Pole mwanaume uliyeacha malezi ya damu wako ukawekeza kwa demu

Pole mwanaume uliyeacha malezi ya damu wako ukawekeza kwa demu

kataip

Senior Member
Joined
Aug 21, 2013
Posts
145
Reaction score
80
Mwanaume huna muda na wanao, mkeo na watu wako. Umepata neema miaka 10 watoto 4.

Mkeo anawaangalia kwa mapenzi na kukueshimu hana out, dinner wala lunch na wanao hata akikuomba mtoke unasema una kazi nyingi.

Unakutana na wasichana kwenye kazi, semina na vikao nk unavuta unawekeza, out, safari nje ya mkoa nk
Wanao wamekuwa kama yatima na unajisifia wewe kidume!!! Kidume gani wanao hajaanza hata kijitegemea kwa lolote?

Simamieni majukumu yenu kwanza ndipo mtoke acha na story za vijiweni huku nyumba mnaziteketeza na kulaumu wake zenu. Mama watoto athaminiwe.

Kataip nikiwa lindo.
 
kwaiyo unatufokea au? hujui zawadi kubwa unayoweza kumpa mwanao ni kumleta duniani hayo mengine atapambana nayo mwenyewe
 
Mbona simulizi imekaa kama mtu aongea peke yake barabarani?Unayajua madhara ya kuonekana unabwabwaja peke yako barabarani?Teh!
 
uzi mchungu hawawezi kuchangia hata kidogo
 
Watachangiaje wakati wamejisaliti na ukweli mchungu wakiamua wabadilike🥊
 
Back
Top Bottom