Bonnie1974
JF-Expert Member
- Mar 19, 2008
- 407
- 17
HiLeo nimekuja na ombi lingine. Hivi mwanamke (mama wa nyumbani)anastahili au hastahili kupewa pocket money ya kujinunulia vitu vyake vidogo mpaka aviorodheshe kwenye list ya vitu vya mwisho wa mwezi! Kwa kweli hili jambo linanishangaza sana kwa huyu bwana maana kupewa hio pesa ni mpaka uiombe kwa nguvu sana ikibidi na ugomvi juu yake. Sasa mume asimpompa mke pesa ategemee akapate wapi! ukiuliza kwa nini hakupi hiyo pocket money kila mwezi anakaa kimya tuu, ukimuuliza haujui kwamba anatakiwa kufanya hivyo anasema anajua. Sasa jamani mtu kama huyu aelewekeje! naombeni msaada tafadhali.
Model ni ileile, haijalishi upo ughaibuni au TZ.Wenzio huku wanaongeza gharama za matumizi ya kila siku kwenye ile hela inayoachwa nyumbani kama matumizi ya siku.
Sitisha mpango wa kukopa fedha kutoka kwa mama yako.
Maliza masomo, tafuta kazi ukimshirikisha mwenzangu.