Umesema "Wana uwezo wa ku mobilize zikapatikana"; kama wana uwezo wa kumobilize na zikapatikana nyie hamna huo uwezo, umekubali kuwa hao unaowapa wana uwezo wa kuuweka huo mradi sokoni wakapata fedha. Yule mwenzenu alikua ana akili, ingawa alikuwa dictator (JPM), alianzisha mradi na kuuweka sokoni na fedha zikapatikana na mradi bado ni wenu. Na alichagua contractors vizuri, hakuwapa matapeli wenu hao. Angalia Bwawa, umeme myauza nyie na pesa mtapa nyie. Contractors- Arab Contractors. SGR - Turkey-Portugal- na mradi ni wenu, ingawa hakutumia contractors wa Tanzania. Na hesabu miradi yake yote utaona hivyo.
Sasa nyie mnauza asset na mnawapa madraka yote. Angalia DP World, hadi chumbani wanaingia kuchukua siri zenu maana lango lenu wao ndiyo wanamiliki na pesa wanakusanya wao wanakupa wewe commission. Bagamoy imepewa kwa KSA, Ambaye kiukweli ni dalali tu, anayetaka hiyo bandari ni Mchina, hiyo sehemu ni strategic kwake kutokana na geopolitics na Marekani. JPM aliwastukia, sasa wanakuja kinyumenyume na hii lazima ni suggestion ya CCM kuwa hawa wachina watafute dalali wawe nyuma ya dalali. It fits with CCM ya mama Samia. Uzeni tu. Wala msiwe na aibu.