Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
IMG_20201128_132724_943.jpg


Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa Wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu Mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.




"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.

Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.

Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.
IMG_20201128_141156_304.jpg



CHANZO: "Hakuna wa kuvunja katiba, hawana sifa"- Msekwa | East Africa Television
 
#HABARI Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa @halimamdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.#EastAfricanRadio
================
Mambo yameanza kuwa sio mambo.
================


Iko hivyo
 
Mzee msekwa angeulizwa,
He, iwapo CCM wakiamua kuwapeleka kina Halima Mdee na henhw lake mahakamani ili wakaweke zuio la kupingwa kufukuzwa uanachama,

He, wataendelea kuwa wabunge?
Cc.
Cha ajabu Leo jumamosi utasikia mahakama zimefunguliwa na tayali kina Covid 19 wameshafungua mashitaka.
 
Dah
Kweli sometimes saa mbovu inasema kweli.

Ngoja tuone chawa nje ya ccm watasemaje.
Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
 
Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
mkuu mtu mwenye akili timamu hawezi kumsikiliza Kitila. kwa common sense tu yule sio chanzo cha media kupata ufafanuzi
 
Back
Top Bottom