SI KWELI PreGE2025 Polepole amesema CCM ni chama imara, kitashinda uchaguzi mkuu kwa kishindo

SI KWELI PreGE2025 Polepole amesema CCM ni chama imara, kitashinda uchaguzi mkuu kwa kishindo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-07-21_09-03-51.jpg
 
Tunachokijua
Balozi Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba.

Mnamo mwezi Julai 13, 2025 Polepole, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram alichapisha barua iliyotoa taarifa ya kujiuzulu nafasi ya ubalozi, ambapo kabla ya Taarifa hiyo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Leo tarehe 18, Julai 2025 Balozi polepole amefanya mkutano na waandishi wa habari mbashara kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo awali alifafanua kuwa mkutano huo ni kwa ajili ya kufafanua barua ya kujiuzulu aliyomuandikia Rais.

"Nitaifafanua barua niliyomuandikia Mhe. Rais kwa hatua na kwa maana njema ili kuondoa upotoshaji"


Taarifa inayomhusisha Polepole


Baada ya mkutano huo, baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wamekuwa wakisambaza taarifa iliyotumia utambulisho wa grafiki za Carry Mastory, kuwa Polepole amesema 'CCM ni chama imara, kitashinda uchaguzi mkuu kwa kishindo'

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu, pamoja na marejeo ya video, umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani kauli hiyo haijatolewa na Polepole katika mkutano wake.

Aidha grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa na Carry Mastory kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, bali imetengenezwa na wapotoshaji kusambaza taarifa isiyo ya kweli.

Kupitia mkutano wake na waandishi habari pamoja na mambo mengine Polepole amekosoa vikali kuhusu mchakato mchakato wa kumpata mgombea wa Urais pamoja na makamu wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akisema 'Wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Mchakato wa kupata wagombea tumeukosea'

"Unajua wakati mwingine lazima tubomoe ili tujenge mimi mkristo kuna mstari unasema wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Huu mchakato wa kupata wagombe kwa kweli tumeukosea"



View: https://www.facebook.com/hpolepole/videos/1035169325065298​
Back
Top Bottom