Iteitei Lya Kitee
JF-Expert Member
- Jan 2, 2008
- 586
- 47
Hapo ndipo na mimi napata shida kuelewa BJ, mtu unapata mateso, unanyanyaswa mpaka unaiona dunia Jehanamu, bado umeganda tuuuu,
Tatizo nini?? Watoto?? Mungu amekupa mikono, akili na neema ya Elimu hata kama ni ndogo, na labda una kazi yako, kwa nini usiondoke ukatafuta maisha na watoto wako??
Kama anataka watoto na anawapenda awape mahitaji yao wakiwa kwangu, then wkikua watajua pumba ni ipi na ngano ni ipi??
OK, unavumilia, ni majaribu Mungu atafanya njia lini?? Wakati presha inakuua?? Unakufa kabla ya siku zako kisa nini??
Kwanza ukijaribu kuangalia wakati unaingia kwene ndoa hukumshirikisha Mungu asilimia mia moja ktk maamuzi yako, lakini mambo yanapokuwa magumu Tunasema Mungu "umeniacha" kwene ndoa yangu.
Mungu si dhalimu jamani, "Hata pamoja na hilo jaribu nitafanya mlango wa kutokea"
We unaolewa by chance, simply coz ametokea wa kukuoa, na kwa sababu unataka kuolewa, baada ya miaka miwil/mitatu
jamaa anaona nilikosea njia, afu mbaya zaidi anakwambia kabisa, hivi ilikuwa je hadi nkakuoa wewe??
Hapo ukiangalia una watoto wawili au watatu, unabaki unasema kama sio hawa watoto, ningeondoka.
Mwanamke jipange sawasawa, tumia akili, nguvu na uwezo uliopewa na MUNGU, mkabidhi Mungu njia zako, ili hata ukikutana na milima na hayo mabonde kwene ndoa unakwenda kwa Mungu kwa ujasiri.
Hakuna sababu ya kuolewa kama, sitakuwa na furaha ktk hio ndoa.
Lakini pia ninayo Imani kabisa ya Kwamba MUME/MKE mwema hutoka kwa BWANA. Kwa majira na nyakati sahihi.
Mnisamehe!!!
Mpaka pale mungu atakapojibu. Kumbuka mungu wetu ni mwaminifu hawahi wala hachelewi, ni kwa wakati wake ndipo atajibu
Kweli PJ,
kila hadithi ina pande mbili kabla ya kutoa hitimisho. Inawezekana kuna kitu huyo bi dada katenda ambacho kimemfanya mume kuwa na vita baridi. DC hebu dodosa tupate upande wa pili wa shilingi.
Kaka angalia huyu mwanamke anakutaka, kwa nini asizungumze na mwenzake anazungumza na wewe? Na wewe kwa nini usiende kuongea na wote wawili? mademu hata kama atakuwa anaishi kwake vizuri akikurtaka atazusha mambo mengi saaana ili kukupa wewe nafasi.
Tafadhali tafadhali usije geuka badala ya kuwa mshauri ukamega mke wa mtu kama tulivyosoma hapa juzi jamaaa kala demu wa jamaa yake wakati wa ushauri.
Mpaka pale mungu atakapojibu. Kumbuka mungu wetu ni mwaminifu hawahi wala hachelewi, ni kwa wakati wake ndipo atajibu
[/COLOR][/COLOR]
Nakubaliana na wewe, na hivyo ndivyo Mungu alivyo.
Lakini lazima wakati mwingine tujiulize na tutafakari juu ya maombi tunayoomba,
Je ni kweli Mungu yupo na wewe ktk hayo unayoomba, Je unaiona nguvu ya Mungu ktk hicho unachokiomba,
Unasikia sauti ya Mungu ktk maombi yako ikikwambia songa mbele??
Jamani huyu mama kwanza haombi, kwa sababu asingekuwa anazunguka makanisa kama kweli anamjua Mungu ake, na anajua anachokiomba.
Mungu ni mwaminifu, amekupa akili, nguvu na utashi wa kuamua, chagua kuendelea kuumia kwa kisingizio cha kumngoja Mungu,
au utafute ustaraabu mwingine. Utamchukia Mungu bure, kumbe wala Mungu hahusiki ktk hilo.
Hii ni story ya mwanamke mmoja ambaye nimekutana naye katika harakati za kupeana ushauri wa kutatua matatizo yanayotusibu katika mahusiano. Amekubali niiweke hapa ili kupata maoni ya wadau. Matatizo yake ni mengi sana ila kwa ufupi ni kama ifuatavyo:
1. Suala na unyumba katika ndoa yao yenye umri wa karibia miaka 4 wakiwa na watoto 2, limekumbwa na ukame wa ajabu. Wanashiriki tendo la ndoa kama mara 2 tu kwa mwezi na ni lazima mume atake. Mwanamke akiomba anaambiwa kuwa mume hawezi kufanya tendo la ndoa mara kwa mara. Wakati wa uchumba wao na siku za awali za ndoa yao, walikuwa wakishiriki tendo la ndoa hata zaidi ya mara 2 kwa week na wote waliliridhika na kufurahia tendo hilo. Hali ilianza kubadilika baada ya kama miaka 2 hivi. Mbaya zaidi hata kama mmoja akirudi safari baada ya kukaa kwa muda mrefu kiasi cha week nzima au zaidi, bado hakuna uhakika wa tendo la ndoa!
