SI KWELI PreGE2025 Polepole amesema twende tukashiriki uchaguzi mkuu kwa utulivu na mshikamano

SI KWELI PreGE2025 Polepole amesema twende tukashiriki uchaguzi mkuu kwa utulivu na mshikamano

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-07-21_09-05-32.jpg
 
Tunachokijua
Balozi Humphrey Polepole ni wanasiasa na mwanadiplomasia kutokea nchini Tanzania ambaye amaye amewahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya chama cha mapinduzi (CCM), mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzani na Balozi wa Tanzania nchini Malawi na baadaye Cuba.

Mnamo mwezi Julai 13, 2025 Polepole, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram alichapisha barua iliyotoa taarifa ya kujiuzulu nafasi ya ubalozi, ambapo kabla ya Taarifa hiyo alikuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Leo tarehe 18, Julai 2025 Balozi polepole amefanya mkutano na waandishi wa habari mbashara kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo awali alifafanua kuwa mkutano huo ni kwa ajili ya kufafanua barua ya kujiuzulu aliyomuandikia Rais.

"Nitaifafanua barua niliyomuandikia Mhe. Rais kwa hatua na kwa maana njema ili kuondoa upotoshaji"


Taarifa inayomhusisha Polepole

Baada ya mkutano huo, Ipo taarifa inayosambazwa katika mtandao wa Facebook, ikitumia utambulisho wa grafiki za Jambo TV, kuwa Balozi Polepole amesema 'twende tukashiriki uchaguzi mkuu kwa utulivu na mshikamano'


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani kauli hiyo haijatolewa na Polepole kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa na Jambo TV, bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji ili kusambaza Taarifa isiyo ya kweli.

Aidha Polepole kupitia mkutano wake na waandishi habari pamoja na mambo mengine amekosoa vikali kuhusu mchakato mchakato wa kumpata mgombea wa Urais pamoja na makamu wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo amesema,

"Hii lugha ya kusema mgombea ni mmoja ni makosa, sio kipindi hiki, hata kipindi cha Magufuli kuna baadhi ya viongozi walikuwa wanasema mgombea ni mmoja, siyo kweli na kwenye kauli rasmi ambayo mimi kwa wakati ule niliitoa kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM.

Tulisema tunafungua kwa watu wote hakuna fomu moja, lazima fomu zichukuliwe, lazima fomu zirudishwe na wadhamini, unyenyekevu, msingi wa chama chetu, tunaanza vikao... nilishindwa hata kuwapongeza, Unapongeza vipi kisicho halali?"

"
Unajua wakati mwingine lazima tubomoe ili tujenge mimi mkristo kuna mstari unasema wakati mwingine inabidi tubomoe ili tujenge. Huu mchakato wa kupata wagombe kwa kweli tumeukosea"

View: https://www.facebook.com/hpolepole/videos/1035169325065298​
Back
Top Bottom