*~Please**Mommy**Please~*


Kuwa na uwezo wa kujitetea sio swali mkuu. Tena umegusa point nzuri...watu waliopooza. Hapa wapo wa aina nyingi. Sasa tuongelee wale wanaoshindwa kupumua, hadi wanasaidiwa na mashine. Hapo madaktari si huwa wanaishauri familia wazime mashine? Hii si ilitokea hadi kwa baba wa taifa? Mngetaka mpaka leo angeweza kuendelea kuwa 'hai'. Sema ndo hivyo...he seizes to be a human. Kwa nini? Anashindwa kuji-support mwenyewe hata kwa basic function ya kupumua.

Kwa hiyo wewe unasema fetus ni mwanadamu? Na ni kitu gani kinamfanya awe mwanadamu kwa maoni yako?
 

Point yako ya kwanza ni kweli. Jinsi technologia inavyobadilika basi imetubidi na sisi binadamu kubadilisha terminologies mbalimbali. Mfano mwingine ni kifo. Kwa sasa hii inaleta tatizo hata kwenye sheria. Maana tumekuja kugundua mtu anaweza kuwa brain dead, na asiwe kafa. Sijui umenipata hapo? Yani hizi mashine zitamsaidia kufanya function kama kupumua na kusambaza damu. Kwa hivyo, ni kitu ambacho lazima tuwe tayari kukabiliana nacho na tuwe tayari kubadilika na nyakati na teknologia.

Kwa hiyo wewe unasema mwanadamu ni pale sperm inapokutana na egg, na sababu uliyotoa ni kuwa ndo mwanzo wa maisha yake. Sawa, Kwa hiyo wewe unavyoona mtu anayetumia 'morning after pill' na mtu anayetoa mimba ya wiki 24+ ni sawa?
 

swala la brain death nakuelewa unaongelea nini, ni swala pana hili na tukitaka tulijadili hapa labda itabidi tuanzishe thread nyingine

Okay, kuhusu “morning after pill” kwanza tuangalie inafanyaje kazi
Hii huwa administered within 72 hours baada ya kujamiiana

Kwanza inasimamisha kwa muda kazi ya ovary kutoa mayai ya uzazi
Pili ina zuia fertilization, kwa maneno mengine huzuia mbegu za kiume zisisafiri kufikia falopian tubes litakakokutana na yai la kike
Tatu iwapo fertilazion imeshafanyika morning after pill inaweza kuzuia fertilized egg kujipandikiza kwenye kuta za tumbo la uzazi

Katika hali ya kawaida yai la kike huwa hai katika fallopian tube kwa muda wa kama masaa 24 lakini mbegu za kiume (sperms) zinaweza kuwa hai ndani ya tumbo la uzazi kwa muda wa mpaka siku 5, fertilazion inaweza kutokea wakati wowote sperm hai inapokutana na yai hai, process ambayo inaweza kutokea ambapo sperms zipo hai siku 5 kabla ya yai la kike kutolewa (ovulation), au kwa maneno mengina fertilazion inaweza kutokea hadi siku tano baada ya kujamiiana, katika hali hiyo kutumia morning after pill kutafanya kazi ya kuzuia utoaji wa mayai ya uzazi au kuzuia fertilazation

Wakati mwingine morning after pill hutumiwa wakati fertilazion imeshafanyika, katika hali hiyo morning after pill inaweza kufanya kazi kwa kuzuia embyo isijipandikize katika tumbo la uzazi hivyo kukosa virutubisho na kufa, kitendo ambacho ni kukatiza uhai wa binadamu sawa na kukatiza uhai huo mimba ikiwa na wiki 24

Tofauti ni kwamba the one who choose abortion at 24 weeks is for sure terminating human life, and the one who use morning after pill may or may not be terminating human life kutegemea na mazingira niliyoelezea hapo juu
 
For that reason, human becomes human as soon as there is life in him (as soon as fertilization takes place) being small, not able to survive out of uterus, being premature etc does not make him less human,


Asante kwa kutoa maelezo sahihi juu ya matumizi ya 'morning after pill'. Going back to what u said earlier..."human life begins at fertilisation", and taking the 3rd scenerio of the workings of the 'morning after pill' - (i.e.: preventing the implantation of a fertilised egg on the uterus), Je unasema mtu huyo atakuwa ame-commit MURDER na anastahili kuhukumiwa kwa sheria za murder?
 
Kweli bro, wakati mwingine nashindwa kuelewa hao watoto wanao tetewa hapa, wakiomba tiketi ya kuingia majukwaa ya kijitu kizima huwa wanawachuja au wanawafahamu na kuwakatalia kuingia kule!?

JF inakosa radha kila kukicha...!


What do you mean? Mnamaanisha hii post ni mojawapo ya huo ujinga mnaouzungumzia? You cant be serious guys!!!!!!!!!!!!!
 
jaman nimesoma hii thread nimenyong,onyea vibaya,inagusa sana!!!!!!!!!
Tunashukuru sana kama message imekufikia na imekugusa, maana ndio lengo la hii thread.

Basi kuwa mwenye kufikisha ujumbe kwa wengine ili hii tabia ya kuua vichanga isiwepo kabisa kama si kupungua.
 
namshukuru mungu kweli zambi ya kudinya nafanya kwani sijaoa ila natumia kondomu katika vitu ambavyo sivipendi ni kuona kuwa nampeleka mtu kutoa mimba!! da ssoo yaani ukiangalia hivyo vipicha soo sad!!

lakini cha kushangaza kuwa kila rafiki yangu wa karibu niliyemuliza kuwa uliwahi kuwa karibu na msichana ambaye kwa wiki ni lazima mkutane hata kwa masaa mawili hivi angalau siku tano per wiki alinijibu kuwa ukaribu huu ulinifanya nigonge dry bila kondomu na mwisho ni mimba sijui sasa na ukimwi je tutapona kwani wengi wao walishaachana na wewe mulize rafikiyo wa karibu huu ni uchunguzi wangu na hivi ndivyo tunavyotia mimba watoto wa watu kisha tukatoe.
 
