Pole sana Flora Mbasha, huyo ndo Lucifer

Pole sana Flora Mbasha, huyo ndo Lucifer

"Tusamehe makosa yetu kama sisi nasi tunavyowasemehe wanaotukosea". Mtu anikosee mara ngapi nimsamhe? Hata saba mara sabini. Mbasha, msamehe mkeo kama unataka kuiona mbingu. Hapa duniani hatuna mji udumuo. Hujui unaondoka lini. Kumbuka kifo hakina kanuni. Ebu jihoji, Je, hujawahi kumkosea mkeo? Basi msamehe. Hakuna mbingu kwa wasiosamehe. Mtaanza tena maisha na Mungu naye atawabariki sana.

Nadhani alimsamehe zamani sana, sema wewe unataka arudie matapishi hilo laweza kua gumu
 
mbasha alikua ananifanya nitokwe machozi kipindi kile, dah
 
hili jukwaa linaitwaje? so ukiingia humu halafu ukakuta fulani kazungumziwa ukasema "haituhusu" unanishangaza.sijui watu wanataka nn kizungumziwe humu,na wakat jina tuu la jukwaa linaonesha ni jukwaa la kuwazungumzia watu maarufu.by the way flora alifanya vitu ovyo sana.
 
Nawashauri warudiane " Alichounganisha Mungu hakuna wa ku kitenga"
Nakumbuka tulikuwa jangwani kwny mikutano ya mwal. Christopher Mwakasege#akasema roho mtakatifu ananiambia kuna watu wana kesi za kusingiziwa mahakamani ,wasimame Mungu amesikia kilio chao anataka kuingilia kati!#
Kati ya wengi waliosimama siku ile pia nilimuona E.mbasha,nae kasimama! Mwakasege aliomba sn!

Nikashangaa haikupita wiki mbili mbasha akashinda ile kesi! Nilibaki na maswali mengi,lkn mwisho nikajisemea Mungu ndo anajua,manaake nikikumbuka tulivyokuwa tunashadadia huku nyuma dah!!!

#nilijifunza kitu kikubwa#
Ndio mjifunZe
 
View attachment 373932 Watu wanaoona mbali walijua tu kuwa mbio zako ni za sakafuni.

Ulimtenda mumeo na ukataka afungwe, na hata aliposhinda kesi hukuridhika ukaamua kukata rufaa.

Bahati nzuri ulichelewesha ndo ikawa pona pona ya Mbasha lakini lengo lako lilikuwa ni kuhakikisha kuwa mumeo asiye na hatia anafia jela, nakumbuka vyema, ulivyo kuwa umepania Kwa kweli Mbasha alinitia huruma Sana kipindi kile.

Ukamdhalilisha Sana hadi kufikia kuzaa nje ya ndoa yako.

Naam, ilikuwa ni kazi ya Lucifer, jamii nzima imeshakudharau Kwa matendo yako.

Biashara yako ya muziki wa injili haiwezi kuwa na soko tena maana jina lako ni baya Sana mitaani.

Baada ya kukutumia atakavyo Hatimae Lucifer amekubwaga, unakumbuka shuka pamekucha eti unataka kurudiana na mumeo, bahati nzuri naye kashtuka hakutaki kabisa maana hatosahu matendo yako, eti unawafuata wachungaji wakusaidie, Kwa lipi?

Pole Sana dada yangu huyo ndo Lucifer, amekulaghai na kukuacha njia panda.
Umenikumbusha mbali sana. Mimi ni mmoja kati wa wanaume wanaomchukia huyu dada kwa maisha yangu yote.

Nitowe angalizo kwa Mbasha kama mume, iwapo anakipenda kifo kimjie mapema basi arudiane na huyo dada.

Amenshindwa polisi, akamshindwa mahakamani, hataweza kumshindwa kuchukua uhai wake wakiwa pamoja ni sawa na kumsukuma mlevi.

Mwanamke aliacha kumtii mungu kama muumba wake pale walipopewa maagizo ktk bustani ya Eden na badala yake akamsikiliza na kumtii nyoka.

Kwangu mimi niliumizwa sana na matendo ya mwanamke yule sijui kwa mwanaume mwenzangu aliyekuwa akishuhudia kila mshale unaolenga kwake.
 
"Tusamehe makosa yetu kama sisi nasi tunavyowasemehe wanaotukosea". Mtu anikosee mara ngapi nimsamhe? Hata saba mara sabini. Mbasha, msamehe mkeo kama unataka kuiona mbingu. Hapa duniani hatuna mji udumuo. Hujui unaondoka lini. Kumbuka kifo hakina kanuni. Ebu jihoji, Je, hujawahi kumkosea mkeo? Basi msamehe. Hakuna mbingu kwa wasiosamehe. Mtaanza tena maisha na Mungu naye atawabariki sana.
Imeandikwa ktk maandiko matakatifu kuwa ugoni ni njia tosha ya kuvunja ndoa ya mkristo tena hakuna msamaha. Kitendo cha mwanamke huyu kuzaa nje ya ndoa ni zaidi ya ugoni.
 
Imeandikwa ktk maandiko matakatifu kuwa ugoni ni njia tosha ya kuvunja ndoa ya mkristo tena hakuna msamaha. Kitendo cha mwanamke huyu kuzaa nje ya ndoa ni zaidi ya ugoni.
Lakini imeandikwa vilevile anayeacha mke asioe na aliyeachika asiolewe. Anayekwenda kinyume chake anahesabika kuwa mzinzi. Mbona huzungumzii kuhusu kusamehe ili nawe usamehe dhambi zako?
 
Lakini imeandikwa vilevile anayeacha mke asioe na aliyeachika asiolewe. Anayekwenda kinyume chake anahesabika kuwa mzinzi. Mbona huzungumzii kuhusu kusamehe ili nawe usamehe dhambi zako?
Mimi namchukulia huyo dada kama gaidi wa ndoa na wakala wa shetani
 
hii kali kama ni kweli kumbe hata mimi wa kwangu kuna siku ataniomba msamaha
 
Nakumbuka tulikuwa jangwani kwny mikutano ya mwal. Christopher Mwakasege#akasema roho mtakatifu ananiambia kuna watu wana kesi za kusingiziwa mahakamani ,wasimame Mungu amesikia kilio chao anataka kuingilia kati!#
Kati ya wengi waliosimama siku ile pia nilimuona E.mbasha,nae kasimama! Mwakasege aliomba sn!

Nikashangaa haikupita wiki mbili mbasha akashinda ile kesi! Nilibaki na maswali mengi,lkn mwisho nikajisemea Mungu ndo anajua,manaake nikikumbuka tulivyokuwa tunashadadia huku nyuma dah!!!

#nilijifunza kitu kikubwa#
Umeona eeee?
 
Inatisha kumsikia mwanamke akimtuhumu baba wa mtoto wake kwenye vyombo vya habari kuwa anambaka na kuwa anatembea na msichana wa kazi.hivi atakuwa anampenda huyo mtoto hasa ukitilia maanani kuwa mtoto huyo hawezi kumbadilisha huyo baba akampata baba mwingine msafi. Kumbe tuhuma hizo ni za uongo zikitoka kwa mtu anayeimba nyimbo za kumsifu mungu.. Mungu ni mwenye huruma tumwombe atupe busara.
 
Its only fools who forget the past……………!
Mbasha kawa kama nyoshi nlikutana nae kwa Kameta producer nikajua binamu yangu Ibetibi toka Goma! Lazima Florah arudishe mpira kwa kipa!
 
Back
Top Bottom