Polepole apuuzwa na Watanzania na kuonekana ni mnafiki na mbaguzi

Amepuuzwa na Watanzania lakini wewe Mrundi unamfungulia uzi kila siku!
 
Polepole ni kirusi ndani ya CCM
Moja ya watu wachache sana ambao ni pro Samia ambao wanafikiri vyema ni wewe, sasa unaposema Polepole ni kirusi bila ya kusema ukirusi wake, napata shida kuendelea kukuweka kwenye kundi la wachache wanaojitambua walio pro Samia.
 
Moja ya watu wachache sana ambao ni pro Samia ambao wanafikiri vyema ni wewe, sasa unaposema Polepole ni kirusi bila ya kusema ukirusi wake, napata shida kuendelea kukuweka kwenye kundi la wachache wanaojitambua walio pro Samia.
Kwani wewe huelewi unafiki na ukirusi wa polepole ndani ya CCM :?
 
Ni kupoteza muda hata kulisoma, maana na mwandishi mwenyewe anajua kuwa it is vice versa of what he is trying to depict. Balozi HPP is our hero and the voice of the voiceless. God bless HPP !
Kama polepole ni heri basi ma hero wamekwisha hapa Duniani
 
Mbona Samia kapuuzwa tangu 2021 naona anaforce fame kwa kuua watu lakin bado hatusemi.
 
NOSENSE
 
We mpumbavu na,chawa unajua kwanza maana ya wa Tanzania? au unawashwa sasa unataka mikuno! jinga kabisa ww
 
Sote tunajua kuwa kwenye demokrasia ya kweli, sifa si jambo la lazima bali ni matokeo ya utendaji. Serikali haishangiliwi kwa maneno ya watu kama wewe bali kwa matendo yanayogusa maisha ya mamilioni ya Watanzania waliokata tamaa kutokana na mfumo wa kifisadi, wa kimabavu na wa kinyonyaji.

Unaposema “Watanzania wa leo siyo wa 1961,” ni kweli. Hivyo basi usidhani unaweza kuwapaka matope viongozi wanaothubutu kusema ukweli, halafu ukatuzubaisha kwa porojo za kupuliza manukato juu ya kinyesi.

1. Kumtetea Rais kwa Misingi ya Kibaguzi

Kumuita Rais "aliyepewa kibali na Mungu” ni ujinga wa kidini. Urais si upako, ni mkataba wa kijamii wa kuwajibika kwa wananchi. Kama Rais Samia ni mbarikiwa, basi afanye kazi ya Mungu: kupambana na rushwa, kusikiliza wakulima, kulinda uhuru wa maoni na haki za vyama vya siasa. Lakini yeye anapambana na vyama vya upinzani, ananyamazisha sauti huru, anaunda Tume ya Uchaguzi bila maridhiano – hiyo ndiyo baraka?

2. Kwa Nini Mnaogopa Kukosolewa?

Polepole hakusema chochote ambacho hakipo kwenye Katiba ya CCM au historia ya chama. Aliuliza: Je, ni kikao gani kilichompitisha Rais Samia kuwa mgombea wa CCM? Hili ni swali la msingi kwa chama kinachodai kuheshimu katiba. Kama hamna jibu, basi jibu si matusi wala kumzulia chuki, ni KUKIRI KOSA na KUREKEBISHA.

3. "Watanzania Wamempuuza Polepole" Ni Wapi?

Hivi unavyosema "hakuna anayemjadili," mbona kila kona ya nchi watu wanazungumzia ujasiri wake na hoja zake? Kwanini viongozi wa serikali na chama wanatapatapa kila siku kutoa majibu na kutafuta matusi mapya? Unapuuza mtu halafu unamwandalia mikutano ya kumjibu? Una akili kweli au unatumia ubongo wa CCM?

4. Kazi Iendelee – Wizi Uendelee?

Unasema “Kazi iendelee” lakini hujiulizi kazi gani?

Ni kazi ya polisi kubambikizia kesi wapinzani?

Ni kazi ya Tume ya Uchaguzi kufuta wagombea halali bila sababu?

Ni kazi ya kuendelea kusaini mikataba ya hovyo kama ule wa Bandari bila ridhaa ya wananchi?

Au ni kazi ya “kupongezana” kila siku huku mamilioni wakilala njaa?

5. Mama Anatosha au Tumechoka?

Mama anaweza kuwa na nia njema, lakini anaongozwa na maamuzi mabaya na washauri wa hovyo kama ninyi "wachawa." Kama mnampenda kweli, basi msimsifie uongo. Mwambieni ukweli: Taifa linataka uchaguzi huru, Tume huru, mahakama isiyo ya chama, na demokrasia ya kweli. Akitii, atatukuka. Akikaidi, ataumbuliwa.

6. Uchaguzi wa 2025 Unakuja – Hakuna Kulala

Sasa hivi nchi imeshachoka kupakwa mafuta ya chooni kuwa harufu ni nzuri. Wabunge wa upinzani wanapigwa risasi, mahakama zinageuzwa matawi ya CCM, huku wachache kama wewe mkifanya kazi ya kuhalalisha dhuluma kwa majigambo ya kijinga. Lakini msidanganyike, hasira ya wananchi haizuiliki kwa kelele zenu za mdomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…