Points 10 za ujenzi: baridi kwenye jengo

Points 10 za ujenzi: baridi kwenye jengo

1.V.O.C hupatikana katika matilio nyingi ndani ya nyumba kuliko Rangi .
Mf.mafuta ya kula,Varnishes,Perfumes,Sprays, Dawa za kupuliza za kuua wadudu,samani za mbao,makapeti na mazuria

- Why Oil paint...?
Hairuhusu Unyevu/Mvuke kuwa absorbed, ambapo inaweza kutorosha joto kwenye kuta.
-Ukuta wa rangi za mafuta hung'aa,ambapo ina maajisha mwanga/joto unadunda na kubaki ndani.
-Rangi za mafuta hazipigwi marufuku ila baadhi ya malighafi ndiyo zakatazwa kuwekwa and maboresho yanafanywa kila leo.

Pitia
Heat transfer
Light & Heat reflection
V.O.C
Matilio ndio nini? Sijawahi kusikia mtu anaambiwa apake rangi ya mafuta ili ipunguze baridi ndani ya nyumba yake.
Marekani majimbo ya New York, New Jersey, Pennsylvania, Virginia, Maryland na DC yamepiga marufuku oil based paints kwa jumla na sio ingredients zake tu.
Haujui unachoongea ( mbaya zaidi haujui kuwa haujui)na unanipotezea muda.

Amandla...
 
Sijui unazungumzia heat pump za aina gani. Vitu muhimu vya kuzingatia ni kubwa ( volume) ya eneo unalotaka kuliongezea joto, idadi, ukubwa na aina ya madirisha na kiasi cha baridi kilicho nje ( sio ndani unavyosema). Heat pump inavuna joto kutoka hewa ya nje ambayo inakuwa compressed kuiongezea joto kabla ya kusambazwa ndani. Sina uzoefu na portable heat pumps kwa hiyo siwezi kuzizungumzia. Kitu kingine muhimu sana kujua ni kiasi gani nyumba yako imekuwa insulated ili kuhakikisha hewa yenye joto haipenyi kwenda nje.
Yote kwa yote, kabla haujanunua heat pump tafuta mtaalam akushauri ipi itakufaa kulingana na ukubwa na hali ya nyumba yako.

Amandla...
Unasema hauwezi jua na hapo hapo una shauri, dah...
Kabla hauja andika hebu pitia hata video youtube kama ni ngumu wa kusoma.

Calculations zinajikita kwenye joto la ndani, kwani ndiyo tunalotaka kuongeza.
Sasa unapiga hesabu ya joto la nje ili iweje...

Hebu pitia usome
 
Cavity wall kuwa na Tiers ,hizo ni ishu za structure, mimi natoa mapendekezo kwa ufupi.
Ndiyo maana kwenye makal zangu nahimiza kukutana na watalaam ili kufanikisha jambo lao...
-Kutoweka matilio sio shida, kuweka ni kuongeza KINGA zaidi.
Zinazowekwa kwenye cavity wall ni ties na sio tiers. Ties zinawekwa kuunganisha zile kuta mbili na kuzi stabilize. Zamani zilikuwa ni viwaya hivi vya chuma vilivyokunjwa kama kipepeo. Siku hizi viko vya aina nyingi.

Amandla...
 
Unasema hauwezi jua na hapo hapo una shauri, dah...
Kabla hauja andika hebu pitia hata video youtube kama ni ngumu wa kusoma.

Calculations zinajikita kwenye joto la ndani, kwani ndiyo tunalotaka kuongeza.
Sasa unapiga hesabu ya joto la nje ili iweje...

Hebu pitia usome
Kumbe umesoma university ya You Tube!!!!
Mimi natoa ushauri kwenye vile ninavyojua na sioni aibu kusema hiki sina uzoefu nacho au sikijui kabisa.
Heat pump inavuna joto kutoka hewa iliyo nje ya jengo ndio maana unahitaji kujua temperature yake. Au university yako ya You Tube imekuambia heat pump inatoa wapi joto?

Amandla...
 