2. Mawasiliano ndani ya nyumba hasa hasa yale ya kimahaba nalo limekuwa tatizo. Yaani ni kama vile wanaishi maktaba. Muda mwingi mume akiwa nyumbani anacheza na simu yake akituma na kupokea sms kutoka kwa watu tofauti. Pia mume akiwa nje na jamaa wengine anakuwa mchangamfu sana, akiongea na vicheko juu.
3. Vitu vingi vya mume vimefunigiwa katika mkoba (brief case) wenye password ambayo mke hajui. Pia mume anazo account za benki ambazo mke wake hazijui kabisa. Na simu za mume zimewekewa password ingawa vitu vyote vya mke ikiwemo simu, account za bank n.k viko wazi na mume anavivinjari wakati wowote anaopenda.
4. Ni nadra kwa mume kukubali na kusifia (to appreciate) kitu alichokifanya mke. Na mara nyingi anamkatisha tamaa katika mipango yake anayomshirikisha.
Kutokana na haya matatizo na mengine mengi, huyo mama amekosa raha muda mrefu na aliwahi kufikiria kujidhuru (got closer to attempt suicide) ila kwa sasa ameamua kutafuta ushauri ama wa kuokoa ndoa au maisha yake. Amesali sana, amfeunga sana na kubadili makanisa kama nguo za mashidano ya mavazi lakini bado nazunguka pale pale. Kwa hiyo wadau nawaomba ushauri wenu ili niongeze kwenye package ya counseling ninayoendelea nayo kwa sasa.
Wasalaam, ....Babu DC
Hapana mtu anapokuja kuhitaji ushauri kwako, kwanza unatakiwa uwe proud kwamba ameku consider kama mtu wa muhim kwake, mwenye hekima pia, angekua anamtaka isingekua story hii unayoisoma hapa, unatakiwa kujua DC kafikisha ujumbe tu na hakutaka kutupa more details pengine ni dadaake au mtu wa karibu, issue ikiwa haikuku touch unapotezea tu silazima kuchangia.Kaka angalia huyu mwanamke anakutaka, kwa nini asizungumze na mwenzake anazungumza na wewe? Na wewe kwa nini usiende kuongea na wote wawili? mademu hata kama atakuwa anaishi kwake vizuri akikurtaka atazusha mambo mengi saaana ili kukupa wewe nafasi.
kweli kabisa ladymya, mnaomshauri kuondoka jamani nani amewaambia kuna ndoa ya amani moja kwa moja? na je kama mama ndio alikua na makosa yaliyosababisha mume awe hivyo kuondoka ndio suluhisho? na ataondoka kwa wangapi? kwa wale wadogo zangu ambao hamjaolewa usiwaze nikiingia akinisumbua tu naondoka amini ukiingia tu unakutana na hayo masumbufu unayoyazungumza sasa. Cha msingi wadada waache kuingia kwenye ndoa kwa kulazimisha kisa ndoa ni heshima omba na subiri mungu akupe mume aliekupangia kama mungu alikuipangia kuolewa na miaka hamsini ndivyo itakavyokua ukilazimisha ndio hivyo utakuwa unaolewa na kuachika mpaka ifike siku yako mungu aliyokupangia.
Ushauri kwa huyo dada asiondoke abaki kwani mume hampigi wala kumnyanyasa anachomnyima ni huo unyumba tu kwani akiondoka huko anakoenda ndio atapata huo unyumba wa mmewe? kwanza kwa hali aliyonayo sasa sidhani kama ana hamu hata ya huo unyumba, na kwa sababu hanyanyaswi atulie tu na kuendelea kumuomba mungu
WOS,
Unasema kweli ila siyo rahisi kwa sababu huyu mama simjui na nimekutana naye online. Sana sana tunawasiliana kwa simu baada ya kuwa tumebadilishana mawazo sana. I wish we could hear from the husband. Hata hivyo anapanga kuchukua hatua, may be ataenda kwa Paroko au Wazazi na baada ya hapo labda tutaweza kupata feedback ya nini kilimsibu mume wake. Ila katika maongezi yao wawili mume amegoma kabisa kuingia kwenye mjadala huo.
Hivi kwa nini watu wengine wanakuwa na mawazo ya ngono kila wakati? Una maana haiwezekani kutoa ushauri kwa akina mama wenye matatizo ya ndoa bila ku-take advantange?
