Pole sana Flora Mbasha, huyo ndo Lucifer

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2015
Posts
1,583
Reaction score
2,702
Watu wanaoona mbali walijua tu kuwa mbio zako ni za sakafuni.

Ulimtenda mumeo na ukataka afungwe, na hata aliposhinda kesi hukuridhika ukaamua kukata rufaa.

Bahati nzuri ulichelewesha ndo ikawa pona pona ya Mbasha lakini lengo lako lilikuwa ni kuhakikisha kuwa mumeo asiye na hatia anafia jela, nakumbuka vyema, ulivyo kuwa umepania Kwa kweli Mbasha alinitia huruma Sana kipindi kile.

Ukamdhalilisha Sana hadi kufikia kuzaa nje ya ndoa yako.

Naam, ilikuwa ni kazi ya Lucifer, jamii nzima imeshakudharau Kwa matendo yako.

Biashara yako ya muziki wa injili haiwezi kuwa na soko tena maana jina lako ni baya Sana mitaani.

Baada ya kukutumia atakavyo Hatimae Lucifer amekubwaga, unakumbuka shuka pamekucha eti unataka kurudiana na mumeo, bahati nzuri naye kashtuka hakutaki kabisa maana hatosahu matendo yako, eti unawafuata wachungaji wakusaidie, Kwa lipi?

Pole Sana dada yangu huyo ndo Lucifer, amekulaghai na kukuacha njia panda.
 
Teh,teh,teh,namshukuru Mungu baba Wa mbinguni aliyeniumba mwanaume! Nawapongeza wadada wanaojitambua,! Kamwe Nazi haiwezi shindana na jiwe... Uzuri na urembo wa mwanamke sio Wa kudumu ubaya Wa mwanaume haujawahi kosa thamani...!! Ivumayo haidumu.. !!! Ni suala la muda tu..!! Utagundua umaarufu hausaidii. Bali huponza...!! Hongera Emanuel Mbasha..muda umeongea endapo hayo ni ya kweli.
 
Kwa hiyo Flora Mbasha kawa jamhuri anakata rufaa kwenye kesi za jinai siku hizi?
 
Eti sio wa kudumu?! Kwendraaaaaaaa
 
"Time heals"walisema.

Mbasha ana subira sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…