Poda imeniponza, amegoma kunielewa

Poda imeniponza, amegoma kunielewa

Usiku huu wakati narejea magetoni, shemeji yenu amecharuka na hataki kuelewa lolote, anadai nimetoka kukutana na mwanamke mwingine.

Sababu ni harufu ya Poda ambayo imebaki mwilini mwangu, kweli sijakataa nanukia Poda.

Lakini Kama mnavyojua mchezo wa pool table, Ni lazima utumie Poda ili kurahisisha fimbo kuteleza mkononi, na hiyo ndyo sababu ya kubaki na harufu kali ya Poda.

Najitahidi kuzima huu moto lakini naona bado haiwezekani, leo nimeyatimba.......
Kwanini usimpeleke site aone powder inavyotumika,unatumie maguvu buda
 
Hakuna nguvu iliyo tumika, ila ipo siku nitamuonesha aone uhalisia
Kwani ni first time unacheza PT kw powder?,hayo alitakiwa ayajue from day one kwenye orientation ya mambo uyapendayo, na yale uyafanyayo muda wa ziada.
 
Na hizi Poda hata ukioga bado harufu inabaki, sasa tumelala anasema eti "sogea huko na mapoda yako" yani ni manyanyaso usiku mzima
Ondoka nenda away lala huko siku tatu mwambie poda hazijaisha🤣🤣
 
Back
Top Bottom