Yaani watu wanaogopa zaidi Ukimwi kuliko M'Mungu...! Duh kazi ipo!
 

unaposema MURDER kama unamaanisha kukatiza maisha maisha ya binadamu basi anayetumia morning pills to kill the embryo is commiting murder and na anatakiwa ahukumiwe sawa na na yule anayefanya abortion au aliye ua mwanamke mjamzito anavyo shtakiwa kuua watu wawili (double murder) .kumbuka pia kuna nchi ambazo mwanamke mwenye mimba hawezi kuhukumiwa kifo ili kuepuka kukatiza maisha ya binadamu asiye na hatia

Suala ni kwamba issue kubwa iliyoko sio lini binadamu awe binadamu, bali ni kwamba mama awe au asiwe na haki ya kukatiza maisha ya mtoto wake anapokuwa bado yupo tumboni, it is well known that human life starts with fertilization

Kumbuka pia kwamba kuna uuaji wa binadamu uliohalishwa kusheria , kwa mfano kuua mhalifu aliyehukumiwa kunyongwa, au mwanajeshi kuua adui vitani hawa wanaua kwa makusudi lakini hawahukumiwi kama wauaji kutegemea na sheria, vilevile ktk nchi zinazo ruhusu abortion mama anapewa haki ya kisheria kumuua mtoto wake ambaye hajazaliwa, umri wa mtoto ukitofautiana ktk nchi mbalimbali, kitendo ambacho mimi na wengine wasio kubaliana na abortion tunaona sio haki kwa mtoto - mtoto hana hatia, na hakuna anayejua for sure maisha yake yatakuwaje na ana haki ya kuishi kama binadamu….
 
kwanza kuna dhambi kadha wa kdaha mmefanya
1.kuzini
2.kuua
wacheni mapenzi kabla ya ndoa....ndio solution.....
 

Kwa nini basi hamkuweka picha za namna hii? Hizi si picha za binadamu, according to your theory? Au ni kwa sababu hazivuti hisia yeyote?
Kwa nini huyu 'binadamu' hapewi same protection by law kama wewe na mimi?
 

Attachments

  • zy1.jpg
    17 KB · Views: 45
  • Fertilized-oocyte.jpg
    9.2 KB · Views: 45
Burazaaaaa tusidanganyane. Wanawake wooote wanapojamiiiana wanajua outcomes zake, kwa hiyo kaka abortion huwa ni maamuzi yao, kwani mtoto akikataliwa na baba ndo umuuuuwe?WANAPENDA SANA UJANA HAWA, INANIUMA SANA, PUMBAVU ZAO WOTE WANAOENDEKEZA UJANA!!
 
Serikali itungie sheria suala la utoaji mimba kama ilivyotungia suala la ubakaji.
 

Hamna haja ya jazba mkuu. Tunajadili ishu kiustarabu tu.

Serikali itungie sheria suala la utoaji mimba kama ilivyotungia suala la ubakaji.

Ndo hapo hata mimi nalenga. Mpaka pale nchi itakapoamua kuwa na sheria ya kulenga hichi kitendo, huwezi kusema ni uuaji. Na sababu niliyotoa ni kuwa sio binadamu. Kumbuka, sijasema kuwa si kiumbe, bali si binadamu. Na kama utasema ni kosa kuua, basi iwe kosa nalo kuua viumbe vingine kama mti (unaung'oa), mbwa, unapovua samaki, nk. Yani kwa sababu hicho kiumbe kinakua na kubadilikuwa kuwa mwanadamu ndo kiwe-treated tofauti?
 
Mtoto unataka kunambia hivyo viumbe ulivyovitaja hapo viko kwenye process ya kugeuka binadamu?
 
Kwa nini basi hamkuweka picha za namna hii? Hizi si picha za binadamu, according to your theory? Au ni kwa sababu hazivuti hisia yeyote?
Kwa nini huyu 'binadamu' hapewi same protection by law kama wewe na mimi?

suala sio picha mkuu mtoto, hapa tunatoa mchango kuhusiana na suala la abortion, to be touched by graphics only depends on someone's understanding and interpretation of such graphics...the photos of embryo destruction can make some one burst in tears...!

huyu unayemuita "kiumbe" ana lindwa na sheria ya Tanzania na nchi nyinginezo, ndio maana wahalifu wenye mimba hawanyongwi wakiwa wamebeba mimba zao na hawaangalii ukubwa wa matumbo yao wanachoangalia ni positive pregnant test..., na ndio sababu kisheria abortion hairuhusiwi Tanzania na nchi nyinginezo, haijalishi na mimba ya mda gani

naomba unijibu haya maswali mawili
hicho kiumbe unachokitaja wewe kinageuka lini kuwa binadamu?
kabla ya kuwa binadamu kiumbe hicho unakiweka kwenye kundi gani la viumbe hai?
 

nchi gani hiyo unayoiongelea wewe?? au hujui kwamba in Tanzania abortion is illegal by law at any stage of preganancy?? exception ni kama kwenye ulazima pale ambapo termination of pregancy is medically important for the mother's life
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…