Poleni sana Clouds FM na TV kwa adhabu kali mliyo pewa

Poleni sana Clouds FM na TV kwa adhabu kali mliyo pewa

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Nime sikitishwa sana na adhabu ya kuzima mitambo na kutofanya biashara kwa muda wa siku saba yaani wiki moja kwa kile kilicho elezwa kuwa mlitangaza habari za kweli lakini hamkuwa na mamlaka ya kutangaza. Poleni sana. Habari zile zili tangazwa na vyombo vingine na mitandao ya kijamii na zilitoka kwa watu sahihi. Mpaka sasa walio wafungia hawaja sema kama mlitangaza habari za uwongo.

Adhabu mliyo pewa mkumbuke maneno ya Lissu kuwa hampaswi kushangilia mwingine anapo umizwa kwa kuwa mtesi akisha wamaliza wale anao waumiza atakuja na kwenu pia.

Adhabu mliyo pewa ina waathiri wafanyakazi, wateja wenu ambao ni watazamaji na wasikilizaji. wafanya biashara wanao fanya biashara na ninyi, serikali kukosa kodi kwakuwa hamuwezi kulipa kwa mfano PAYE ya wafanyakazi kwa mwezi wakati hawaja zalisha hivo lazima mkalukuleti kuondoa kodi ya wiki moja na kukosa mapato kutoka kwenye makapuni, kuongezeka kwa gharama bila uzalishaji mfano kulipa umeme, mishahara, kodi nk wakati hamzalishi.

Ni wakati sasa wa vyombo vyote vya habari kujifunza kuwa hakuna aliye salama zaidi ya TBC, UHURU, DAILY NEWS, CHANNEL 10 na vyote vinavyo milikiwa na chama tawala na serikali. Wengine wote mkumbuke mko katika mtego wa panya kuingia waliomo na wasio kuwemo. Kisa hiki wengi hawakijui lakini kinaelezea vizuri haya yaliyo wapata.

Poleni sana na tume wa miss sana.
 
Namwona milad anamsaidia kampeni jiwe.... Daily nin yeye tu na insata
 
watakuwa wamejifunza,
waache kukurupuka na kulopoka ovyo. wakumbuke kuwa wanapo kuwa kwenye matangazo ya tv wanatizamwa hicho sio kijiwe cha kahawa
 
Ila kiukweli kabisa, tunaofanya Biashara kipindi hiki, ni kipindi kigumu kuwahi kushuhudiwa baada ya kile cha Uhujumu Uchumi na Moringe.
 
Ni kama ile habari ya mtu aliyeuawawa na simba aliyekuwa anamfuga!
Hata hivyo ndio maana ya utawala wa sheria.
 
Bashiite hakufukuzwa kazi ali acha mwenyewe
Hao clouds wamezidi kufanya makosa ya kujirudia

Kabla ya hii adhabu week moja kabla walipewa adhabu ya kukifungia kipindi cha jahazi wakasamehewa


Naww usishangilie anguko la wenzako

Mbona mmefurahi bashite kuwa mwananchi wa kawaida
 
Sisi ambao hatujui kilichotokea mnatusaidiaje ili tufahamu ?
Kwani walifanya kosa gani?
Walistahili kula umeme shuwain...
Hao clouds wamezidi kufanya makosa ya kujirudia

Kabla ya hii adhabu week moja kabla walipewa adhabu ya kukifungia kipindi cha jahazi wakasamehewa


Naww usishangilie anguko la wenzako

Mbona mmefurahi bashite kuwa mwananchi wa kawaida
Wangefungiwa maisha tu washenzi hao.
Clouds inatakiwa iwatimue wafanyakazi wawili wanaihujumu kwa kuvunja sheria makusudi
Moja ana upara
Nimepitia comments mbali mbali humu nimeona kuna wengine wana jibu bila kujua kosa linalo daiwa kufanywa na Clouds FM na TV. Heri hata wale walio uliza kuliko wale waliojibu bila kujua kilicho pelekea adhabu hii.
Naomba msome post hii ya Malisa ita wasaidia.

MAMBO MATANO KUHUSU CLOUDS KUFUNGIWA.
1. Clouds wameadhibiwa kwa kutangaza wagombea kupita bila kupingwa. Kwa lugha rahisi wanadaiwa kutoa taarifa kuwa mgonjwa amefariki kabla daktari hajadhibitisha. Lakini je, ni kweli walifanya hivyo?

Wagombea waliopita bila kupingwa walitangazwa na Wasimamizi wa uchaguzi. Clouds walichofanya ni kuripoti tu. Mkurugenzi Ludewa alimtangaza Joseph Kamonga wa CCM kupita bila kupingwa. Mkurugenzi Ruangwa akamtangaza Majaliwa kupita bila kupingwa. Clouds kama chombo cha habari wakaripoti bila kuongeza wala kupunguza neno. Kosa lao ni lipi?

Mkurugenzi ni "credible source" kwenye taarifa zinazohusu uchaguzi. Kama Mkurugenzi amesema fulani kapita bila kupingwa, tulitarajia media ziripotije? Kama kuna makosa yalitendeka waliopaswa kuadhibiwa ni wakurugenzi sio media. Media ni chombo tu cha kufikisha taarifa. Kuiadhibu media na kuiacha source ni uonevu.

2. Vyombo vya habari vilivyoripoti ni vingi. Kwanini Clouds peke yao wameadhibiwa? Uhuru walitoa orodha ya majimbo ambayo CCM imepita bila kupingwa, lakini hawajapewa hata onyo. Double standards.

3. Adhabu waliyopewa Clouds ni kubwa sana. Kwanza hawakustahili adhabu kwa sababu hawajafanya kosa lolote. Lakini hata kama wangekua wamekosea adhabu waliyopewa ni kubwa. Kuzima matangazo kwa siku 7 sio kwamba unaiadhibu Clouds peke yake bali umewaadhibu wasilikizaji na watazamaji wa Clouds pia. Ni vema wangepigwa faini kuliko kufungiwa, maana kufungiwa ni kuadhibu wasikilizaji ambao hawahusiki.

4. TCRA iache umangi-meza. Iweke utaratibu wa rufaa pale inapotoa adhabu kwa vyombo vya habari. Kumuadhibu mtu na kumnyima haki ya kukata rufaa ni ukatili.

5. Clouds wajifunze kupitia hili. Waache kujipendekeza kwa serikali na kwa chama chakavu. Huyo wanayejipendekeza kwake hapendekezeki. Huyo wanayetaka kumfurahisha hafurahii. Ndio maana pamoja na juhudi zote za kuipamba serikali na chama, bado wanagongwa nyundo. Ni wao waliovamiwa na bunduki studio, ni wao waliosababisha Nape akafurushwa kazi kwa kuwatetea, ni wao waliofungiwa kipindi chao pendwa cha Jahazi, na sasa wamezimiwa matangazo kwa wiki nzima. Hivi hawajifunzi tu?

Malisa GJ
 
Back
Top Bottom