Pole sana mtani, ila iga busara za Uamsho walipoachiwa huru

Miezi 8 si haba. Lakini wako UAMSHO walikaa miaka 9. Kwa hiyo kama kuumia mtani hujawafikia UAMSHO.

Ningefurahi ukawaiga UAMSHO. Hakika wameonesha hekima kubwa toka waachiwe huru. Wamejirudi.

La muhimu ni namna walivyo "behave" walipoachiliwa. Hatukuwasikia wakituambia unayotuambia mtani. Unafikia hata kumuudhi aliyekusamehe! Kwamba hakuna aliyekuhurumia bali umetoka kwa nguvu ya umma? Really? Ipi? Ni nguvu ipi ya umma unafanya kazi kwenye kutoa watu jela lakini inashindwa kuzuia watu wasiende jela? Mtaniii?

Mtani ushakuwa mtu mzima na uzee ushabisha hodi. Haipendezi kila siku uwe wa vituo vya polisi, jela na mahakamani ! Mtani kuna marafiki wa kweli na kuna wapambe! Hebu tusikilize marafiki wa kweli.

Achana na siasa fanya biashara. Na kama siasa ndio biashara yako basi acha siasa za kibabe. Hazilipi kwa kuwa sifa ya ubabe ni sifa ya serikali zoote duniani. Hakuna chombo au mtu anaweza kuwa mbabe kuliko serikali.

Dai chochote kwa kistaarabu utaeleweka. Serikali kuiambia hupoi, mpaka kieleweke, una kiberiti, utafanya nchi iwe Libya, n. k. haifai. Serikali ina uwezo wa kufanya hicho kibiriti kikuchome mwenyewe! Serikali ina uwezo wa kufanya wéwé peke yako uishi kama uko Libya!

Mtani hakuna sifa ya mtu kutembelewa na watu wengi gerezani, Sawa na mgonjwa ajisifie kutembelewa na watu wengi kitandani akiwa wodini It's an illusion! Haimfanyi awe mgonjwa bora kuliko wagonjwa wengine!

Mtani miaka inasonga hairudi nyuma. Na ukweli ni kuwa bado hauna hiyo "nguvu ya umma". Wenye nguvu ya umma hawakamatwi usiku, wakasafirishwa usiku, wakakaa ndani miezi 8 Huku wenzake wanachomudu ni kuvaa t-shirt zenye hukumu!

Sikupenda walichofanya UAMSHO lakini nimependa busara zao baada ya kuachiwa. Ukiziiga utakuwa salama. Ukifuata wapambe basi utatembelewa tena jela. Na hao wapambe watalala na kula makwao wewe ukilia njaa. Jela hakujawahi kuwa kuzuri hivyo sio mahali pakupenda kwenda.

Wenzako wanaokupa moyo Mtani kina Godbless Lema na Tundu Lissu wapo ughaibuni wanakula maisha na kuendesha shughuli zao huku wakilipwa madola kila mwezi. Usiwe mjinga, jua limezama shtuka!

Umelia kwa uchungu sana Mtani kila uliposimulia miezi yako 8 jela, itoshe kusema imekufunza. Ogopa mwanaume kulia kwa kiwango kile tena mbele ya umati akiwa na mke wake kando yake.

Anyway, akili ni nywele!
View attachment 2144111
Acha kupandikiza roho yako ya uoga kwa watu wengine. Kama wewe ni wale wakila wakashiba basi siku imekamilika bila kujali wengine wana hali gani basi wewe kaa kimya, wacha waliozaliwa kwa ajili ya watu wengine wapambane.
 
Hoja ya kwanza... huwezi kulinganisha Uamsho na Mbowe.
Hoja ya pili... yawezekana changamoto za Uamsho ziliisha walipotoka mahakamani.
Hoja ya tatu... changamoto anazosimamia Mbowe bado ni endelevu.
Hoja ya nne... Uamsho hawakuwa threat kwa serikali na ccm
Hoja ya tano... Nchi yetu haina dini
Hoja ya sita... Hivi kesi ya Uamsho nayo iliaanika serikali??
Hoja ya saba... Ni upofu kumwambia mwanasiasa akae kimya wakati yeye, wananchi na wanasiasa wenzake wanajua nguvu yake.
Yes hapa sasa tupo sawa kabisa namimi nampinga huyo jamaa kwa hoja zako nzito kabisa hizi!
 
Soma vizuri nilichoandika. Inawezekana vipi uchukue hela umpe mtu akale bata na familia yake, afu wewe urudi kwako ukilia njaa. Kwanini hizo hela ulizomchangia mtu usizitumie kwa biashara au mambo mengine ya kimaisha!
Hufahàmu uwezo wa Mbowe kifedha,na huko Dubai kesha enda mara nyingi bila michango
 
Bosi Mbowe kesi bado anayo. Yaani ni kama ilivyokuwa kwa Sabaya tu. Sabaya walivyomuachia akasema ataitisha presa conference aseme yote, mhhhh nikajisemea moyoni huyu kaisha. Sasa mshaurini huyu Mwenyekiti wenu wa kikundi cha ngo ajitafakari

..Jamhuri ilishafunga ushahidi, halafu ikasalimu amri.

..Mazingira hayo ndiyo yanayompa confidence Mbowe afanye anavyotaka.

..Kama ni kumkamata tena Mbowe, itabidi Jamhuri ichonge kesi mpya, siyo hii ambayo Kibatala na jopo lake waliisambaratisha.

..Jamhuri wangekuwa na akili wangeondoa kesi kabla Luteni Urio hajatoa ushahidi.

