako,koroga na funika ichemke,ikikarbia kuiva weka chumvi na funika ichemke,baada ya hapo tayari kwa kuliwa kwa ugali au wali.

NB: Chumvi tunaeka karbia na chakula kuiva ila kutokupoteza madini moto kwa kuchemka kwa muda mrefu.
Kwa mwenye kujazia karbun.

IMG_20201022_203643_035.jpg
IMG_20201022_203643_035.jpg
 
Mimi naona kupika kwa kutumia mafuta na karanga kwa wakati mmoja naona kama kiafya siyo!

Inapaswa kuwa kimojawapo kati ya mafuta au karanga tu na siyo vyote kwa wakati mmoja!
 
Nijuavyo mimi chumvi inapaswa kuchemka na kuiva na chakula ili kutengeneza radha nzuri ya chakula.

Pia chumvi ikichemka na kuiva vya kutosha huondoa makali ya sodium yasiyotakiwa mwilini kiafya.

Ndiyo maana chumvi mbichi ya mezani haitakiwi kutumika kiafya.
 
Si maanishi ukiweka tu unakoroga alafu unaepua la,unaiacha ichemke ambayo itakua nitofaut nakueka chumvi pale tu unapokanga vtunguu.
Ikichemka sana madini joto hupotea na ndomana wanaouza chumv ya kupima wanapaswa kuifunka ili ispigwe sana na jua
 
Hayo maji ya kukorogea unga wa karanga yanatakiwa yawe ya baridi, vuguvugu au moto?
 
Mimi naona kupika kwa kutumia mafuta na karanga kwa wakati mmoja naona kama kiafya siyo!

Inapaswa kuwa kimojawapo kati ya mafuta au karanga tu na siyo vyote kwa wakati mmoja!
Karanga znamafuta pia,ila silazma ueke nyingi kwakua unaeka na mafuta
 
Back
Top Bottom