Poland yatafakari mpango wa kumiliki silaha za nuclear za kujihami.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Waziri mkuu wa Poland Donald Tusk anasema ni wakati sasa wa Poland kufikiria kuwa na silaha za juu zaidi ya za kawaida ikiwemo silaha za nuclear.

Hatua hii inakuja baada ya Marekani kujiondoa kama mdhamini mkuu wa usalama wa Ulaya pamoja na kuwa na sera zisizotabirika tena katika mahusiano yake na washirika wake mbalimbali.

Donald Tusk amerejelea mfano wa kuvamiwa Ukraine akisema kama wangebaki na silaha zao leo wasingeweza kuvamiwa na Urusi.

Katika hatua za muda mfupi kwa sasa Poland wako katika mazungumzo na Ufaransa kuwa chini ya mpango wao wa ulinzi wa sera ya nuclear.

Screenshot_20250308-170929_X.jpg
 
View attachment 3263801
Sawa, ila Putin nae akiyapa silaha za nyuklia makoloni ya ufaransa wasilalamike
 
Hivi ni kwanin Europe wanamuona Urusi kama threat kubwa sana kwao? Maana NATO ni kwa ajili ya Urusi.

Base za marekani huko ulaya ni dhidi ya Urusi

Hizi nukes wanazoimba sasa hivi ulaya ni kwa ajili ya Urusi

Hii hofu yote inatokanas na nin hasa? Kuna mtu anaweza kunisaidia ufafanusi?
 
Nchi zenye au zilizowahi kuwa na communist ideology first ni dictatorship regimes hence zinaongozwa na "vichaa". Secondly, kichaa ni wa kwenda naye kwa kujihami vilivyo maana hujui next second ataamua nini.
 
wakitoa ufafanuzi nitag mkuu
Nchi zenye au zilizowahi kuwa na communist ideology first ni dictatorship regimes hence zinaongozwa na "vichaa". Secondly, kichaa ni wa kwenda naye kwa kujihami vilivyo maana hujui next second ataamua nini.
 
Urusi ni baba lao kwani nchi zote za ulaya zinamgwaya halafu kumbe nchi zote za ulaya zilikuwa zinajivunia marekani baada ya trump kusema kuwa anafikiria nchi yake kujitoa Nato naona nchi za ulaya zinaanza kujiharishia kwa kuigopa urusi ila hasahasa kiboko yao zaidi ni jasusi mbobezi vladimir putin.
 
Sawa, ila Putin nae akiyapa silaha za nyuklia makoloni ya ufaransa wasilalamike
Awape tu, nyakati zimebadilika, kila mtu sasa amiliki silaha za nyuklia tu, hata Taliban, Iran na Belarus nao wamiliki nuclear.
 
Na sisi raia tupewe bunduki mbilimbili kujilinda
 
Waziri mkuu wa Poland Donald Tusk anasema ni wakati sasa wa Poland kufikiria kuwa na silaha za juu zaidi ya za kawaida ikiwemo silaha za nuclear.

Hatua hii inakuja baada ya Marekani kujiondoa kama mdhamini mkuu wa usalama wa Ulaya pamoja na kuwa na sera zisizotabirika tena katika mahusiano yake na washirika wake mbalimbali.

Donald Tusk amerejelea mfano wa kuvamiwa Ukraine akisema kama wangebaki na silaha zao leo wasingeweza kuvamiwa na Urusi.

Katika hatua za muda mfupi kwa sasa Poland wako katika mazungumzo na Ufaransa kuwa chini ya mpango wao wa ulinzi wa sera ya nuclear.

View attachment 3263801
Nuclear arms race inarejea tena.
 
Hivi ni kwanin Europe wanamuona Urusi kama threat kubwa sana kwao? Maana NATO ni kwa ajili ya Urusi.

Base za marekani huko ulaya ni dhidi ya Urusi

Hizi nukes wanazoimba sasa hivi ulaya ni kwa ajili ya Urusi

Hii hofu yote inatokanas na nin hasa? Kuna mtu anaweza kunisaidia ufafanusi?
Nadhani ndio nchi yenye nguvu kisilaha kuliko yeyote.NA NI HATARI HASWAA.ni dhana yangu.
 
Nchi zenye au zilizowahi kuwa na communist ideology first ni dictatorship regimes hence zinaongozwa na "vichaa". Secondly, kichaa ni wa kwenda naye kwa kujihami vilivyo maana hujui next second ataamua nini.
Safari hii upepo upo kwa vichaa.....mganga wao mzuri kuliko wa hao wanaojiona wazima
 
Hivi ni kwanin Europe wanamuona Urusi kama threat kubwa sana kwao? Maana NATO ni kwa ajili ya Urusi.

Base za marekani huko ulaya ni dhidi ya Urusi

Hizi nukes wanazoimba sasa hivi ulaya ni kwa ajili ya Urusi

Hii hofu yote inatokanas na nin hasa? Kuna mtu anaweza kunisaidia ufafanusi?
Hii ni kutokana na Ukomunisti na vita baridi. Russia ilikuwa inalazimisha mataifa yote jirani yake kufuata sera za ukomunisti na udikteta, ilijenga hadi ukuta kutenga Ujerumani Mashariki na magharibi.
 
Wachapane tu tuone nani mbabe.....sisi tutawauzia chakula na madini, watakuja kupigwa timing na wachina maana alishaanza kujisogeza Africa muda ndo maana hata Marekani kamfata Tshisekedi asaini mkataba wa madini huku akijua hio njia mchina alianza kupita nayo
 
Sio Marekani tena?!
Marekani ilikuja baadae sana, kumbuka Poland ilikuwa nchi ya kwanza kufungua mipaka kwa raia wa Ukraine waliokuwa wanakimbia machafuko. Huyohuyo Poland alitoa vifaa vya kijeshi vya zamani ili tu apatiwe vifaa vya kisasa kutoka Marekani.

Huyo Poland na Uingereza zinaongoza kwa chuki dhidi ya Urusi kuliko mataifa yote Ulaya.
 
Wachapane tu tuone nani mbabe.....sisi tutawauzia chakula na madini, watakuja kupigwa timing na wachina maana alishaanza kujisogeza Africa muda ndo maana hata Marekani kamfata Tshisekedi asaini mkataba wa madini huku akijua hio njia mchina alianza kupita nayo
Nyie hamuwezi kuwauzia chakula kwa sababu bado hata kujilisha wenyewe ni shida, Ukraine yenye vita inauza ngano na mafuta ya kula Africa.
 
Back
Top Bottom