...Iwapo mwanamke amebakwa (na majambazi/mwendawazimu/etc) akapata ujauzito, ni halali kuitoa hiyo mimba au?
Si halal hata kidogo...
Hakika ni kuwa siku hizi imekuwa ni biashara kwa madaktari hasa katika nchi zetu za Afrika na nyinginezo kuwatishia wagonjwa ili wapate biashara au kufanya upasuaji ili wapate pato kubwa zaidi.
Uislamu umeweka mikakati yake katika kila jambo. Ikiwa mzazi ataambiwa na daktari mtaalamu na aliyebobea katika suala la magonjwa kwa mzazi na mtoto bila kuwepo ushawishi wa aina yoyote ile itafaa kwa mzazi kukubali kutolewa mimba ili aokolewe mama.
Hata hivyo, wazazi wanatakiwa waende kwa daktari wataalamu katika fani hiyo na ikiwa kutakuwepo na daktari mcha Mungu muadilifu itabidi muende kwake, ili kupata ushauri juu ya afya ya mama mjamzito.
Daktari ndiye atakaye mshauri juu ya afya yake na kama kuna dharura itakayo sababisha utowaji wa mimba. Utowaji wa mimba hiyo itazingatiwa tu kuwa kuna uwezekana wa mama kufariki kwa kuwa na kiumbe hicho, au kuendelea kwake kuwa na mimba hiyo kutamletea mauti.
Na isitoshe kukubalika huko, bali kumetakiwa uthibitisho huo utolewe na daktari mwenye kuaminika kabisa. Na muhimu kwanza atafutwe daktari muadilifu mwenye kuaminika...
Ama kuitoa mimba tu kwa sababu ya kutotaka mtoto, au kukhofia riziki yake, au malezi yake, au kuchelea gharama za maisha kama kumsomesha, kumvisha, au kumlisha n.k. hayo yote hayaruhusiwi kisheria.
Mnamfikiriaje mwanamke wa namna hiyo? Fikiria ni mtu unayemjua anakuomba ushauri.
Inajulikana kuwa hicho kilichopo tumboni hakihusiki kwa njia moja au nyingine na jarima ile ya kubakwa mwanamke huyo, na maadam haikuwa ridhaa ya mwanamke kufanywa hivyo na alijitahidi kupambana na mbakaji/wabakaji akazidiwa, ni wajibu wake kukihifadhi hicho kiumbe na M'Mungu Atakilinda na kukijaalia kuwa ni chema na poza kwa mama yake.
Na ikiwa mwanamke huyo hajaolewa, basi ni jambo jema kwa wanaume wenye imani kumsitiri na kumsaidia kumtoa katika mitihani hiyo iliyomkumba. Ama kama ana mume, basi mume wake ajitahidi japo ni vigumu sana, kusubiri na kukikubali kiumbe hicho ambacho hakina hatia yoyote ile. Na malipo makubwa yanawasubiri watu aina hiyo.