Pita hapa ujifunze maneno ya kiingereza tunayoyatamka kimakosa, usisahau nawe kuweka ya kwako

Afadhali utanisaidia kumwelesha huyo "mtoto" Mlaleo ... Nadhani una hekima ya kumwelewesha tu anitake radhi kwa kuniita "mjinga" wakati nilijitolea tu kumfuta ujinga bila malipo yoyote....

Naamini utamwambia "Aoneshe hekima yake, afiche upumbavu wake"... Na anaweza pia kunikosoa kwa hili neno "kuonesha" akiamini neno sahihi ni "kuonyesha"

Siku huzi kuna watu wanaenda shuleni kusomea ujinga.
 
Hapo hats Mimi bado inanishinda kutofautisha kat ya number plate na plate number
Mkuu NUMBER PLATE ni kile kibati (plate) ambako namba za gari au pikipiki huandikwa, yaani PLATE YA NAMBA.

PLATE NUMBERs ni namba za gari au pikipiki zinazoandikwa kwenye plate, yaani NAMBA ZA KWENYE PLATE.
 
Maneno ya kizungu yaliyofanywa kuwa ya kiswahili ni mengi, mfano:-
1- Young Africans Sports Club - Yanga
2- Carrier Corps - Kariakoo
3- Shell Petrol Station - Sheli (vituo vya mafuto tunaviita sheli)
4- Soup - Supu
5- Helicopter - Edikopta
6- Extinguisher - ikstingisha
7- Sandals - Sandoz
8- Suit - Suti
9- Platform shoes - Raizoni
10- Week - Wiki
11- Bicycle - Baskeli
 
Week kwa Kiswahili ni Juma
Ni kweli "Week" kwa kiswahili ni Juma lakini kwenye matumizi yetu ya lugha ni "Wiki ya nenda kwa usalama" au "Juma la kwenda kwa usalama" ?
Itabidi trafiki (Traffic) wabadilishe lugha.
 
Shizzle = Shizo
My nizzle = Manizo
Coral = Koro
Little = Lito
Needle = Nido
Parastatal = Parastoto
Nipple = Nipo
Change = Chenchi
Film = Filamu
Washer = Washel
Soft Drinks zote tunaziita Soda.
Pikipiki zote ni Honda.
 
Ni "Wiki ya Kwenda kwa Usalama".
Na si hao watu wa usalama barabarani peke yao wanaofanya kosa hilo, magazeti pia, viongozi mbalimbali, walimu n.k.
Hiyo imeshaingia kwenye mfumo hatuwezi badilisha ndiyo tukubali matokeo.
Kwa mfano siku za Juma (Wiki) ni :-
1- Jumamosi
2-Jumapili
3-Jumatatu
4-Jumanne
5-Jumatano
6-Alhamisi (Al Khaamis) (Hii siku kwa kiarabu ni siku ya tano ya Juma, Hivyo tuna Jumatano 2, moja ya Kiswahili na moja ya Kiarabu)
7- Ijumaa
 
Kwa sie tuliokuwa tunatumia Garimoshi aka train, kulikuwa na waya flani ukishushwa tu ni ishara muda mfupi ujao garimoshi linaingia...ule waya wenyewe na wananchi wangu tulikuwa tunauita "ZIGINALI" kumbe "SIGNAL"
 
Nimewahi ambiwa kuna kijiji kimoja huko ktk wilaya ya Kilombero kinaitwa Zi(n)ginali kwa sababu hiyo hiyo!
Na kuna vijiji vingine vinaitwa "CHEKERENI" ambapo inatokana na neno "CHECK LINE" na vijiji vya namna hii vingi vipo kwenye makutano ya barabara na reli (hata ukisafiri kwenye baadhi ya maeneo ukisikia kondakta anasema anaeshuka Chekereni basi lazima mbele kidogo mtakatiza kwenye reli
 
Maimoria= Memorial ( soko maarufu huko Moshi, Wachagga buwana)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…