Pishi la mboga ya majani ya maboga

Mimi naona kupika kwa kutumia mafuta na karanga kwa wakati mmoja naona kama kiafya siyo!

Inapaswa kuwa kimojawapo kati ya mafuta au karanga tu na siyo vyote kwa wakati mmoja!
Sasa utaivisha vipi vitunguu na ingredients nyingine zinazotangulia kabla ya kuweka mboga?
 
Sasa utaivisha vipi vitunguu na ingredients nyingine zinazotangulia kabla ya kuweka mboga?

Ipo namna ya kufanya ilimradi uchague kimojawapo kati ya kutumia mafuta au karanga , nazi, n.k

Matharani kama unatumia karanga;
Unaweza kuchemsha kwanza mboga kisha wakati wa kuunga unaweka hivyo vingine vyote pamoja na karanga au vyote ukaweka mwanzoni kabisa baada ya kuosha na kukatakata mboga pamoja na hayo mazagazaga mengine na karanga pamoja!
 
Kwa wavivu kama ninyi inakupasa kuwa na vitendea kazi, just find an electric grater maisha yawe marahisi...
Hizi mboga huwa ni tamu kinyama

Changamoto ni kwenye kukata vile vidogo vidogo...uvivu
 
Huu upishi unaotaja ni aina ya kuvukisha, ni sahihi pia...

Jinsi unavyobadili mbinu ya mapishi na ndivyo unavyopata ladha tofauti ya final product...

Aroma itayotoka kwenye kitunguu kilichokaangwa haitafanana na ile ya kitunguu kilichovukishwa...
 
Badala ya karanga wawezapia tumia coconut pulp/milk au vyote kwa pamoja
 
Huu upishi unaotaja ni aina ya kuvukisha, ni sahihi pia...

Jinsi unavyobadili mbinu ya mapishi na ndivyo unavyopata ladha tofauti ya final product...

Aroma itayotoka kwenye kitunguu kilichokaangwa haitafanana na ile ya kitunguu kilichovukishwa...

Labda tuseme itategemea na motives behind sababu wewe kama kipaombele chako ni radha kwanza kwa mwingine ni kulinda afya kwanza kwa hiyo inategemea!

Sababu karanga zina mafuta, mafuta yana mafuta sasa kupika kwa kutumia mafuta amabyo Yana mafuta halafu ukaange Viungo kwa mafuta ni mafuta juu ya mafuta, umeona sasa mtu aneepuka kula mafuta mengi atapenda kutumia kimojawapo na siyo vyote kwa pamoja.
 
Mkuu bado kuna mafuta ambayo kiafya hayana shida sana, halafu pia mafuta ya kuivishia kitu kama kitunguu huwa ni kidogo sana, 5mils maybe ambayo ni kama kijiko cha chai...
 
yaani mdogo wangu hakuna pishi nitakuta hujalalamika, hivi chapatti tumeshaweza!?
Zile chapati nilishanawa mikono,nimeshindwa na sina mpango wa kujaribu tena aseee😂😂😂

Hizi mboga nazipatia kupika,kukata kata tu ndio huwa mtihani
 
Huwa nafanya hivyo ila mchanga hujawahi kutoka wote
Mimi huipenda sana hii mboga na hujipikilisha mara nyingi tu, ukitaka pambana na mchanga weka maji mengi kwenye beseni ama ndoo kubwa kisha kamata majani yako matano mpaka nane yapikiche kwenye hayo maji (inataka muda wa kutosha), ukimaliza unachukuwa majani mengine hivyo hivyo mpaka unamaliza yote.
 
Shukrani mkuu
 
Mimi naona kupika kwa kutumia mafuta na karanga kwa wakati mmoja naona kama kiafya siyo!

Inapaswa kuwa kimojawapo kati ya mafuta au karanga tu na siyo vyote kwa wakati mmoja!
True, unaweza kuweka kila kitu pamoja na Karanga bila mafuta ukapika kama chukuchuku flani hivi huwa nzuri pia badala ya Karanga ukaweka nazi.
 
Hakuna mtu anajua kupika msusa kama bibi yangu.
Aisee mnyamwezi yule anaipatia sana.😋
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…