Poland: Rais apiga marufuku Sheria ya Vyombo vya Habari

Poland: Rais apiga marufuku Sheria ya Vyombo vya Habari

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Rais wa Poland Andrzej Duda leo ametumia kura yake ya turufu kukataa sheria tata ya umiliki wa vyombo vya habari ambayo wakosoaji wanasema inalenga kunyamazisha kituo cha habari cha TVN24 kinachomilikiwa na Marekani.

Katika taarifa kupitia televisheni, Duda amesema kuwa ameipinga sheria hiyo kufuatia shutuma kutoka kwa Umoja wa Ulaya na Marekani.

Sheria hiyo iliyoidhinishwa na bunge mwezi huu, ingezizuia kampuni kutoka nje ya Umoja wa Ulaya kuwa na hisa za kuiwezesha kuwa na kauli ya mwisho katika kampuni za vyombo vya habari nchini Poland.

Duda anasema amekubaliana na kanuni hiyo lakini haipaswi kutumika kwa mipango iliyopo ya biashara na mikataba ya uwekezaji.

Rais huyo wa Poland ameongeza kuwa watu aliozungumza nao wana wasiwasi kuhusu hali hiyo na kwamba wana maoni tofuati. Amesema watu hao wamezungumzia kuhusu amani na utulivu na jinsi ambavyo hawahitaji mvutano mwingine.

Chanzo: DW Swahili
 
Back
Top Bottom