Poleni sana wamachinga, hiyo ndiyo CCM haijawahi kubadilika

Yaani hawa wanovunjiwa na kusema hawajui kitu ni wapuuzi, inabidi wavijenge na wawasubiri hao wanaobomoa...

Watu Mia wanatosha kabisa kuishikisha adabu serikali
 
Hapa naona busara inapaswa itumike, kwanza kwa kukutanana na viongozi wa Machinga ili kuongelea kuhusu kuhamishiwa katika maeneo mapya watakayopangiwa. Pili bado wapewe muda wa kutosha ili waweze kujipanga kuondoka, ikiwezekana mpaka ifikapo mwisho wa mwaka.
 
Ajira huto,,utaratibu huufuati na kwa bahati mbaya hata vyama vya upinzani haviwasaidii
 
Aina yetu ya uchumi ndio inazalisha watu wa aina hiyo
 
Hii nchi imeyumba sana, sijui tunaelekea wapi?
 
Mie nilizoe kuwa ukisikia machinga Basi ni yule anazunguka na bidhaa kidogo,pengine heleni,nguo mitumba nk.Lakini siku hizi unakuta machinga kajenga Banda kaweka bidhaa Kama Duka vile lakini naye Ni machinga
 
20000 ndio izuie serikali kufanya Mambo yake? Waulize Kimara waliobomolewa nyumba zao
 
Machinga anatembea na bidhaa zake,Sasa Mali zipi zimeibiwa?
 
Kwa hiyo ccm haina directory?inajiongoza kama mbuzi asiye na kamba!
Hivi unajua maana ya demokrasia?

Ila si shangai na ndio maana kwa demokrasia yetu,wanasiasa hawapo huru kwenye vyama vyao, wakiwa na mitizamo tofauti CCM utasikia "hana adabu....... mtovu wa nidhamu.......".

Ukiwa upinzani unaitwa "msaliti........ mara kanunuliwa ".

Yaani demokrasia yetu ndani ya hivi vyama sizani kama kuna mgongano wa mawazo kwani baadhi wa viongozi ambao wanajifanya miungu watu hawapendi kupingwa.

So kuwa ndani ya hivi vyama haina maana kwamba hautakuwa na mtizamo binafsi.
 
Kuna mijitu ikihemkwa haina hata muda wa kutafakari. Yanaweza kuhamaki na kitu ambacho wala hayajelewa. Haya tunayaita mabongolala.mara nyingi hatuyasaidii, unayaacha kama yalivyo.Unayajulisha tu kuwa ni mabongolala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…