Pishi la Pweza

Pishi la Pweza

ndetichia

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
27,767
Reaction score
6,575
Pishi la Pweza

Vipimo
Pweza 1 Kilo
Mafuta ½ kikombe
Chumvi 1 kijiko cha chai
Tangawizi mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Masala ukipenda 1 kijiko cha supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha pweza kisha mkatekate
Mtie viungo vyote ulotayarisha na chumvi
Muache nusu saaa akolee viungo
Mtie ndani ya sufuria bila maji mfunike kisha weka jikoni, atatumbuka maji mwenyewe kwa moto wa kiasi paka awe rangi ya damu yam zee (maroon)
Akishawiva kwa rangi hiyo basi sasa mwaga maji yote,chukua pweza pekee weka kwenye bakuli au sahani
Weka karai au kikaango (frying pan) motoni tia mafuta acha kwa muda wa dakika tano hivi mafuta yapate moto.
Mimina pweza kwenye karai aacha wakaangike paka wabadilike ukiwageuza geuza kila baada ya muda wa dakika kumi hivi. Pweza tayari kwa kuliwa kwa ugali, bagia, kacholi au muhogo

kazi kwenu
 
napenda mno vyakula bahari, pweza, ngisi prawns, crabs etc na viwe vya kuchemsha na viungo vichache
 
Back
Top Bottom