Mimi sibishani. Ninapenda sana kujifunza lakini kwa bahati mbaya hauna cha kunifundisha. Ningekuamini zaidi kama ungenitajia vitabu vinavyohusu ujenzi katika maeneo ya baridi na sio kunitaka nisome kuhusu specific heat (capacity) ya materials na latitudes na longitudes! Sadly, umecram tuu vitu bila kuvielewa.
Shida ya watu kama wewe unasahau kuwa hii ni www hivyo inabidi kuwa muangalifu na kitu unachokiandika hasa unapoingilia taaluma za watu.

Amandla...
Umekuja na kebehi na ngebe na majivuno....
Well,mkuu nimekaa kwenye mikoa ya baridi for 7 years,nimeshafanya hizo projects, na nina update ujuzi kila napopata nafasi....

Nd ndiyo maana nkakwambia kabla ya kubisha ni heri ukapitia, Makala mitandaoni,soma points nilizokupa au hata pitia video....

Sasa kama mwenye taaluma haujui jinsi Orientation ya jengo inavyochagiza baridi au joto...kwenye jengo.
Nakuelkeza na nakuambia pitia.

Tena hata mifano ukitaka una tajiwa.
 
Zinazowekwa kwenye cavity wall ni ties na sio tiers. Ties zinawekwa kuunganisha zile kuta mbili na kuzi stabilize. Zamani zilikuwa ni viwaya hivi vya chuma vilivyokunjwa kama kipepeo. Siku hizi viko vya aina nyingi.

Amandla...
Mkuu,I know about them, hizo ni ishu za structure,,,
Yani,siwezi nikajaza hizo taarifa kwenye makala ya kuhusu ishu za joto.
Naandaa makala kuwapa end users maono na siyo Lectures,hilo lazima uelewe.
 
Umekuja na kebehi na ngebe na majivuno....
Well,mkuu nimekaa kwenye mikoa ya baridi for 7 years,nimeshafanya hizo projects, na nina update ujuzi kila napopata nafasi....

Nd ndiyo maana nkakwambia kabla ya kubisha ni heri ukapitia, Makala mitandaoni,soma points nilizokupa au hata pitia video....

Sasa kama mwenye taaluma haujui jinsi Orientation ya jengo inavyochagiza baridi au joto...kwenye jengo.
Nakuelkeza na nakuambia pitia.

Tena hata mifano ukitaka una tajiwa.
Kumbe experience yako ni kwa sababu umekaa kwenye mikoa yenye baridi Tanzania? Nitarudia tena, hamna point ulizonipa. Mtu anaejua masuala ya thermal comfort ya jengo hawezi kuniambia nikasome kuhusu latitude, equinox n.k. bila kusema zinahusika vipi na majengo.
Wewe sana sana ni Fundi Mchundo kama mimi. Tofauti yetu mimi ninajijua sijui kila kitu kwa hiyo nakubali kukosolewa.

Amandla...
 
Kumbe umesoma university ya You Tube!!!!
Mimi natoa ushauri kwenye vile ninavyojua na sioni aibu kusema hiki sina uzoefu nacho au sikijui kabisa.
Heat pump inavuna joto kutoka hewa iliyo nje ya jengo ndio maana unahitaji kujua temperature yake. Au university yako ya You Tube imekuambia heat pump inatoa wapi joto?

Amandla...
So usicho kijua ndiyo hautaki jifunza,,,
Aya,mkuu....
Mimi hata nikutane na fundi,akiniambia kitu nisichojua lazima nikapekue kurasa...

Trust me,kasome pale nilipo kuelekeza kuna vitu utajifunza kuliko kubishana.
 
Mkuu,I know about them, hizo ni ishu za structure,,,
Yani,siwezi nikajaza hizo taarifa kwenye makala ya kuhusu ishu za joto.
Naandaa makala kuwapa end users maono na siyo Lectures,hilo lazima uelewe.
Tena uliziita double wall badala ya cavity wall. Ties ni sehemu muhimu ya cavity wall na zinawekwa tuu na mafundi.
Tatizo ya madarasa mnayotoa humu ni kuwa watu wanayabeba hivyo hivyo bila kujiongezea. Unapomwambia mtu apake rangi ya mafuta ndio itamuongezea joto, atapaka halafu atashangaa atakapojikuta bado anahitaji blanketi.
Humu, humility ni important na sio dhambi kukiri kuwa hauelewi kila kitu katika jambo fulani.

