Hii ni story ya mwanamke mmoja ambaye nimekutana naye katika harakati za kupeana ushauri wa kutatua matatizo yanayotusibu katika mahusiano. Amekubali niiweke hapa ili kupata maoni ya wadau. Matatizo yake ni mengi sana ila kwa ufupi ni kama ifuatavyo:
1. Suala na unyumba katika ndoa yao yenye umri wa karibia miaka 4 wakiwa na watoto 2, limekumbwa na ukame wa ajabu. Wanashiriki tendo la ndoa kama mara 2 tu kwa mwezi na ni lazima mume atake. Mwanamke akiomba anaambiwa kuwa mume hawezi kufanya tendo la ndoa mara kwa mara. Wakati wa uchumba wao na siku za awali za ndoa yao, walikuwa wakishiriki tendo la ndoa hata zaidi ya mara 2 kwa week na wote waliliridhika na kufurahia tendo hilo. Hali ilianza kubadilika baada ya kama miaka 2 hivi. Mbaya zaidi hata kama mmoja akirudi safari baada ya kukaa kwa muda mrefu kiasi cha week nzima au zaidi, bado hakuna uhakika wa tendo la ndoa!
2. Mawasiliano ndani ya nyumba hasa hasa yale ya kimahaba nalo limekuwa tatizo. Yaani ni kama vile wanaishi maktaba. Muda mwingi mume akiwa nyumbani anacheza na simu yake akituma na kupokea sms kutoka kwa watu tofauti. Pia mume akiwa nje na jamaa wengine anakuwa mchangamfu sana, akiongea na vicheko juu.
3. Vitu vingi vya mume vimefunigiwa katika mkoba (brief case) wenye password ambayo mke hajui. Pia mume anazo account za benki ambazo mke wake hazijui kabisa. Na simu za mume zimewekewa password ingawa vitu vyote vya mke ikiwemo simu, account za bank n.k viko wazi na mume anavivinjari wakati wowote anaopenda.
4. Ni nadra kwa mume kukubali na kusifia (to appreciate) kitu alichokifanya mke. Na mara nyingi anamkatisha tamaa katika mipango yake anayomshirikisha.
Kutokana na haya matatizo na mengine mengi, huyo mama amekosa raha muda mrefu na aliwahi kufikiria kujidhuru (got closer to attempt suicide) ila kwa sasa ameamua kutafuta ushauri ama wa kuokoa ndoa au maisha yake. Amesali sana, amfeunga sana na kubadili makanisa kama nguo za mashidano ya mavazi lakini bado nazunguka pale pale. Kwa hiyo wadau nawaomba ushauri wenu ili niongeze kwenye package ya counseling ninayoendelea nayo kwa sasa.
Wasalaam, ....Babu DC
Mimi naona tatizo hili linaanzia kwenye MSINGI. Nitafafanua kama ifuatavyo:
1.Wanandoa wengi siku hizi wanaingia kwenye ndoa bila kufuata utaratibu au wanafuata utaratibu lkn hawapati MAFUNDISHO SAHIHI ya ndoa.Ndoa ni kitu kikubwa, zaidi ya kutoshirikiana kimwili na mume kwa zaidi ya wiki mbili.
Ndoa by itself, ina maisha , yaani lifecycle(Marriage Lifecycle) kwa faida ya wengine nitaielezea kwa ufupi, kama ifuatavyo:
i. Honeymoon stage - 0 yrs to 4 or 5 yrs
ii.Torture Stg - 5 yrs to 10 yrs
iii.Torelance Stg - 10 yrs to 15 yrs
iv. Compromise Stg - 15 yrs onwards
Hii ni rule ambayo ina-exeptions vilevile , wengine honeymoon or all those other stages zinakuwa fupi sana ama kinyume chake. Hivyo huyo mama na mwenzake ni vizuri ajue yupo kwenye stage gani kati ya hizo.
2.Kuhusu ku-involve washauri/wasimamizi wa ndoa au ndugu hilo siyo sawa, kwani uzoefu unaonesha mara nyingi wana-tend kuwa biased.
3. Viongozi wa dini vilevile siyo sahihi kuwahusisha, hawa wanahusishwa pale unapo-intend ku-divorce or ku-separate , kwani baada ya hapo wanakupa kibali cha kwenda Baraza la Usuluhishi , then ikishindikana, shauri linaenda Mahakamani, hivyo tusiwe wepesi wa kushauri watu waende makanisani au misikitini, after all misikitini hawafungishi ndoa na taratibu za ufungishaji ndoa za kikristo na kiislamu, they do differ.
USHAURI
Huyo mama akae chini na kufanya self-assessment, kipi kimekwenda mrama , nini kama yeye amekosea au anatakiwa kufanya kurudisha amani, kwani the way i see it , tatizo lao liko-extended mpaka kwenye masuala ya finance. Arekebishe yale yaliyo yake , automatically , and I repeat , automatically things will start to fall in line.
ALL THE BEST