Samawati
Member
- Oct 6, 2010
- 90
- 71
Asante FL,
Nitamfikishia ujumbe wako. Ila kwa maelezo yake..yeye ndiye humsalimia na kumpokea mume akirudi home na nyumba waliyonayo ina maji ya kutosha ikiwa ni pamoja na heater. Ila mume ni mpenzi wa kuchat na simu na kuangalia movie peke yake. Hataki usumbu wa mke. Hapo ndio anapouliza, afanye nini?
Huyu mama ananikumbusha kisa likichonipata ndoa yangu ya kwanza. Miye nliolewa nikiwa na miaka 18 ndo kwaanza namaliza kidato cha sita sijui hili wala lile. Huyo mume alikuwa kanizidi miaka 13 na alikuwa keshaonja na kujua maisha ni kitu gani. Nikazaa watoto mapacha wakati niko mjamzito tulikatazwa na daktari kushiriki tendo kwa vile watoto walikaa vibaya na tumbo lilikuwa linanisumbua sana. Kume mwenzangu alikuwa na kimada chake cha zilipendwa akawa anajipumzishia hapo. Nimejifungua, akaendelea naye na visa juu ya visa. Kukatiza stori ni kwamba sikukaa naye miaka miwili nilianza! Kuja kushtukia nishapata mtu mwingine siku nyingi. Tukaharakisha divorce, na sasa niko raha mustarehe na mume wangu wa pili. Nnachotaka kumwambia ni kuwa ndoa hiyo huenda siyo aliyoandikiwa. Ajiulize kama kweli huyo ndo mume aliyeandikiwa? Mwanaume anakutesa hakupi sex mwanaume gani nawe ni mwanamke kamili damu inachemka? Asimzingue.... akikuona wa nini wenzio husema watakupata lini! SEPAAA!!