Amandla...
 
Kumbe experience yako ni kwa sababu umekaa kwenye mikoa yenye baridi Tanzania? Nitarudia tena, hamna point ulizonipa. Mtu anaejua masuala ya thermal comfort ya jengo hawezi kuniambia nikasome kuhusu latitude, equinox n.k. bila kusema zinahusika vipi na majengo.
Wewe sana sana ni Fundi Mchundo kama mimi. Tofauti yetu mimi ninajijua sijui kila kitu kwa hiyo nakubali kukosolewa.

Amandla...
🤣🤣🤣😂😂😂
Kukuondoa Shaka mkuu,nachokiandika nimekisomea ,nimekiishi na kukifanyia...

Sasa kama unakubali kukoselewa, kubali na kufanya tafiti ya niliyokwambia.
 
So usicho kijua ndiyo hautaki jifunza,,,
Aya,mkuu....
Mimi hata nikutane na fundi,akiniambia kitu nisichojua lazima nikapekue kurasa...

Trust me,kasome pale nilipo kuelekeza kuna vitu utajifunza kuliko kubishana.
Kasome kuhusu Heat Pump na utajua joto linatoka wapi. Kwenye nji za baridi joto hilo linafuatwa kwenye udongo.
Naona bado unakazania kuwa nikisoma kuhusu specific heat ya materials, maana ya longitude na latitude basi ndio nitajua kuhusu ujenzi bora katika sehemu za baridi! Hauko serious. Ungekuwa umesomea kama unavyodai, ungetaja vitabu na authors wake vinavyohusu ujenzi katika maeneo yenye baridi. Ati nisome specific heat ya material ndio nijue!
Unajua ukuta wa Trombe?

Amandla...
 
Hebu soma Makala zangu,nahimiza watu kutumia wataalam....

Jaribu kuandika makala ya kitaaluma uone jinsi ilivyo ngumu kwenye kuweka lugha nyepesi.

Tena uliziita double wall badala ya cavity wall. Ties ni sehemu muhimu ya cavity wall na zinawekwa tuu na mafundi.
Tatizo ya madarasa mnayotoa humu ni kuwa watu wanayabeba hivyo hivyo bila kujiongezea. Unapomwambia mtu apake rangi ya mafuta ndio itamuongezea joto, atapaka halafu atashangaa atakapojikuta bado anahitaji blanketi.
Humu, humility ni important na sio dhambi kukiri kuwa hauelewi kila kitu katika jambo fulani.

Amandla...
 
Kasome kuhusu Heat Pump na utajua joto linatoka wapi. Kwenye nji za baridi joto hilo linafuatwa kwenye udongo.
Naona bado unakazania kuwa nikisoma kuhusu specific heat ya materials, maana ya longitude na latitude basi ndio nitajua kuhusu ujenzi bora katika sehemu za baridi! Hauko serious. Ungekuwa umesomea kama unavyodai, ungetaja vitabu na authors wake vinavyohusu ujenzi katika maeneo yenye baridi. Ati nisome specific heat ya material ndio nijue!

Amandla...
😂😂😂🤣🤣🤣
Okay tufanye sijasoma ufurahi,
1.now Joto lazalishwa kwa umeme,Radiation tu.
Just type portable radiators, zinauzwa hadi kariakoo

2.pia njia nyingine kubwa ni kutoka kwenye Boilers (maji huchemshwa,na kuzalisha joto kupeleka kwenye radiators)
Commonly used in Amerika.
-Kwenye Rmani za America Utakuta kuna (Boilers' Room).
 
