PKK/YPG wameanza kukamatwa huko Syria

PKK/YPG wameanza kukamatwa huko Syria

Hii nchi kwa manufaa makubwa inabidi ipasuliwe! Lakini bado wanaweza wakatwangana hata hayo maeneo waliyogawana.

Wakisema waunde serikali moja bado wanahofia kugeukana kwa sababu kila upande una maslahi yake.

Wakisema wapigane mpaka mshindi apatikane bado hali ni ileile!

Ila ngoja tuone hali itakuwaje! Muda ni mwalimu.
Hii nchi kuna hatari ikawa kama libya
 
Waarabu wanasikitisha sana! Ila ngoja tuone, tuupe muda nafasi!
Hakuna cha muda wala nini,wanawake hakuna kutoka nje bila waume zao.
Wanawake hakuna kwenda shule.
Wanawake kuolewa na miaka 6.
Wanawake hakuna kuendesha gari.
Wanawake hakuna ruksa kununua karoti
Wanawake hakuna ruksa kununua tango.
Wanaume ni mwendo wa kuvaa vipedo.
Wanaume hakuna kunyoa ndevu.
Wanaume kuoa wanawake 4.
 
Wakurdi wapo Syria, uturuki na iraq, sidhani kama wataacha kudai nchi yao
Kule Iraq wamepewa Autonomy hapa Syria walikuwa wanadai Autonomy lakini Wakurdi wa Turkiya na wale wa Iran sidhani kama watafakiwa?!
 
Kama Assad asingeikimbia nchi yake, kungekuwa na uwezekano wa kufanyiwa tukio kama la Sadam au Gaddafi.
 
Waasi wameweka USD10miln kwa yoyote atakaye mpata
Kupitia Urusi, wamethibitisha kulikuwa na makubaliano na wanamapinduzi, kuwa Assad aondoke ili kupisha njia tulivu ya kukabiziana madaraka.​
 
Hii nchi inaweza kuwa uwanja wa mapambano Kwa muda mrefu sana kama Sudani na Libya.

Ngoja tukatafute hela, hapo ndio fursa na ubilionea unapopatikana sasa.
 
Dah nimekumbuka mbali sana. Sijui ilikuwa ni utoto au huruma. Nilitakaga kutimkia kuungana na wa Kurdi, enzi zile watu wanajitolea. Mimi naumia sana, kuona watu wanaokandamizwa.
 
Ndoto za Wakurdi za kutaka Autonomy wanaweza kuziacha kama watapewa nafasi muhimu kwenye Serikali ijayo.
Kurd ni kete ya baadaye dhidi ya Turkey, siyo sasa. Ila ramani ya taifa lao imeshachorwa pale.
Kwasasa wenye mamlaka wanaendelea kupachangamsha kwanza pachangamke kama maharage ndani ya chungu
 
Kurd ni kete ya baadaye dhidi ya Turkey, siyo sasa. Ila ramani ya taifa lao imeshachorwa pale.
Kwasasa wenye mamlaka wanaendelea kupachangamsha kwanza pachangamke kama maharage ndani ya chungu
Israel imesema itawasaidia Minorities wote wa Middle east.
 
Kipi kipya, Turkey ina vita yake na kurds tokea vita inaanza whether Assad angebaki au angetoka bado makundi yanayosupportiwa na Turkey yangevamia tu.

Pia PKK sio magaidi, mind you silaha walikua wanapewa na USA kupambana na ISIS je USA wanafadhili ugaidi?
Kwanini marekani asisapoti magaidi.

America anachoangalia ni maslahi yake tu.
 
Jeshi la Anga la Israeli leo limetekeleza mashambulio makubwa nchini Syria kwa kushambulia vituo karibu 100 vya jeshi la Syria.

Silaha nyingi zimeharibiwa haswa silaha za hali ya juu na maangamizi makubwa.
 
Back
Top Bottom