Pole sana ewe rafiki yangu mwema

Pole sana ewe rafiki yangu mwema

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
POLE SANA EWE RAFIKI YANGU MWEMA
1732508804121.jpg

Yawezekana ulilala mwili tu ila akili na nafsi yako zilikesha zikiweweseka juu ya hilo jambo unalokabiliana nalo. Moyo na nafsi zimeinama

Yawezekana ulilala ukiwa na maswali mazito yaliyokosa majibu, umeamka ukiwa na maswali yaleyale yasiyokuwa na majibu juu ya hatma yako ya matamanio uitamaniyo kuiishi duniani

Yawezekana maswali hayo umesababishwa na uliyemwamini, yawezekana yametokana na matarajio yako kutokuwa vile ulivyotarajia kabis

Unailazimisha furaha ila haidumu, unajaribu kuonekana uko sawa mbele za watu ila ndani mwako kunafukuta kwelikweli. Ukiwa pekee yako au ukijisahau unaongea huku ukijijibu

Yawezekana changamoto unaijua ilipo ila unaogopa kufanya kitu kwasababu unaogopa kupoteza au kuanza upya. Hutaki kujisahihisha ila unaendelea kujilaumu. Huo ni UGALATIA

Kujilaumu hakutakusaidia kitu kwenye jambo linalohitaji maamuzi. Kujilaumu ni kujiumiza zaidi lawama haindoi tatizo unalokabiliana nalo

Jisahihishe, kisha fanya mabadaliko kuendelea kujilaumu huku ukilialia hakutakusaidia kitu. Fanya kitu katika hilo linalokutesa rafiki yangu.
 
Back
Top Bottom