Point za madaraja - Matokeo ya form four yako kisiasa zaidi

Acha umburula mtoa mada kuwa makini naona hata wachangiaji wengi wameshindwa kuthink big. Kuna kitu kinaitwa Penalty au sio, hususani ukifeli Mathematics.
Nawe unajiona umethink big, wakati umeshindwa kulinganisha, angalia shule ya wigamba mwenye number, 0088 na 0101 wote wana F ya B math ila wana division 4 wakati mmoja anapoints 45 na mwingine 43 wakati number 0082 anapoints 45 ila yeye amepewa division 0 pomoja na number 0095 mwenye points 43 pia ana 0 labda kama wanavigezo vingine sio mathematics japo nilihisi ni C ya kiswahili ila nimeona number0001 kwa Dr nchimbi ana points 43 na hana C ya kiswahili ila amepewa div 4
 
mimi nimeona hizi point zilivyochanganyika jana nikashangaa. ni uzembe mkubwa sana. mbona wanakusanya hela nyingi sana za hii necta wanashindwa vipi kufanya kazi kwa ufanisi?
 
aise hili ni janga,yani hii tabia ya mradi liende wakifika mkazini ufanisi utakua ni mdogo sana
 
mods Invisible fanyeni RAIS apate ujumbe huu. Twatoa siku 1 tu. 24hrs.
Masikitiko makubwa.
Najua watu wa media wapata haya madudu.
 
Last edited by a moderator:
Acha umburula mtoa mada kuwa makini naona hata wachangiaji wengi wameshindwa kuthink big. Kuna kitu kinaitwa Penalty au sio, hususani ukifeli Mathematics.

acha ujinga ,tumeyafuatilia kwa makini haya matokeo. Hakuna cha penalty. Ingia na wewe uone maajabu.
 
kama sio nchi yao vile wanafanya watakavyo tu. Soon watakiona cha moto ..... Inauma sana ,kwa hali hii tutaweza kushindana katika soko la ajira na majirani zetu?
 
Duuuh hii imezid yaan ni bora huu mtihan urudiwe tena au mitihan isahihishwe upya maana haya matokeo ni lugha kugongana.

KWELI UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI
 
Walimu wenyewe wa siku hizi majanga tu, hawana lolote, kazi kudai mishahara tu utadhani wabunge wa bunge la katiba. Lakini kazi hawawezi, bure kabisa hii

Kwani walimu ndo wanapanga hizo grades ? Wakishasahihisha kazi inabaki kwa baraza. hivyo Nadhani haitakuwa vizuri sana kuanza kuwabebesha pengine lawama.
 
Duuuh hii imezid yaan ni bora huu mtihan urudiwe tena au mitihan isahihishwe upya maana haya matokeo ni lugha kugongana.

KWELI UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI

Ni hatari, yaani huku mtaani matokeo yameleta shida sana kueleweka hasa kwenye div IV na ZERO! Ni formula gan imetumika kuweka division coz point 42 na 43, wana zero huku wenzao wenye same point na wengine mpaka point 45 wana IV! NECTA, toeni majibu tafadhali..
 
Yaani ilimu imeshuka saana. Inasikitisha Kuona Tabora boys, ilboru , kibaha zikiwa hoai.
 
nikimaliza elimu hii nitaweka vyeti vyangu ndani na kuugeukia ujasiliamali siwezi kwenda kugombea kazi na watu wenye elimu hii ya leo nasema maarifa ndicho kitu muhimu kwangu vyeti sivihitaji sana ila sasa naona maarifa hayazingatiwi ila vyeti ndio muhimu
 
Tanzania ingekua daladala ningeshashuka zamani, maana 2napelekwa kusikojulikana.
 
Kwa kweli haya matokeo yanatisha sana, ila nashangaa kuona hata wadau wa elimu wamekaa kimya, waziri wa elimu ana haki ya kujiuzuru!!!!! upuuuuzii mtupu !!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…