Poleni sana mliomwaga damu kwa ajili ya CHADEMA, ukweli mmeuona!

Poleni sana mliomwaga damu kwa ajili ya CHADEMA, ukweli mmeuona!

Tatizo letu. Watanzania tumeichukia Ccm kiasi kwamba hatusomi habari za Ccm isijekuwa baada ya jiwe kuhamia Dodoma ametoa tangazo la nafasi za kazi ya Lumumba buku saba tawi la dodoma na chato
 
Sumaye Jana katoa hoja za kitoto sana, labda ya ile serikali kunyang'anya mashamba yake.
 
Mbowe anafanya siasa za kihuni. Mafioso kabisa jamaa. Eti sumu haionjwi!

Sumaye anayo mengi moyoni; PM mstaafu, anayelindwa na serikali bado ana hofu ya usalama wake toka kundi la Mbowe!! Najaribu kurejea matukio ya vifo na majeruhi wa wanachama wa CDM.....

Mh Mbowe anadai '...safari hii ana kikosi cha hatari...' na watapiga kambi mkoa wa Tanga kwa mafunzo na operesheni maalum. Vikosi vyetu vya usalama wawafuatilie, mapango yalindwe, accounts na biashara za huyu bwana zichunguzwe.......
 
Tukiongea ukweli ni kwamba Mbowe ameharibu CDM. Kuwapokea hawa jamaa na kuwasaliti akina Slaa alisababisha chama kikaangukia pua.

Kwa uchaguz wa 2015 mtu sahihi ambaye angewezana na JPM ni Slaa. Sasa from nowhere Akaja mzee wa blich la kikongo akapewa kugombea urais ilihali tunatambua wazi yeye na wazir mkuu mwenzie walikuja kutafuta tu madaraka na walipoyakosa matokeo yake ndo hayo.

Mbowe asipobadili mtazamo naiona ACT ikinyemelea kuwa chama kikuu cha upinzani.
 
Great thinkers!

Hii ni thread kwa ajili ya wana CHADEMA asili waliomwaga damu na kuipigania.

Naamini mmeshagundua utapeli katika Chama hiki chini ya Mwenyekiti wake.
Chadema ni watu walioamua kusakatonge nje ya CCM

Mbowe ameiua Chadema kwa Tamaa za ruzuku na shortcut ya mabadiliko kupitia Lowassa
Yaan chama kilichokuwa kinara wa kupinga ufisadi kikakaribisha mafisadi na kuyapa nafasi nyeti za kugombea urais, hii kamari aliyebet Mbowe imejibu sasa!

Chadema ya 2014 kushuka chini ilikuwa inaaminika mno lakini sasa hivi dah hapa Shinyanga tu ni aibu

Nimeamini Zito na Kitila kumbe ni kweli walitolewa kafara zababu ya uenyekiti tukarubuniwa eti ni wasaliti

Hata yanayosemwa kuhusu Wangwe nimeyaamini, umwenyekiti Chadema ni kaa la moto/sumu
 
Maoni yangu yana base kabla hata Kubenea hajaingia Chadema...tuliza mzuka unisome vyema...mimi sio mtu wa kufuata mafuriko

Mhhh mkuu nasikia Kubenea alimwagiwa tindikali tupe story. Tusiende mbali mwandishi mwangosi ilikuwakuwa je?
 
Rubbish.......

Tambua mkuu Meningitis, waliomwaga damu katika Chadema, wamefanya hivyo kutokana na udikteta wa Mwenyekiti wako Jiwe......

Kuna aliyemwaga damu zaidi ya Jiwe katika nchi hii??
 
1000 digits,
Sina shaka sana na maoni yako, lakini unaonekana unajenga hoja kwa mambo ya ukweli unachanganya na propaganda. Ni sawa na kupika wali mzuri, mtamu na unaonukia sana, lakini una mawe. Sina hakika wali wa hivyo kama utalika pamoja na kwamba ni mtamu. Jaribu kutenga propaganda na ukweli tujue unasimamia kipi, kinyume na hapo itakuwa ni chuki binafsi, hata kama kuna ukweli fulani humo ndani ya maelezo yako.
 
Meningitis umeisha nunuliwa kamanda??
Sio wewe au umeondoka na Boss wako Sumaye ili ukaunge mkono!!
Ndio maana tunawastukia, njaa mbaya saana.
M4 C inasonga mbele ikiongozwa na kamanda Mbowe.
Mchujo unaendelea mtaisha wote mapandikizi wa Lumumba!!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
meningitis, Yaani Jiwe atuulie ndugu zetu lawama tumpe Mbowe?
Mnapoleta hoja za ushindani wa kisiasa msiingize maneno yenye kukumbusha hisia za majonzi.
Hivi maneno hayo waweza kuwaambia wazazi wa Ben? Au mke wa Azory?
Usirudie tena kuleta hoja za aina hii maana zinatukwaza sana
 
mangyi,

Kwa hili uko sahihi kabisa. Sioni aibu kukiri ukweli wa hiki ulichokisema.
 
Back
Top Bottom