Poleni Watanganyika, Umakamu wa Rais umewalazimu muwe watulivu

Nimemuelewa Nyerere alichokuwa anataka kukisema. Ila mfano wake nadhani haukuwa mfano bora...
Ametoa mifano mingi kwa muktadha tofauti, kwa mfano, mfano wa US states kuwa na state rights unaweza kuwa sawa kwa muktadha huo wa kila state kuwa na state rights, lakini ukiuweka katika habari ya Tanzania kwenye states mbili moja kubw a moja ndogo kwa ardhi na watu unakuwa si sawa.
 
Nani kakwambia Mzee Mwinyi Ni Mzanzibari?
 
Hivi kuna muungano gani mwingine hapa duniani ambao unafanana na huu wa kwetu?

United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland? Maybe?
 
Bahati mbaya huwajui wazenji vizuri hasa wapemba ni noma kwa swala la akili za darasani huwezi kujifananisha nao hata kidogo

Kwa wale wanao wafahamu vizuri watu hawa ikitokea mnasoma darasan moja na mpemba basi jua atawakimbiza darasani vibaya sana

Hawa watu ikitokea anaipenda shule basi huwa wana akili sana darasani fanya tathmini au uliza walio bahatika kusoma na wapemba darasa moja watakwambia

Hakunaga mpemba mzembe darasani
 
Ndio mana Hua mnaambiwa wazenj ni wabaguzi aisee, mbona hicho kitu unachowaza , sisi hatujawahi kukiwaza hta Siku moja , acha kuteseka mkuu
 
Muungano wa Serikali mbili ndio unaifanya Zanzibar kuwa 'mkoa Maalum' kuliko ambavyo ingekua Serikali tatu

Katika Serikali mbili, Serikali ya Muungano ambayo ina mamlaka makubwa juu ya Zanzibar, practically ndio Serikali ya Tanganyika, mawaziri wabunge, vombo vya usalama, mahakama ambavyo ni vya Serikali ya Muungano vyote Zanzibar ina nguvu kidogo sana.

Serikali tatu ina ,maana Tanganyika ingekuwa na Serikali yake, yenye vyombo vyake ambavyo vina mamlakaTanganyika pekee, na Zanzibar vivyo hivyo, kishakungekuwa na Serikali ya Muungano ambayo ingeshughulikia mambo ambayo ni selected ambayo yangeifanya kuwa na nguvu kiasi fulani na huku kila nchi ikiwa haijamezwa na mwenzake
 
Nyerere anafananisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama United States, sasa United States zile state zina state government na kisha kuna federal government

Sasa kwa case ya Tanganyika na Zanzibar, mbona hakuna state government ya Tanganyika?
Wewe unaanza kunielewa ,na unaanza kuja kwenye kiini cha mjadala.
Mungu akuongezee ufahamu na uwezo wa kupembua yaliyo nyuma ya pazia.
Hii ndiyo mantiki faida yake,.
Nyerere kasema "There is no country smaller than the other in sovereignty term"
"Zanzibar was a sovereign and Tanganyika was a sovereign no county is small in Union maters."
 
Natowa Pongezi kwa Ndugu Mpango kwa kuukwaa umakamo wa Raisi,
Ni chaguo jema na zuri
Chaguo lenye Kuleta matumaini kwa Taifa
Hongera mama Samia, Raisi Wangu wa Jamuhuri ya Muungano, Tanzania
 
Kwa kweli
 
1. Zanzibar si mkoa maalum, ni semi-autonomuous part of a union.
2.Serikali ya Muungano ina mamlaka kuhusu Zanzibar kwenye mambo machache tu yaliyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
3.Hakuna serikali ya Tanganyika.
 
Hivi kuna muungano gani mwingine hapa duniani ambao unafanana na huu wa kwetu?

United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland? Maybe?
Kinda sorta but not quite.

Sisi tumeua Tanganyika, wao England bado ipo.
 
Hao wanaomchukia ulikua na ushahidi madhubuti Kama walikua wanaomchukia?
Basi tafuta sababu ujue kwa Nini walikua hivyo,
Unadhani manji angempenda?
Lissu,
Familia ya Ben saa 8
Familia ya Erick kabenderA,
Orodha ni ndefu,
Watumishi wa umma nao walikua na sababu,katika utumishi wa umma,kisheria Kila mwaka walistahili kupata nyongeza,kwa mujibu wa Sheria,sio kwa hisani ya mtu Fulani,nA mwishoe hizo nyongeza ndio Zina determine akistaafu apewe mafao kiasi gani,Sasa Kama hajaongezewa maana yake akistaafu atapewa mafao kidogo, vaa koti la watumishi wa umma halafu ndio utoe comments
 
Mama atolewe ukomo wa utawala! Katiba ibadilishwe atawale milele! Hata asipotaka tutamlazimisha!
Naona mnataka kazi irudiwe tena. Waliotuletea demokrasia hawataki ujinga huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…