Polepole apinga utaratibu wa kuwahamisha machinga, amuonya RC Dar. Ashutumu mikopo kusababisha utegemezi

Polepole apinga utaratibu wa kuwahamisha machinga, amuonya RC Dar. Ashutumu mikopo kusababisha utegemezi

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Mkufunzi wa shule ya uongozi Eng. Humprey Polepole amevishutumu vyombo vya kibeberu IMF na World Bank kwa kusababisha umasikini mkubwa na utegemezi wa milele kwa kutoa mikopo kandamizi kwa nchi masikini Kama Tanzania na ameionya Serikali iliyopo madarakani kuwa makini na mikopo hiyo.

Wananchi wa Kenya waliandamana kupinga mkopo uliokopwa IMF nchini Kwao Ila hata Tanzania juzi imekopeshwa mkopo mkubwa wa Tsh 1.3 trilioni na pole pole anasema huko ni kuingia katika mdomo wa mamba yaani ukoloni mamboleo chini ya mabeberu.

Mkufunzi huyo mzalendo ambaye alidai serikali imepigwa photocopy alienda mbali na kumkemea Amos makala RC wa Dar kuwa aache kunyanyasa masikini wamachinga, Bali atende haki. Huyu hapo chini

 
Kwa hisani ya Shule huru ya uongozi
20210925_212012.jpg
 
Polepole analialia aada kukosa madaraka.
Alishhiriki sana uonevu na madhila mengi yaliyofanyika kipindi cha Mwendazake.

Hana moral authorityn ya kusema sasa wakati alinyamaza na kushiriki maovu ya awamu iliyopita.

Alishiriki kununua wapizani
Alishiriki au hakukemea utekaji, watu kupotea, kuokotwa maiti beach, kuonewa kwa wapinzani nk.

Alisema anataka kuwafunza watanzania adabu akijua atakuwepo kwen poower xycles muda mrefu.

Huyunalishiriki kuharibu uchaguzi tangu uchaguzi wa serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu.

Mzee wa Veite!!

Analeta tu chokochoko kwa Raisi SSH hana jingine.

Namshauri aridhike na ubunge wa kuteuliwa au areje kudaibserikali tatu anazoamini aje hukun tudai katiba mpya.
 
Polepole the genius.
U Genius wake ni upi? Nakumbuka aliwahi sema bila katiba mpya uwajibikaji hauwezi patikana je alipokua Mbunge aliwahi dai katiba tena??

Aliwahi sema CCM haijawahi shinda uchaguzi kwa uhuru na haki lakini alipokua katibu muenezi alifanya nni kuhakikisha CCM inashinda kupitia chaguzu huru na haki??

Aliwahi sema vyeo kma ma DC havifai zaidi ya kulipana fadhila!! Mbona alipoteuliwa kuwa DC wa ubungo hakukataa teuzi??

Ni hivi Polepole anaongea haya baada ya kuona hana chake serikali hii, ila kama issue ni mikopo mbona alikua anatetea deni la taifa lilipokua linaongezeka kipindi cha JPM kwa hoja kwamba lina jenga nchi kupitia miundombinu??? Leo hii kwa Mama haangalii faida ya mkopo ila anaangalia implications zake kwenye ukoloni mamboleo?? Kwanini hizi double standards??

This man is not a genius ni mnafiki tu, leo akirudishwa serikalini trust me atakua wa kwanza kusifia chanjo na tozo!!
 
Back
Top Bottom