..Hapo ndio wangeweza kum-blackmail Mbowe kwa kumtishia kuwa Urio ana ushahidi mzito dhidi yake.

..Na huku kitaa watu wangekuwa kwenye hatihati wakiamini huenda Urio ana taarifa za ugaidi [ bomb shell ]dhidi ya Mbowe.

Cc Nguruvi3, Erythrocyte
 
Acha story zako. Toka lini ccm wakawa na huruma nakushika sikio.
Ukiona DPP anafuta kesi jua wameshindwa walikurupuka kuficha aibu wanazugia kuifuta eti jamhuri haina nia ya kuendelea swaini sasa kama haina nia kwann wakamate. Huwezi ukamkamata mtu umtie jela miaka then useme huna nia huo ni upuuzi na utoto, toka lini mahakama ikawa na huruma. Kuhusu uhamsho wale walionewa hawana ushahidi hata kama wangewaweka ndani miaka elf 1000 still wasingepata ushahidi. Mbowe katoka kwa biti la USA na sio kwa huruma ya mama ambae alisema anao ushahidi na wenzake wawili washafungwa. Toka lini mahakama ikamsamehe muhalifu tena wa kesi kubwa ugaidi, uhaini?
 
Bosi Mbowe kesi bado anayo. Yaani ni kama ilivyokuwa kwa Sabaya tu. Sabaya walivyomuachia akasema ataitisha presa conference aseme yote, mhhhh nikajisemea moyoni huyu kaisha. Sasa mshaurini huyu Mwenyekiti wenu wa kikundi cha ngo ajitafakari

Ushahidi wa siro na police zake umeshindwa mtia hatia, ushahidi wa sabaya makonda uhitaji torch
 
DPP hajamaliza kusoma kurasa 1500 za mashahidi.
Tusubiri amalize.
Kesi ya kujibu ipo
 
Miezi 8 si haba. Lakini wako UAMSHO walikaa miaka 9. Kwa hiyo kama kuumia mtani hujawafikia UAMSHO.

Ningefurahi ukawaiga UAMSHO. Hakika wameonesha hekima kubwa toka waachiwe huru. Wamejirudi.

La muhimu ni namna walivyo "behave" walipoachiliwa. Hatukuwasikia wakituambia unayotuambia mtani. Unafikia hata kumuudhi aliyekusamehe! Kwamba hakuna aliyekuhurumia bali umetoka kwa nguvu ya umma? Really? Ipi? Ni nguvu ipi ya umma unafanya kazi kwenye kutoa watu jela lakini inashindwa kuzuia watu wasiende jela? Mtaniii?

Mtani ushakuwa mtu mzima na uzee ushabisha hodi. Haipendezi kila siku uwe wa vituo vya polisi, jela na mahakamani ! Mtani kuna marafiki wa kweli na kuna wapambe! Hebu tusikilize marafiki wa kweli.

Achana na siasa fanya biashara. Na kama siasa ndio biashara yako basi acha siasa za kibabe. Hazilipi kwa kuwa sifa ya ubabe ni sifa ya serikali zoote duniani. Hakuna chombo au mtu anaweza kuwa mbabe kuliko serikali.

Dai chochote kwa kistaarabu utaeleweka. Serikali kuiambia hupoi, mpaka kieleweke, una kiberiti, utafanya nchi iwe Libya, n. k. haifai. Serikali ina uwezo wa kufanya hicho kibiriti kikuchome mwenyewe! Serikali ina uwezo wa kufanya wéwé peke yako uishi kama uko Libya!

Mtani hakuna sifa ya mtu kutembelewa na watu wengi gerezani, Sawa na mgonjwa ajisifie kutembelewa na watu wengi kitandani akiwa wodini It's an illusion! Haimfanyi awe mgonjwa bora kuliko wagonjwa wengine!

Mtani miaka inasonga hairudi nyuma. Na ukweli ni kuwa bado hauna hiyo "nguvu ya umma". Wenye nguvu ya umma hawakamatwi usiku, wakasafirishwa usiku, wakakaa ndani miezi 8 Huku wenzake wanachomudu ni kuvaa t-shirt zenye hukumu!

Sikupenda walichofanya UAMSHO lakini nimependa busara zao baada ya kuachiwa. Ukiziiga utakuwa salama. Ukifuata wapambe basi utatembelewa tena jela. Na hao wapambe watalala na kula makwao wewe ukilia njaa. Jela hakujawahi kuwa kuzuri hivyo sio mahali pakupenda kwenda.

Wenzako wanaokupa moyo Mtani kina Godbless Lema na Tundu Lissu wapo ughaibuni wanakula maisha na kuendesha shughuli zao huku wakilipwa madola kila mwezi. Usiwe mjinga, jua limezama shtuka!

Umelia kwa uchungu sana Mtani kila uliposimulia miezi yako 8 jela, itoshe kusema imekufunza. Ogopa mwanaume kulia kwa kiwango kile tena mbele ya umati akiwa na mke wake kando yake.

Anyway, akili ni nywele!
View attachment 2144111
Kama nitakua nimekuelewa vizuri ni kwamba,unacho kisema fundamentalists wa mambo ya kidini, kwa kiswahili watu wenye misimamo mikali ya kidini, tumia vizuri nguvu ya DOLA nao wanatii, sio wao tu bali hadi wafuasi wao, maanake hakuna mfuasi hata mmoja wa UAMSHO aliyefurukuta kwa ajili ya kuwafanya wale watu/masheikh watoke lakini sio kwa Mbowe. Umenipa somo kubwa sana hapa, nimekuelewa vizuri mkuu!
 
Back
Top Bottom