1. Sikuzungumzia asbestos kwenye rangi. Rangi za mafuta zina VOC ( Volatile Organic Compounds) na ingredients nyingine zinazoweza kusababisha cancer mtu ukiwa exposed nayo ndio maana kuna majimbo Marekani yamepiga marufuku na matumizi yake yanakuwa phased out. Nisichokielewa ni kwa nini unadai kuwa oil paints zinasasaidia kupunguza baridi ndani ya nyumba.
2. Kioo kinaruhusu mionzi ya joto (infra red rays) pamoja na rays nyingine kuingia lakini haviruhusu IR kurudi tena nje na hivyo kuongeza joto ndani ya chumba. Hii inaitwa Greenhouse effect. Unene wa kioo hauna impact kubwa katika kupunguza heat transfer. K.m. kioo chenye unene wa 0.7 inch kinapunguza heat loss kwa asilimia 0.1 ukilinganisha na kioo chenye unene wa 0.1 inch. Na kumbuka kioo kinene ni kizito zaidi na hivyo kukifanya kuwa kigumu kukiweka kwenye shata.
3. Double glazed ( vioo viwili vyenye nafasi kati yake) ni bora zaidi katika kupunguza upoteaji wa joto ya ndani ya nyumba ( vinapunguza upoteaji huo kwa asilimia 80 ukilinganisha na kioo kimoja chenye unene unaofanana). Siku hizi hiyo nafasi ya kati inajazwa gesi ili kupunguza zaidi upotevu wa joto. Triple glazed glasses zinatumika kwenye maeneo yenye baridi kali ambayo hayapo Tanzania.
4. Kingine cha kuzingatia katika utengenezaji wa madirisha ni kutokuwa na nafasi zinazopenyeza hewa dirisha likifungwa. Lakini unatakiwa kuzingatia kuwa ni muhimu sana kwa hewa fresh kuingia ndani ya nyumba hivyo 100 sealing haiwi recommended.
5. Ujenzi wa kuta mbili unaitwa "cavity wall construction" kwa sababu ya ile gap ( inchi mbili hivi) inayokuwepo kati ya kuta. Kuta hizi zinaunganishwa na "ties". Ujenzi wa kuta hizi unahitaji umakini sana kuhakikisha mortar na takataka nyingine hazidumbukii katika hiyo nafasi na hivyo kutengeneza daraja la ku transfer joto na umande kati ya hizo kuta mbili. Siku hizi hizo gap zinajazwa na insulating materials. Kwa vile ni ujenzi ambao haujazoeleka Tanzania utapata taabu sana katika ufungaji wa madirisha na milango. Cavity walls zinatumika kwenye kuta za nje tu.
6. Kitu muhimu katika paa sio aina ya bati bali insulation inayowekwa chini yake ili kuzuia upotevu wa joto. Insulation ni nzuri vile vile kwenye nyumba zilizokuwa air conditioned. Insulation iwe na unene wa kati ya sm 5 na 10. Hizi bidhaa zinapatikana Tanzania.
7. Kama umejenga kwa zege, ni vizuru vile vile kuweka insulation.

Amandla...
So Unasema paa la Vigae na paa la bati zote kiwango cha kutpisha joto ni sawa....dah
 
Kasome
A
1.Principals of architecture Design by D.K Ching
Na Architect's Data by Neufert....
Hapo utajifunza Orientation ya jengo inavyosaidia Jengo.

2.Architecture of light by Sage Russell, ujifunze kuhusu light.

3.Buidling Constructio by D.K Ching
Kuna good notes juu ya Heat na Fenestation

B
1.Fanya Case studies kwenye Majengo ya Shule zilizojengwa na wakoloni, check Orientation zake na madirisha na majengo ya NHC.

2.Uwe unatoka nje ya Dar,kwenda mikoa ya baridi...

C.
1.Kama haujui/hauna uhakika fanya upekuzi au hata uliza kwa wengine...

2.Updates sana ulivyosoma shule.
 
