Pre GE2025 PM Majaliwa: Rais Samia ni Tiba ya Maendeleo, hakuna mbadala

Pre GE2025 PM Majaliwa: Rais Samia ni Tiba ya Maendeleo, hakuna mbadala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Shida sio Kodi zenu Bali matumizi ya hizo Kodi zenu.

Pia hakuna anaelipa Kodi Kwa hiari Bali ni takwa la kisheria
Sawa, hebu eleza jinsi hao ambao hatujawapa kodi zetu walivyoweza kuzitumia vibaya hizo kodi zetu, hapo tutaweza kufananisha walivyoweza kutuletea au kutokutuletea maendeleo japo wote tuliwapa pesa sawa.
 
Sawa, hebu eleza jinsi hao ambao hatujawapa kodi zetu walivyoweza kuzitumia vibaya hizo kodi zetu, hapo tutaweza kufananisha walivyoweza kutuletea au kutokutuletea maendeleo japo wote tuliwapa pesa sawa.
Mifano Iko Mingi sana eg umewahi ona ripoti ya CAG ikisema rushwa imepungua kwenye awamu hizo?

Pili ni akili za wapi kutumia 27T kujenga Sgr harafu ukaacha Nchi Ina 80% ya Barabara za mavumbi na hazipotiki?

Hiyo ni mifano ya watu wasio na akili.
 
Mifano Iko Mingi sana eg umewahi ona ripoti ya CAG ikisema rushwa imepungua kwenye awamu hizo?

Pili ni akili za wapi kutumia 27T kujenga Sgr harafu ukaacha Nchi Ina 80% ya Barabara za mavumbi na hazipotiki?

Hiyo ni mifano ya watu wasio na akili.
Hawa wote na aliyepo nani ameweza kubadili maisha yetu, naona bado tupo kwenye mlo mmoja usio na uhakika.
 
Hawa wote na aliyepo nani ameweza kubadili maisha yetu, naona bado tupo kwenye mlo mmoja usio na uhakika.
Walau JK na Samia ndio wameweza Kwa vitendo.

Mkapa na Mwinyi waliweka msingi,yule mwingine aliharibu Uchumi
 
My Take
Nakubalina na PM 💯 💯

Kwenye suala la Maendeleo Samia hana mshindani Kila mtu anaona huko aliko 👇👇

---
RAIS DKT. SAMIA NI TIBA YA MAENDELEO – MAJALIWA

▪️ Waziri Mkuu asema Rais Dkt. Samia amedhamiria kutekeleza na kukamilisha miradi yote ya kimkakati.
▪️ Aeleza kuwa Rais Dkt. Samia ni kiongozi anayeona, kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.
▪️ Atoa wito kwa wananchi kuendelea kuiunga mkono CCM kwa weledi na uaminifu.
▪️ Asisitiza kuwa CCM imeleta, inaleta na itaendelea kuleta maendeleo nchini.
▪️ Asema chama hicho kinasema, kinaahidi na kinatekeleza.

Maswa, 16 Februari 2025 – Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni "tiba ya maendeleo" kwa Watanzania kutokana na jitihada zake za kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoboresha maisha ya wananchi.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo la Maswa Mashariki, uliofanyika katika Uwanja wa Nguzo Nane, Maswa, mkoani Simiyu, Waziri Mkuu amesema kuwa Rais Dkt. Samia ni kiongozi mwenye maono makubwa, anayeona, kusikiliza na kutatua changamoto za Watanzania kwa ustadi wa hali ya juu.

"Rais Dkt. Samia amejidhihirisha kama kiongozi shupavu mwenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo. Anafanya kazi kwa bidii kuhakikisha miradi yote ya kimkakati inatekelezwa na kukamilika kwa wakati, huku akihakikisha wananchi wananufaika na huduma bora za kijamii," alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa CCM itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli, kwa kuwa ndicho chama chenye dira na dhamira ya kuwatumikia wananchi kwa weledi na uaminifu mkubwa.

"CCM ni chama kinachosema, kinaahidi na kinatekeleza. Tumekuwa tukitekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali kama afya, elimu, miundombinu, maji na umeme. Chama hiki kimeleta maendeleo, kinaendelea kuleta maendeleo na kitaendelea kuongoza kwa maendeleo," alisisitiza Waziri Mkuu.

Aliwataka wananchi waendelee kuiunga mkono Serikali inayoongozwa na CCM kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakuwa na tija kwa jamii.

Imetolewa na:

Idara ya Siasa na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi (CCM) – Mkoa wa Simiyu
Premier Chawa, naye huyo ni chawa tu kama chama wengine.
 
Premier Chawa, naye huyo ni chawa tu kama chama wengine.
Chawa wa maendeleo
20250225_172459.jpg
20250225_140614.jpg
20250225_140623.jpg
20250224_061924.jpg
 
Yaani unalima wewe kisha unamshukuru mama Samia kwa kupata mazao! Sina fungu la kukuweka.
Unajitoa ufahamu 😂😂
-Uhakika wa soko ,sera zinazotuhakikishia bei nzuri
-Suppoet ya pembejeo za ruzuku

Una swali jingine? 🤪🤪
 
!kikamilisha miradi ya Reli ya SGR kufika kanda ya ziwa na Kigoma nimekaa paleee
 
Back
Top Bottom