Kwa kweli watu wengine mmeniacha hoi. Nitamchukuaje mtu ambaye wala simjui na sijui anaishi wapi? Na una hakika gani kama mimi siyo mtoa ushauri kwa watu wenye matatizo mbali mbali (as a professional counselor)?
Kwa kweli nazidi kuamini kuwamba wanume tuna matatizo kuliko tunavyojitambua.
Ulichokiongea nikweli dadaangu, ang'ang'anie huku akimuomba mungu amuepushe mumewe na magonjwa, mbona yakobo alimng'ang'ania malaika mpaka akambariki. Aiombee hiyo paipu ya mumewe isisimame akiwa kwa wanawake wengine ispokua kwake tu, mungu si hana upendeleo na ukimwomba chochote anafanya aombe hivo, atairudisha mwenyewe.
Umegundua eeh tena hawa ndo wenzake huyo baba, hii post imewachomaaa.
Mimi naona tatizo hili linaanzia kwenye MSINGI. Nitafafanua kama ifuatavyo:
1.Wanandoa wengi siku hizi wanaingia kwenye ndoa bila kufuata utaratibu au wanafuata utaratibu lkn hawapati MAFUNDISHO SAHIHI ya ndoa.Ndoa ni kitu kikubwa, zaidi ya kutoshirikiana kimwili na mume kwa zaidi ya wiki mbili.
Ndoa by itself, ina maisha , yaani lifecycle(Marriage Lifecycle) kwa faida ya wengine nitaielezea kwa ufupi, kama ifuatavyo:
i. Honeymoon stage - 0 yrs to 4 or 5 yrs
ii.Torture Stg - 5 yrs to 10 yrs
iii.Torelance Stg - 10 yrs to 15 yrs
iv. Compromise Stg - 15 yrs onwards
Hii ni rule ambayo ina-exeptions vilevile , wengine honeymoon or all those other stages zinakuwa fupi sana ama kinyume chake. Hivyo huyo mama na mwenzake ni vizuri ajue yupo kwenye stage gani kati ya hizo.
2.Kuhusu ku-involve washauri/wasimamizi wa ndoa au ndugu hilo siyo sawa, kwani uzoefu unaonesha mara nyingi wana-tend kuwa biased.
3. Viongozi wa dini vilevile siyo sahihi kuwahusisha, hawa wanahusishwa pale unapo-intend ku-divorce or ku-separate , kwani baada ya hapo wanakupa kibali cha kwenda Baraza la Usuluhishi , then ikishindikana, shauri linaenda Mahakamani, hivyo tusiwe wepesi wa kushauri watu waende makanisani au misikitini, after all misikitini hawafungishi ndoa na taratibu za ufungishaji ndoa za kikristo na kiislamu, they do differ.
USHAURI
Huyo mama akae chini na kufanya self-assessment, kipi kimekwenda mrama , nini kama yeye amekosea au anatakiwa kufanya kurudisha amani, kwani the way i see it , tatizo lao liko-extended mpaka kwenye masuala ya finance. Arekebishe yale yaliyo yake , automatically , and I repeat , automatically things will start to fall in line.
ALL THE BEST
Nahisi kuna chanzo cha matatizo hayo ambacho huyo dada ama hakijui au anakificha. Hayo yaliyoelezwa hapo juu ni matokeo ya (ma)tatizo fulani. Yapasa kama huyo dada amechoshwa na hayo, arejee nyuma ajue mzizi wa tatizo na kuun'goa kisha matatizo yataisha. Kinyume na hayo, hakuna ufumbuzi wa kudumu.
Ila Dick naona umerukia kwenye hitimisho. Nadhani wengi wamesema kuwa huwezi kujua kwa uhakika kosa ni la nani. Na sidhani kama kuna mtu ameomba tutambue nani mwenye kosa katika issue hii. Kitu cha msingi ni kutoa maoni ambayo yanaweza kumwondoa huyo mama hapa alipo ili apige hatua kwenda kwenye point nyingine. Siyo ku-criminalise mtu yeyote kwa sababu sisi siyo baraza la usuluhishi wala mahakama. Ingawa maoni yetu, (na naamini hivyo) yanaweza kuwa na msaada mkubwa. Haya tuna ushahidi nao kwamba maoni ya wadau hapa JF yameweza kuwasaidia baadhi ya watu kutatua matatizo yao ambayo walidhani hayatatuliki![/QUOTE]
kweli kabisa DC kwenye issue serious kama hizi ndio za kupatia vitu ambavyo vinaweza kukusaidia na wewe yakikutokea
Sana wanaume wanamaudhi sana sasa unamnunia mwenzio ili iweje. Na huyu dada naye si atambae zake tu siku hizi hakuna cha kubembelezana kihivyo ukiboreka unaanza mbele