PLO Lumumba apuuzwe kama maprofesa wengine wa Afrika

PLO Lumumba apuuzwe kama maprofesa wengine wa Afrika

Jana ndiyo kajichimbia kaburi kabisa na sasa ukikutana naye atakuwa anaongea pekee yake kama kichaa wa Lumumba @ kipara kipya
Nadhani hilo jina la Lumumba huwa lina madhara kwenye bongo zao
 
Pamoja na mambo yote hayo, ila wazee wa chadema mshaurini Lissu atulie kulinda legacy yake......siku hizi cha kuogopwa ni technologia na Mungu tu basi...........anaongea mengi na mengine yeye kama mwanasiasa binafsi naona si sawa kulinda career yake.......maana Politiksi izi e deti gemu
 
Katika mahojiano ya Jana VOA

-Anasema Vyama vya upinzani havijaenea kama CCM,kwa hiyo hii inathibitisha ushindi wa kishindo wa CCM kwenye uchaguzi mkuu 2020?
-Mbona hakuzungumza kuhusu credibility ya uchaguzi ule,ambao dunia nzima ilisema una dosari nyingi?
-Je, kuzuia Uhuru wa vyombo vya habari na demokrasia ya vyama vya siasa vya upinzani ikiwemo kufanya mikutano ya hadhara nako ni kuenea kwa CCM?
-Yeye kama mwanasheria,tena akiwa Mkenya,Tukio la Mbunge Lissu na mpinzani mkuu wa hayati Magufuli kupigwa risasi mchana kweupe,bila serikali kuonesha accountability,anaona ni sahihi?
Tunawafahamu vizuri wakenya,tukio hili lingetokea Kenya lingeweza kumtoa hata Rais madarakani.
-Alisema kila sekta ya uchumi Tanzania imekua ndani ya miaka mitano,mfano wa harakaharaka ni ATCL na TPA,haya mashirika yamekua kweli?
-Anasema ameshafika Chato,ila hawezi kuifahamu vizuri kama sisi watanzania.Miradi mingi ndani ya muda mfupi imeelekezwa kule,bila hata ya bajeti,katika mazingira hayo lazima pesa nyingi imepigwa.
-Anasema Agricultural sector imekua!
Kilimo na mifugo kimekua lini?
Bei ya mazao kama Korosho,pamba na mpunga ikoje?
Inafika mahali mtu unalima pamba halafu unakopwa!.

-Cha maana alichosema ni kuhusu Lissu kumsamehe marehemu.
Si busara sana kuendelea kumchukia marehemu magufuli,japo TL aliumizwa sana kuliko yeyote kwenye utawala wa hayati Magufuli. Jiulize risasi zote hizo?matibabu akanyimwa?ubunge kavuliwa?Kwa binadamu wa kawaida si rahisi kusahau na kusamehe haraka,ni kwa neema ya Yesu tu.

Nimejifunza kitu kuhusu PLO Lumumba:

Inawezekana kabisa huyu mzee anatumia taaluma yake na umaarufu kujipatia pesa,kwa marais fulani fulani,ili awaseme vizuri.
Na hata hivyo haifahamu vizuri katiba ya Tanzania (au anafanya makusudi).

Nimejifunza kitu pia kuhusu Tundu Lissu:

Bado ana hasira sana na hayati Magufuli na watesi wengine,na bora chama chake CHADEMA,kiangalie namna ya kumsaidia.
Kwa upande mwingine,huyu mtu ana vyanzo vingi sana vya habari vikiwemo na vya ndani ya serikali.
Alikuwa na details zote wakati wa kuugua mpaka kifo cha rais Magufuli.

Namwomba arudi Tanzania,makosa serikalini hayataisha,aendelee kukosoa na kuishauri serikali huku akiwa nyumbani.

Ni maoni yangu tu. Hayako sahihi kihivyo.
Hana tofauti na Mbunge Msukuma. Anamzidi kingereza tu.
 
Pole sana kwakuwa hakusema mnayoyapenda kuyasikia?

Hivi CHADEMA kwenu nyinyi ni maana ya haya maneno?

Demokrasia?
Uhuru wa maoni?
Uhuru wa vyombo vya habari?

Nauliza hili swali kwakuwa nimekuwa naona haya maneno mnayapenda pale mnapokuwa mnafurahishwa na muktadha fulani na kama ni jambo basi ni lile linalo wafurahisha nyinyi!
Ruta pole sana kaka. Naona huko mnapukutika kama mchwa.
 
Back
Top Bottom