Pokea pesa kutoka Paypal kuja M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money

Haja address tatizo bado kwasababu inaelekea hata chanzo cha tatizo hajakijua.
Tatizo ndio hilo paypal TZ hata malipo haipokei. Sasa unahamishaji pesa amnayo hujapokea
Aisee watanzania, hebu rudia kusoma nilichoandika ndugu, nimesema nafikiria kutengeneza sijasema kuwa tayari inawezekana
 
Aisee watanzania, hebu rudia kusoma nilichoandika ndugu, nimesema nafikiria kutengeneza sijasema kuwa tayari inawezekana
Shida ni PayPal wao kama wao kuondoa hiki kitu na ni pale kanuni za miamala zitakapobadilishwa nchi hii.
Sasa utawezaje kufanya PayPal TZ accounts zipokee pesa kwa kutengeneza mkuu?
 
Asante kwa wazo lako 🙏. Nategemea mapendekezo mengine kama haya. Kwa pamoja tutaweza.
 
Shida ni PayPal wao kama wao kuondoa hiki kitu na ni pale kanuni za miamala zitakapobadilishwa nchi hii.
Sasa utawezaje kufanya PayPal TZ accounts zipokee pesa kwa kutengeneza mkuu?
Nitafanya juu chini kupata solution
 
Wazo lako ni zuri sn na utakapofanikiwa tu Naomba unitonye mkuu maana binafsi nimeshapigania sn issue ya PayPal bila mafanikio. Kimsingi tuko wengi tu tunaotamani huduma ya PayPal nchini. Kikwazo ni viongozi wetu tuliowachagua wenyewe. Viongozi wa serikali hii hawana uelewa juu ya biashara za mtandaoni. Kwao wao wanaposema suala la fursa kwa vijana wanaangazia zaidi machinga, bodaboda, mama ntilie na biashara ndogondogo za bidhaa za kusindika.
Nirudi kwako, kwa kuanzia Si itabidi awali ya yote uwafikishie wazo lako hili BOT? BOT hii hii ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo miaka yote hii imetugomea kutusikiliza! Aisee watakuelewa kweli?
Labda tuvizie siku Mama anafanya uzinduzi mahali tuwape dili mtu2/3 waende na bango.
 
Wadau, Naona fursa za uchumi zinazidi kukua na Kuna dalili za mabadiliko makubwa ktk nyanja ya biashara za kimataifa. Vipi hili suala letu? Kuna mwenye kujua ni lini mama atatusikiliza nasi? Msaada wako Pascal Mayalla tafadhal. Neno lako ni lenye kusikilizwa na wengi mkuu
 
Ngoja tumuombe mangekimambi atusadie ku push hili
 
Hivi kuna mtu aliewahi kufanikiwa kutoa pesa kutoka paypal kwa kutumia website ya Xoom aka-ingiza direct kwenye airtel money m-pesa halopesa au tigo pesa?
kama jibu ni ndio ebu ni-PM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…