LGE2024 Pius Msekwa aeleza kutofurahia ushindi wa 99% wa CCM, asema anafurahia tu pale uchaguzi unapomalizika na pande zote zinaridhika

LGE2024 Pius Msekwa aeleza kutofurahia ushindi wa 99% wa CCM, asema anafurahia tu pale uchaguzi unapomalizika na pande zote zinaridhika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kaongea point,hawa CCM sijui wanajiona ni nani
CCM hasa hao walio kwenye USUKANI, ni kama wamepagawa..UTU na HAYA zimewatoka kabisa...MAMBO YA AJABU kabisa tunayayashuhudia miaka hii ya 2016- 2024

Na hivi kazi ya Msajili wa Siasa huwa ni NINI?..haya maupuuzi hayamgusi?..dah
 
Hawa wazee ndo waasisi wa mambo yote ya hovyo serikalini. Nawaashangaa sana wanalaumu upuuzi. Warioba ni nguli wa sheria lakini hakumshauri Mwalimu wakati anataifisha mali za watu enzi hizo.. hadi leo kuna watu wanalipwa fidia. Huyu Msekwa akiwa spika ndo mikataba inayoumiza taifa hadi leo ilisainiwa. Hawa wangekaa tu kimya maana sio wasafi. Wanalazimisha kuvunjiwa heshima.
Hebu rudi kwenye mada..
 
Mama Samia, Rais wetu mpendwa, umepatwa na nini?...mbona hufananii kabisa na haya MAUCHAFU...kwanini unaturudisha kipindi cha giza??..BADILIKA
 
CCM hasa hao walio kwenye USUKANI, ni kama wamepagawa..UTU na HAYA zimewatoka kabisa...MAMBO YA AJABU kabisa tunayayashuhudia miaka hii ya 2016- 2024

Na hivi kazi ya Msajili wa Siasa huwa ni NINI?..haya maupuuzi hayamgusi?..dah
Kwani hao Wazee hawakumbuki Mwalimu Nyerere alisema nini kuhusu hii Katiba ??!
Mbona wao katika lawama zote wanazozitoa hivi sasa hawazungumzii kuhusu mapungufu aliyoyaona Mwalimu kwenye Katiba ??!
Afadhali Mzee Warioba ameshasema sana kuhusu Katiba, lakini Mzee Msekwa sijamsikia akisema kuhusu Katiba !
Point yangu kubwa ni moja tu ,
Je kwenye Chaguzi ifuatwe Sheria na kanuni zinavyoelekeza au ifuatwe Huruma ya Viongozi watakaosimamia hizo chaguzi ??!
 
Wote hao hakuna yeyote aliyevunja Katiba !
Sawa wapo kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu ya Tanzania lakini kwenye madaraka yao kuna jinai ya wazi wazi ambayo wanaifanya kinyume na katiba iliyowaweka madarakani.Mfano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Samiah Suluhu aliwahi kusema ni vijikaratasi tu,unategemea huyo mtu ailinde Katiba?Pili baada ya Magufuri kupora uchaguzi 2020 akaona aibu kwa aliyoyafanya na kuona kwamba atakosa misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali.Kwa vile wazungu wanapenda nchi zetu zitawaliwe na wanawake akaamua kuwaingiza wabunge 19 wa Chadema kwa kisingizio kuwa CHADEMA inastahili na wanawake wengine wakatolewa gerezani usiku na kwenda kuapishwa na Spika usiku huo huo.Je Katiba ilitekelezwa vema?

Tume ya Uchaguzi imejaa wakurugenzi ambao ni makada wa ccm na tulisikia kwa masikio yetu fidhuli Magufuri akijigamba kuwa mimi nikuteue,nikupe gari,nikulipe mshahara halafu niosikie mpinzani ameshinda,basi utakuwa huna kazi.Je ndivyo Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 inavyotuagiza?Mimi ninavyojua Katiba yetu haijambagua mtu ila watendaji wake hasa wana ccm wa leo wamekuwa na ubaguzi mbaya ambao baada ya miaka kadhaa wataona faida yake au hasara yake.
 
Magufuli yupo , anakusikia. Magufuli hayupo tulikuwa na Nyerere hayupo, Mwinyi hayupo, Mkapa hayupo kazi ya kiongozi yeyote ni kuendeleza mazuri aliyoyakuta na kuacha mabaya Sasa kwanini tihangaike na Magufuli
Kila jambo hupandwa pumbavu.Unafikiri ungekuwa Mtanzania bila Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete,Magufuri,Samiah?Aliyepanda chema kama Nyerere,Mwinyi,Mkapa na Kikwete atakumbukwa kama Yesu na Mohamed na aliyepanda kibaya kama Magufuri na sasa Mama Samiah anakiendeleza atalaumiwa milele kama shetani anavyolaumiwa.
 
Back
Top Bottom