😂😂😂🤣🤣🤣
Okay tufanye sijasoma ufurahi,
1.now Joto lazalishwa kwa umeme,Radiation tu.
Just type portable radiators, zinauzwa hadi kariakoo

2.pia njia nyingine kubwa ni kutoka kwenye Boilers (maji huchemshwa,na kuzalisha joto kupeleka kwenye radiators)
Commonly used in Amerika.
-Kwenye Rmani za America Utakuta kuna (Boilers' Room).
Radiators ni tofauti kabisa na heat pumps. Nilikuwa nashangaa hiyo bei uliyotoa ya heat pump kumbe ulikuwa unazungumzia radiators!
Heat pump zinavuna joto kwenye hewa na sio kupitia umeme, gas au kitu kingine. Kwa sababu zinavuna joto basi matumizi yake ya umeme ni madogo kulinganisha na heaters au radiators.
Boiler room maana yake tuu ni kuna mtungi wa maji ambao unapashwa joto na hayo maji ya moto yanasambazwa vyumbani ili kuvipasha joto. Huo mtungi (boiler)unapashwa moto kwa makaa ya mawe, kuni, gesi au umeme. Mara nyingi inatumika pia kusambaza maji ya moto kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Boilers huwa zinaunganishwa na radiator ambamo maji ya moto yanapita na hivyo kukipa joto chumba. Mara nyingi boiler room inakuwa kwenye basement.

Amandla...
 
Kasome
A
1.Principals of architecture Design by D.K Ching
Na Architect's Data by Neufert....
Hapo utajifunza Orientation ya jengo inavyosaidia Jengo.

2.Architecture of light by Sage Russell, ujifunze kuhusu light.

3.Buidling Constructio by D.K Ching
Kuna good notes juu ya Heat na Fenestation

B
1.Fanya Case studies kwenye Majengo ya Shule zilizojengwa na wakoloni, check Orientation zake na madirisha na majengo ya NHC.

2.Uwe unatoka nje ya Dar,kwenda mikoa ya baridi...

C.
1.Kama haujui/hauna uhakika fanya upekuzi au hata uliza kwa wengine...

2.Updates sana ulivyosoma shule.
1. Kitabu cha Francis DK Ching kinaitwa Architecture: Form, Space and Order. Hizo principles ziko ndani. Kitabu kizuri zaidi cha Francis D K Ching kinaitwa Green Building Illustrated alichoandika pamoja na Ian M Shapiro. Hivi vitabu ni vya level ya mwanzo tu.
2. Neufert anakupa tu basic principles.
3. Building Construction cha Francis DK Ching kinakupa basics tu za ujenzi.
4. Mimi nimesoma kwenye shule za mawe zilizojengwa na wakoloni. Na nimeishi pia ndani yake.
5. Majengo yapi ya NHC ni mfano wa kuigwa? Lile lililo karibu na Aga Khan?

Kwa taarifa yako nimezaliwa kwenye baridi.

Narudia tena, inaelekwa kuwa umevisoma hivyo vitabu lakini haujavielewa.

Amandla...
 
So Unasema paa la Vigae na paa la bati zote kiwango cha kutpisha joto ni sawa....dah
6. Kitu muhimu katika paa sio aina ya bati bali insulation inayowekwa chini yake ili kuzuia upotevu wa joto. Insulation ni nzuri vile vile kwenye nyumba zilizokuwa air conditioned. Insulation iwe na unene wa kati ya sm 5 na 10. Hizi bidhaa zinapatikana Tanzania.
Wapi niliposema vigae na paa la bati vina viwango sawa vya kupitisha joto. Nilichosema kuwa kwenye paa kilicho muhimu zaidi kuliko aina ya paa ni insulation. Inakisiwa kuwa karibu robo ya joto lote ndani ya nyumba linapotea kupitia kwenye paa. Ndio maana nilikuambia jaribu kujifunza kutoka kwa wagogo ambao paa zao ni za udongo na zimepandwa majani hivyo joto halipotei. Dodoma kuna baridi sana usiku.
Badala ya kukazania tuu kuangalia picha za nyumba za marekani na za wakoloni angalia nyumba za wenyeji zilijengwaje. Utajifunza namna ya kupata hali ya hewa nzuri bila kutumia heat pump.

Na usiwe muongo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom