Polepole: Agenda ya uteuzi wa Samia ni Res Judicata kwa sasa

Polepole: Agenda ya uteuzi wa Samia ni Res Judicata kwa sasa

Katika desturi za kimahakama, uamuzi ukisha fikiwa baina ya watu wawili kuhusu shauri fulani, mahakama hiyo hiyo hairuhusiwi tena kurudia kulisikiliza shauri hilo hilo baina ya watu hao hao tena. Hiyo ndio maana ya Res judicata.

Sasa hivi CCM tayari tuna mgombea urais, Dkt Samia, mchakato majimboni umepamba moto, uteuzi wa madiwani ndio unaelekea tamati. Ni ukweli uliowazi kuwa sasa haiwezekani kurudia huu mchakato. Kupinga uamuzi wa mkutano mkuu kumteua Dkt Samia sasa hivi ni usaliti. Samia ni mgombea wa CCM na wana CCM wote lazima tumtetee.

Ni ukweli, kukosoa, kujikosoa na kukosoana ni nyenzo ya mapinduzi, lakini wakati gani, mahali gani na kwa njia gani hilo linafanyika ni jambo la muhimu pia. Hili lisipozingatiwa tutashindwa kutofautisha kati ya kukosoana na kushambuliana.

Jambo la muhimu kwa sasa ni kuona ni namna gani tutavuka kivuko cha uchaguzi bila kupoteza umoja wa kitaifa, amani na utulivu wetu.
Usijitoe akili, kama uteuzi wake haukufuata Katiba ya Jamhuri ya Muungano, vipi akiwekewa pingamizi na wagombea wengine wa Urais huko mbeleni?

Kinachotakiwa ni CCM kutathimini huo mchakato kwa uweledi then kichukue hatua sahihi.
Kama ni mchakato halali basi kiseme kikiwa backed na vifungu vya Sheria na kama ni batili basi mchakato urudiwe.
CCM iache kuendeshwa kichawa chawa!
 
Res Judicata imeeleweka kikamilifu. polepole na kikundi chake cha kuendeleza hila walizotaka Mama yetu Mh. Rais SSH asiapishwe kuwa Rais hawatafanikiwa na wataaibika na kufadhaika kunako Oktoba 2025.
Hawezi kufadhaika, HHP hana mpango wa kumkwamisha mama yenu ila Mungu aliye hai ndio hataki akilazimisha kwa mtazamo wa kibinadamu utabatilishwa kwa fedheha......Mark my words with precise impact
 
Back
Top Bottom