Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,702
Ulimtenda mumeo na ukataka afungwe, na hata aliposhinda kesi hukuridhika ukaamua kukata rufaa.
Bahati nzuri ulichelewesha ndo ikawa pona pona ya Mbasha lakini lengo lako lilikuwa ni kuhakikisha kuwa mumeo asiye na hatia anafia jela, nakumbuka vyema, ulivyo kuwa umepania Kwa kweli Mbasha alinitia huruma Sana kipindi kile.
Ukamdhalilisha Sana hadi kufikia kuzaa nje ya ndoa yako.
Naam, ilikuwa ni kazi ya Lucifer, jamii nzima imeshakudharau Kwa matendo yako.
Biashara yako ya muziki wa injili haiwezi kuwa na soko tena maana jina lako ni baya Sana mitaani.
Baada ya kukutumia atakavyo Hatimae Lucifer amekubwaga, unakumbuka shuka pamekucha eti unataka kurudiana na mumeo, bahati nzuri naye kashtuka hakutaki kabisa maana hatosahu matendo yako, eti unawafuata wachungaji wakusaidie, Kwa lipi?
Pole Sana dada yangu huyo ndo Lucifer, amekulaghai na kukuacha njia panda.